Msekwa: Chama (CCM) hakitoi maagizo kwa serikali

Hawa magamba wanatuchanganya sana mkutano wa Nec juzijuzi hapa et wanaagiza serikali ipunguze bei ya mafuta yataa heeeeee? nisawa na mkono wakushoto kuagiza mkono wa kulia sasa hao watu wanatumia kichwa kufikiri kweli?
<br />
<br />
ule ni uamuz wa NEC si wa CCM.
 
msekwa ana mkono mrefu kaiba twiga wetu kaenda kuuza nje..sijui ataendelea kumkomalia lowasa ajivue gamba!?ccm inanuka ni majizi wakubwa
 
Jana kwenye mdahalo Nape alisema kuwa rais ni kama muuza duka na chama ni wenye duka.
Mwenye duka anamwekekeza muuza duka nin cha kufanya. Hapa alikuwa anaeleza dhana ya chama kuiagiza serikali.
Msekwa amezeeka!... Ame loose kumbukumbu.

CCM ya sasa inaugua ugonjwa ambao wataalam wa afya bado hawajaugundua! Hivi tangu lini chama tawala na serikali vikawa vitu viwili tofauti? Mkuu wa serikali kwa maana ya Rais ndiye Mwenyekiti wa ccm na historically at least Mwenyekiti anaonekana kuwa na VETO vote! Pengine Mzee Msekwa angefanunua kama Mh Jakaya Mrisho Kikwete- mwenyekiti wa ccm ni mtu tofauti kabisa na Mh Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni hivi majuzi tu tuliona mazingaumbwe pale rais aliyepandisha bei ya mafuta alipomuamuru mwenyekiti wa ccm ashushe bei ya mafuta & guess what? mwenyekiti wa ccm ndiye huyo huyo rais. cheusi-chekundu ndio jina la haya mazingaumbe and it can happen in ccm!
 
Msekwa ametumia akili kujibu swali hilo. Katiba ya nchi inaonyesha kuwa serikali inawajibika kwa Bunge siyo kwa Chama chochote. Ingawa ni kweli kuwa serikali yetu inaendeshwa kwa kufuata manifesto ya Chama, ni makosa vile vile kufanya hivyo kwa vile manifesto hiyo haijaidhinshwa na bunge. Kimsingi serikali inaweza kuwa inaingiza vipengele vya manifesto kwenye bajeti na hivyo kuvihalalisha vitekelezwe, lakini si sahihi kwa serikali kukurupuka kuwa inatekeleza ilani hiyo bila kuwa imepata idhini ya bunge kufanya hivyo.
 
Msekwa ametumia akili kujibu swali hilo. Katiba ya nchi inainyesha kuwa serikali inawajibika kwa Bunge siyo kwa Chama chochote. Ingawa ni kweli mkuwa serikali yetu inaendeshwa kwa kufuata manifesto ya Chama, ni makosa vile vile kufanya hivyo kwa vile manifesto hiyo haijaidhinshwa na bunge. Kimasingi serikali inaweza kuwa inaingiza vipengele vya manifesto kwenye baqjeti na hivyo kuvihalalisha vitekelezwe, lakini si sahihi kwa serikali kukurupuka kuwa inatekeleza ilani hiyo bila kuwa imepata idhini ya bunge kufanya hivyo

Naomba nikuulize, katika ngazi ya utekelezaji, Ilani - Sera - Program ni kipi kinaihusu serikali na kipi kinahusu chama? Maana serikali kama mtendaji haiwezi kupelekewa Ilani itekeleze, kwanza ilani haiwezi kutekelezwa bila kutafsiriwa katika sera( ambazo kwa msingi ndizo zinazopata baraka za bunge) na baadaye hizo sera zinatengeneza mipango ambayo ndio haswa watendaji wanafanyia kazi.
 
Kama na wewe ni mwepesi kuamini hayo kwenye red basi nyinyi ndiyo mnaofanya humu paonekane kijiwe cha porojo badala ya ThinkTank.

Hii ndiyo taabu ya mitandao ambayo mnawasiliana bila kujua mwenzako ni calibre ya aina gani. Hivi wewe na akili yako unaweza kuamini porojo kwamba Luhanjo alipoenda kwenye media basi wewe umekuwa more informed figure than the president!

Kama huju kwamba president yoyote is the most informed person in the world nenda pale Butiama kwenye makumbusho ya Mwl. Nyerere. Utaona kuna redio yenye zaidi ya mitabend 24. Nyerere alikuwa anatembea nayo na alikuwa anakamata karibu kila station duniani.

Ukisoma maelezo unaambiwa kwamba alipewa zawadi toka Ujerumani mwaka 1962.

Leo unatuletea habari za wapuuzi kwamba Rais anashindwa kujua Publc imejulishwa nini tena na mtu alieko ofisi moja! Nimeyasoma hayo magazetini nikayapuuza lakini cha kushangaza inaonekana kuna wengi kama wewe mmepatikana wa kuamini porojo hiyo!

Kama ni kumpa likizo apishe uchunguzi wa bunge hilo ulitakiwa ulitegemee maana hujamsikia Kikwete akitutangazia kuwa Luhanjo kakosea.

Rudi kwenye mada ya Msekwa, toa hoja zitakazotufanya tui-miss JF tunapokatiwa umeme au coverage.

Mkuu katika hali ya kawaida inatakiwa iwe kama ulivyosema. Lakini hali halisi ni hiyo kuwa rais wetu is out of touch, he is less informed than any in the system. Nasema hivyo kwa kuwa kauli zake, maamuzi yake na vitendo vyake vinaonesha kuwa he is not informed.

Mawaziri wake walio makini wanafanya maamuzi kwa mujibu wa sheria na taratibu, lakini anakuja kuwatia aibu mbele ya watu kwa kutafuta cheap credits ambazo hazisaidii utendaji wa serikali. Kama Rais hajui taratibu na sheria, is he informed? Kama angekuwa informed na kama angekuwa anajua ni nini kinaendelea hapa Tanzania he would definetly be much different than he is now.
 
Salam wadau,
Nilikuwa naangalia kipindi cha medani za siasa na uchumi, cha startv ambapo mgeni mwalikwa alikuwa makamu mwenyekiti wa ccm bara ndg. Pius Msekwa.

Akijibu swali alilokuwa ameulizwa na mtangazaji wa kipindi ndg. Mwolekwa juu ya dhana ya chama kushika hatamu, Msekwa amesema sasa hivi chini ya mfumo wa demokrasia ya vyama vingi chama hakiwezi kuiagiza serikali nini cha kufanya bali hilo ni jukumu la bunge na cabinet. Kwamba chama (ccm) kilikuwa kinatoa maagizo kwa serikali wakati wa mfumo wa chama kimoja.

Hivi karibuni baada ya ccm kutangaza kujivua gamba, katibu mwenezi wa chama hicho amekuwa akisikika mara kadhaa akisema kwamba chama (ccm) kimeiagiza serikali yake kufanya moja, mbili, tatu n.k
wadau mimi naona hizi ni statements mbili toka kwa viongozi wa juu wa chama kimoja lakini zinakinzana.

Naomba mawazo yenu.

Jeshini tulikuwa tunaangalia statement ya mwenye cheo kikubwa zaidi na ndiyo iliyokuwa ikifanyiwa kazi. Sasa unaweza kuangalia kati ya Nape na Msekwa nani ni bosi wa mwingine na ukachuchukua maelezo ya huyo bosi kuwa ndiyo sahihi zaidi.
 
Inawezekana Msekwa anasema ukweli kwamba CCM imeshindwa kuongoza....na badala yake 'kila mtu' serikalini anafanya atakavyo!
 
Ninasita kuchangia zaidi hasa kwa sisi ambao hatukuona kipindi hicho.

Kama kuna mtu aliifahamu vizuri maana ya Chama kushika hatamu kuliko hata Nyerere basi ni huyu Msekwa ambaye aliandika kitabu kabisa kuhusu principle ya Chama Kushika hatamu.

Leo, anaposema Chama hakitoi maagizo huku anaunganisha na dhana kwamba Chama hakishiki hatamu, maana yake ni kinyume na dhana yake iliyojaza journals siku zile.

Kwamba ideology ya Msekwa imebadilika. Kama ni kweli, basi nina mashaka na mleta mada ama hakumwelewa Msekwa, kwani kubadili ideology si rahisi kufafanuliwa kama mleta mada alivyoileta ambapo hata paragraph moja haikutimia!

Mkuu heshima kwako,

Nimekusoma una ponti za msingi lakini hapo kwenye red naona umepotoka.

Hivi unaposema maelezo yangu hayajitoshelezi hata paragraph moja unamaanisha nini? hivi kuna idadi ya maneno ninayotakiwa kuandika ili iitwe paragraph? labda unisaidie hapo kwanza hiki kiswahili ni lugha yetu lakini wakati mwingine ni ngumu!

Hata hivyo nataka nikufahamishe kwamba nilimsikiliza kwa makini sana msekwa, mimi ni mtazamaji mzuri sana wa hicho kipindi, ni mara chache sana kukikosa.

Msekwa alizungumza kwa urefu kabisa juu ya suala hili, tena akatilia mkazo "dhana potofu" ya watu kwamba chama ndicho kinatoa maagizo kwa serikali nini cha kutekeleza. Achana na mambo ya vitabu vyake, nchi hii kwa machapisho tu haijambo, ugonjwa mkubwa tulionao ni kutekeleza kwa vitendo yale tuanyoyanena na kuyaandikia "papers"!! Msekwa amesisitiza kwamba bunge ndilo linalotoa maagizo kwa serikali kutekeleza mipango na shughuli mbalimbali za maendeleo.

Kwamba enzi za chama kimoja ndipo chama kilikuwa na uwezo wa kuielekeza serikali nini cha kutekeleza, kwamba mambo yote ya maendeleo ya nchi yalikuwa yanajadiliwa kwenye vikao vya chama na kisha kupelekwa serikalini kwa utekelezaji. Bila shaka nimejitahidi kukamilisha paragraph na utakuwa umenielewa. Though, ahsante kwa maoni yako.
 
Msekwa ametumia akili kujibu swali hilo. Katiba ya nchi inaonyesha kuwa serikali inawajibika kwa Bunge siyo kwa Chama chochote. Ingawa ni kweli kuwa serikali yetu inaendeshwa kwa kufuata manifesto ya Chama, ni makosa vile vile kufanya hivyo kwa vile manifesto hiyo haijaidhinshwa na bunge. Kimsingi serikali inaweza kuwa inaingiza vipengele vya manifesto kwenye bajeti na hivyo kuvihalalisha vitekelezwe, lakini si sahihi kwa serikali kukurupuka kuwa inatekeleza ilani hiyo bila kuwa imepata idhini ya bunge kufanya hivyo.

Mkuu heshima yako,

Mara kadhaa tumewasikia viongozi wa magamba including wabunge kwa nyakati tofauti na kupitia majukwaa tofauti wakiitaka serikali yao kutekeleza mambo mbalimbali. Nape amekuwa akilizungumza hili mara kwa mara kwamba wameiagiza, mara wameitaka serikali kufanya hili na lile. Na juzi kwenye mdahalo amezungumza kitu hicho hicho kwahiyo hakuna namna jambo hili linaweza likabadilika kutoka chama kuiagiza serikali kufanya hili na lile hadi kuwa kwamba bunge ndilo pekee linaloiagiza serikali.

Mara kadhaa tumeshuhudia mawaziri wakijibu hata maswali bungeni na kunukuu ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi, kwahiyo serikali inakuwa inatekeleza maagizo ya chama tawala. Labda tuseme kwamba ni vigumu kwa chama kuiagiza serikali itekeleze mambo fulani kwa kuwa mwenyekiti wa chama ndio huyo huyo kiongozi wa serikali, kwahiyo JK hawezi kujiagiza mwenyewe nini cha kutekeleza!!??
 
Naomba nikuulize, katika ngazi ya utekelezaji, Ilani - Sera - Program ni kipi kinaihusu serikali na kipi kinahusu chama? Maana serikali kama mtendaji haiwezi kupelekewa Ilani itekeleze, kwanza ilani haiwezi kutekelezwa bila kutafsiriwa katika sera( ambazo kwa msingi ndizo zinazopata baraka za bunge) na baadaye hizo sera zinatengeneza mipango ambayo ndio haswa watendaji wanafanyia kazi.

Swali lako sikulielewa vizuri labda kwa sababu ya maneno uliyotumia; Ilani, sera na program katika siasa ni maneno yayonamaanisha jambo lile lile tu. Ilani ni ahadi kuhusu sera za chama na ndani ya ilani hiyo kunaweza kutokea program kadhaa kadhaa ili kutekeleza sera hizo za chama.

Hata hivyo kwa ujumla wake inabidi ufahamu kuwa serikali inafuata sheria iliyotungwa na bunge- unaweza kuiita program lakini bunge halitungi programs bali linatunga sheria. Ingawa chama tawala kitakuwa na sera zake kulingana na manifesto yake, lakini sera hizo siyo sheria kwa hiyo serikali haiwezi kutekeleza sera hizo bila kuwa imeidhinishwa na bunge na kuwa sheria.

Kwa hiyo Kikao cha Kamati kuu ya CCM kinapoamaua serikali ipunguze bei ya mafuta au ifanye jambo fulanie kimsingi hilo ni pendekezo tu na serikali haiwajibiki kulitekeleza kwa vila halijawa sheria. Sana sana serikali inaweza kupeleka mswada wa sera hiyo bungeni ili iidhinishwe na kuwa sheria. Kama tulivyoona hivi karibuni bunge linaweza lisiridhie na serikali ikashindwa kutekeleza hiyo policy.
 
Mkuu heshima yako,

Mara kadhaa tumewasikia viongozi wa magamba including wabunge kwa nyakati tofauti na kupitia majukwaa tofauti wakiitaka serikali yao kutekeleza mambo mbalimbali. Nape amekuwa akilizungumza hili mara kwa mara kwamba wameiagiza, mara wameitaka serikali kufanya hili na lile. Na juzi kwenye mdahalo amezungumza kitu hicho hicho kwahiyo hakuna namna jambo hili linaweza likabadilika kutoka chama kuiagiza serikali kufanya hili na lile hadi kuwa kwamba bunge ndilo pekee linaloiagiza serikali.

Mara kadhaa tumeshuhudia mawaziri wakijibu hata maswali bungeni na kunukuu ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi, kwahiyo serikali inakuwa inatekeleza maagizo ya chama tawala. Labda tuseme kwamba ni vigumu kwa chama kuiagiza serikali itekeleze mambo fulani kwa kuwa mwenyekiti wa chama ndio huyo huyo kiongozi wa serikali, kwahiyo JK hawezi kujiagiza mwenyewe nini cha kutekeleza!!??

Ndiyo makosa kwa vile serikali yetu imezowea kujifanyia mambo kiholela. Kazi ya serikali ni kutekeleza sheria iliyotungwa na bunge; siyo kutekekeleza mambo yaliyoamuliwa na Chama chochote. Iwapo inataka kutekeleza maagizo ya chama chjakle lazima kwanza iyapeleke maagizo yale bungeni kama mswada bwa sheria na iwapo bunge litaridhia nndiyo inanze kuyatekeleza.
 
Mwishoni mwa wezi Julai mwaka huu, CC ya CCM ilikaa naamini ilikuwa Dodoma. Baada ya kikao kile, Nape alionana na waandishi wa habari na kudai kuwa chama kimeagiza serikali kushusha bei ya mafuta kwa sababu wananchi wanateseka. Tukamsikia Masebu akitoa maelekezo ya kushushwa bei na hapo ndipo vurugu mechi ikaanza mjini Dar wafanyabishara kutunishiana misuli na serikali. Na hayo yalikuwa ni maagizo ya chama kwa serikali kwa mujibu wa Nape.
Sasa kama Msekwa anadai chama hakitoi maagizo, je hiyo serikali inatimiza sera na ilani ya uchaguzi wa chama gani??

Hawa wazee umefika wakati wapumzike sasa, tangu niko darasa la kwanza miaka ya 1980....namsikia Msekwa.......hivi hakuna wengine wa kuweza kuongoza aidha ndani ya chama au kwenye bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro (NCAA). Ubongo wa Msekwa umeshachoka hadi amesahau kuwa serikali ya JK inatekeleza ilani ya uchaguzi wa Chama Cha Magamba.
 
Mfumo wa sasa Chama ndio kina iweka serikali madarakani, ,mawaziri pammoja na raisi,wamezipata nyadhifa hizo kupitia chama chao.Ikiwa watakwenda kinyume na matakwa ya chama,wanaweza wakachukuliwa hatua za kinidhamu,kwa lugha nyingine serikali inawajibika kwa chama,lakini chama hakiwajibiki kwa serikali.Ila ikiwa watu hao hao wapo pande zote kwa nyadhifa mbalimbali,inakuwa vigumu kufanya check and balance,inatakiwa kiongozi makini anayeweza kutenganisha majukumu ya hizo kofia mbili.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom