kifinga
JF-Expert Member
- Dec 5, 2011
- 5,249
- 9,499
Pole mkuu umeandika kwa uchungu sanaHakuna mtu au waziri simpendi kama huyu mama Wa utumishi. Huyu mama alipoulizwa bungeni kuhusu ongezeko la mishahara alikuja na mbwembwe nyingi kusoma matrioni ya pesa na kusema serikali itaongeza mshahara. Miezi imepita hakuna la nyongeza yeyote. Hivi huyu mama anaona watumishi ni vikaragosi kila siku kuwahadaa kwa majibu yake ambayo hayatekelezeki.
Bunge la mwisho hivyo hivyo akaulizwa na akaja na majibu Yale Yale na ahadi ya increment mwisho wa mwezi huu. Mshahara umetoka lakini hakuna chochote zaidi ya kuwaongezea hasira watumishi.
Akiwa anajibu hoja anakuja na majibu yenye mihemko lakini mwisho ya siku hakuna linalotokea. Hivi hawa wanahitaji watumishi waandamane ndio wajue watu wamechoka ahadi amabazo zilitakiwa zitekelezwe bila hata ya kutokea adha yeyote. Hivi hata hizi increments ambazo ni haki ya mtumishi nazo kuzipata mpaka watu wagome.
Serikali hii iliahidi kutatua kero za watumishi ila imeshindwa zaidi imezidi kuongeza matatizo na kupunguza ari ya watumishi kufanya kazi. Wameongeza 15% na hii imekuwa ni tatizo ukizingatia kuwa mishahara yenyewe ni duni.
Mpaka hapa hii inaashiria kuwa serikali hii haiwezi tatua matatizo ya wananchi wake . Ikiwa imeshindwa kutatua matatizo ya watumishi ambao hawafikii hata robo ya watanzia VIP itaweza tatua matatizo ya watanzania zaidi ya million 50.
Tuikatae na tuiendele kuipiga vita mpaka mwisho. OVER