Naam,
Yameshasemwa na kuzungumza mengi yamezungumzwa kuhusu mishahara ya watumishi. Mengi yakiwa ya kukatisha tamaa, kusuta, kuonya na kuudhi kwa wakati mmoja.
1) kwamba, akiwa kilimanjaro kwenye may mosi mkuu wa nchi alisema angeongeza mishahara kwa mujibu wa sheria . Siku zikapita hakuna kitu huku watumishi wa umma wakiwa kimya.
2) kwamba, akiwa huko unguja kwenye kilele cha kuzima mwenge alisema anmetenga pesa kwa ajili ya kuongeza mishahara ya watumishi na akawataja kwa idadi kuwa (59,000) wangeongezewa mwezi huu. Watumishi wakaendelea kusubir .
3) kwamba, akiwa kwenye sherehe za ALAT hapo tarehe 3/10/2017 aliwananga watumishi kwamba hatoongeza ndululu hadi hapo uzalishaji utakapo ongezeka! Pamoja na kuongea kwa ubabe lakini mtaalamu huyu wa mahesabu alishindwa kuwambia watumishi wake huo uzalishaji anaosema utaanzia wapi hadi wapi? ( bench mark) akaishia kupiga mikwara bila aibu
Jana mishahara imetoka kwa waliowengi. Tukumbushane hapa je kuna nyongeza yeyote ya mishahara kwa watumishi wa umma au zile zilikuwa ngonjera kama za makinikia?
My take; aja ya mja kunena na kuhoji sio ukosefu wa uzalendo wala uasi kwa taifa. Watumishi twambizane, tumeongezewa au tumepigwa chenga?