Leo katika hotuba ya Rais,alikua akitamka kwa sifa kua serikali inawalipa madaktari hela nyingi Tshs 900,000.Ila Laki tisa,ukikata PPF,PAYE inabaki kama TShs 550,000.Ukiangalia Dr anasoma miaka 5,anafanya kazi za riak kubwa sanaMbunge au waziri anapewa maslahi mazito sana,wengi hata ulinzi baada ya kustafu wanapewa.We unampa Dr mshahara net laki tano na nusu unategemea awe na umakini kwkazini.
Matatizo hapa sio kwamba 900000 hazitoshi kwa kazi ya madaktari. Tatizo ni pale messenger wa BOT, TRA, etc analipwa zaidi ya hizo. Wao serikali inazipata wapi? tatizo ni pale a lazy Procurement officer (Store keeper) wanapompa TShs 300000 (officially) halafu anamiliki mali za mamilioni bila kuonekana kuwa ni tatizo. Tatizo ni pale Regional traffic Officer anapojenga kitegauchumi worth billions bila mtu kumuwajibisha wakati rushwa kwa hawa trafic inadaiwa na kutolewa waziwazi!
Kimsingi, madai ya madaktari yanawakilisha dukuduku kubwa la matatizo ya mfumo usiowajibika na wa kulindana katika kufuja rasilmali za taifa na matumizi mabaya ya pesa za mlipakodi. Hii inafanyika waziwazi na hakuna dalili yoyote mbeleni inayoonyesha kuna nia ya dhati ya kuondoa madhila haya. Kinachoudhi, ni maneno yanayotumika kuelezea kinachofanyika kupambana na haya maovu.
- Kusingizia utatuaji wa matatizo kufuata utawala bora ambao wote tunajua haupo kwani waliopewa dhamana ya huo utawala ndio wakosaji
- Kusingizia kufuata utawala wa sheria wakati kila mtu anajua mahakama zetu sio huru na ni sehemu ya huo uozo
- Kutumia vibaya vyombo vya dola kukandamiza haki za raia.
Kwa hiyo kila Mtanzania anadai chake kwa kuwa inaonekana huo uwezo wa kulipa una matabaka. Wako wanaojiona wana haki zaidi ya kufaidi keki ya taifa zidi ya wengine. Hii itakapoondoka na/au kuonekana kuwa inashughulikiwa kwa dhati, wengine watavuta subira kwani muda utakuwa mfupi na kila mtu atapata kinachowezekana kwa haki ya taaluma yake.
Hotuba ya Mh. Rais ingeambatana na kuueleza uma serikali inafanya nini kuongeza uwezo wao kuwalipa wataalamu wake, hasa hasa, kwenye kubana matumizi makubwa ya serikali, kuwabana wabadhirifu na kuwachukulia hatua kali (pamoja na kurudisha walichoiba). Haya yanaweza kuongeza uwezo wa serikali kulipa wataalamu wake bila hata kuongeza uzalishaji! Juhudi za kuongeza tija katika uzalishaji ndizo zitaonyesha uhalisia wa kukua kwa hali ya Taifa kiuchumi.
Kwa maoni yangu, walichoanzisha Madaktari ni mwanzo wa kuanguka serikali kama haitakuwa makini. Walimu wana madai hayo hayo; manesi nao hivyo hivyo, Polisi (wasiokuwa makachero au trafiki) wanasota sana na ndio sababu wasipowasilisha mgawo kwa wakubwa wanatishiwa kupelekwa kikosi cha FFU, mbwa au farasi. Nchi italipuka wote wakigoma. Naona Serikali imecheza kamari kwa kutegemea kudra za mwenyezi Mungu na Walimu wasigome kwa mtindo wa madaktari. Vyovyote vile iwavyo, siku chache za mbaleni zitakuwa na changamoto nyingi kwa watawala. Nawaomba wasitumie nguvu ya dola bali busara.