Mshahara wa mwezi Septemba kwa Watumishi wa Umma...

MOD nyuzi za hivi kila mwezi ni kupandishana mapigo ya moyo ru.
Nashauri mzifute tu,kila mtu apambane na akili yake.
Serikali ilishasema wote tarehe yetu ni moja,ukiona wewe bado basi usiendelee kumaliza salio la bank kwa SIM BANKING.

Unadhani wote tuna SIM Banking?
 
Hili jinamizi linaloshindwa kuongeza mshahara sijui limetokea wapi!
Mapumbavu utayasikia jiongeze kwa kufanya vibiashara angalau kwa ajili ya kujipatia kakipato huku akisahau kuwa ni sharti kwa mwajiri kuboresha maisha ya mwajiriwa wake, mwingine utamsikia acha kazi, niache kazi unajua kwa kufanya kazi hii nimepoteza mambo mangapi ambayo siwezi kuyapata tena!
Kilimo,biashara nikiamua kufanya nitafanya na nikipata kipato kingine tofauti na mshahara wangu si kwamba ndo haki zangu zikanyagwe.
 
Watanzania daini katiba mpya vinginevyo mtapata tabu sana. Kuna kakikundi ka watu ndo kameifanya Tanzania yakwao.Wananeemeka na kila kitu.
 
Hakuna mtu au waziri simpendi kama huyu mama Wa utumishi. Huyu mama alipoulizwa bungeni kuhusu ongezeko la mishahara alikuja na mbwembwe nyingi kusoma matrioni ya pesa na kusema serikali itaongeza mshahara. Miezi imepita hakuna la nyongeza yeyote. Hivi huyu mama anaona watumishi ni vikaragosi kila siku kuwahadaa kwa majibu yake ambayo hayatekelezeki.

Bunge la mwisho hivyo hivyo akaulizwa na akaja na majibu Yale Yale na ahadi ya increment mwisho wa mwezi huu. Mshahara umetoka lakini hakuna chochote zaidi ya kuwaongezea hasira watumishi.

Akiwa anajibu hoja anakuja na majibu yenye mihemko lakini mwisho ya siku hakuna linalotokea. Hivi hawa wanahitaji watumishi waandamane ndio wajue watu wamechoka ahadi amabazo zilitakiwa zitekelezwe bila hata ya kutokea adha yeyote. Hivi hata hizi increments ambazo ni haki ya mtumishi nazo kuzipata mpaka watu wagome.

Serikali hii iliahidi kutatua kero za watumishi ila imeshindwa zaidi imezidi kuongeza matatizo na kupunguza ari ya watumishi kufanya kazi. Wameongeza 15% na hii imekuwa ni tatizo ukizingatia kuwa mishahara yenyewe ni duni.

Mpaka hapa hii inaashiria kuwa serikali hii haiwezi tatua matatizo ya wananchi wake . Ikiwa imeshindwa kutatua matatizo ya watumishi ambao hawafikii hata robo ya watanzia VIP itaweza tatua matatizo ya watanzania zaidi ya million 50.

Tuikatae na tuiendele kuipiga vita mpaka mwisho. OVER
 
Back
Top Bottom