Msekwa: Chama (CCM) hakitoi maagizo kwa serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msekwa: Chama (CCM) hakitoi maagizo kwa serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwita Maranya, Aug 28, 2011.

 1. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Salam wadau,
  Nilikuwa naangalia kipindi cha medani za siasa na uchumi, cha startv ambapo mgeni mwalikwa alikuwa makamu mwenyekiti wa ccm bara ndg. Pius Msekwa.

  Akijibu swali alilokuwa ameulizwa na mtangazaji wa kipindi ndg. Mwolekwa juu ya dhana ya chama kushika hatamu, Msekwa amesema sasa hivi chini ya mfumo wa demokrasia ya vyama vingi chama hakiwezi kuiagiza serikali nini cha kufanya bali hilo ni jukumu la bunge na cabinet. Kwamba chama (ccm) kilikuwa kinatoa maagizo kwa serikali wakati wa mfumo wa chama kimoja.

  Hivi karibuni baada ya ccm kutangaza kujivua gamba, katibu mwenezi wa chama hicho amekuwa akisikika mara kadhaa akisema kwamba chama (ccm) kimeiagiza serikali yake kufanya moja, mbili, tatu n.k
  wadau mimi naona hizi ni statements mbili toka kwa viongozi wa juu wa chama kimoja lakini zinakinzana.

  Naomba mawazo yenu.
   
 2. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2011
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mzee Msekwa umri unapita inawezekana hata mambo ya kawaida ya msingi anayasahau. Chama ndio kinaiagiza serikali kupitia ilani inayoitangaza wakati wa kamoeni, na kupitia wabunge ambao walikuwa wanaimba kuhusu ilani hiyo.
   
 3. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nadhani hapa kunamkanganyiko maana Nepi naye kwenye mdaharo alikuwa anajigamba kuwa chama ndo kinaelekeza serikali cha kufanya na wakienda nje huwarejesha kwenye mstari.

  Kama haya yanayofanywa na serikali ya jk ndiyo maagizo na maelekezo ya chama basi chama cha magamba ndo kinachoipeleka nchi shimoni na kitalaumiwa milele. Siamini kama mwazo ua watu kama Nepi ndo yanayotuongoza sas hivi!
   
 4. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #4
  Aug 28, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Jana kwenye mdahalo Nape alisema kuwa rais ni kama muuza duka na chama ni wenye duka.
  Mwenye duka anamwekekeza muuza duka nin cha kufanya. Hapa alikuwa anaeleza dhana ya chama kuiagiza serikali.
  Msekwa amezeeka!... Ame loose kumbukumbu.
   
 5. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #5
  Aug 28, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  hapa Msekwa anajitoa. Hatak kuhusishwa ktk madudu ya serikal.
  Au atuambie kuwa Mwenyekiti hataki ushaur wa chama.
   
 6. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #6
  Aug 28, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,479
  Likes Received: 12,758
  Trophy Points: 280
  Kama hakitoi kwa sirikali kitakuwa kinatoa kwa mafisadi
   
 7. t

  tonyk2 Member

  #7
  Aug 28, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa magamba wanatuchanganya sana mkutano wa Nec juzijuzi hapa et wanaagiza serikali ipunguze bei ya mafuta yataa heeeeee? nisawa na mkono wakushoto kuagiza mkono wa kulia sasa hao watu wanatumia kichwa kufikiri kweli?
   
 8. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #8
  Aug 28, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hili ndilo jambo lililonishangaza na nikaanza kujiuliza kama mzee msekwa anastahili kuwepo kwenye safu ya uongozi wa ccm kwa sasa. Nadhani huyu mzee anastahili kuwa pembeni labda awe mshauri tu. Haiingii akilini kwamba chama kimenadi ilani halafu kiiachie serikali itekeleze bila maelekezo ya chama. Ama kwa kuwa viongozi wengi wa chama ndo hao hao wa serikali kwahiyo anaona kwamba chama hakiwezi kuiagiza serikali?

  Mkuu usisahau kwamba mwenyekiti wa ccm ndiye raisi kwahiyo kiongozi wa chama ndiye huyo huyo kiongozi wa serikali. Kwahiyo chama kimekuwa lege lege na hivyo ni lazima serikali nayo itakuwa lege lege.

  Lakini muuza duka (JK-Raisi) ndiye huyo huyo mwenye duka(JK-M/Kiti wa chama). Sasa inakuwaje muuza nduka anapokuwa ndiye mwenye duka?

  Yeah, huyu mzee bila shaka anajaribu kukinasua ccm kutokana na ulege lege wa serikali yao. Ye mwenyewe ambaye ni makamu mwenyekiti wa ccm bado pia ni mwenyekiti wa bodi mbalimbali za mashirika ya umma; Ngorongoro anayotuhumiwa kufanya ufisadi ikiwa mmojawapo.

  Mafisadi wenyewe wametapakaa kuanzia kwenye chama hadi serikalini!

  Na kwa kuwa wanaiagiza tu serikali bila chama kufanya uchambuzi wa kina na serikali inatekeleza maagizo ya chama bila kuyatafakari kwa umakini, tukaishia kupanga foleni za kununua mafuta hivi karibuni ili wao watuhadae kwamba serikali yao ni sikivu, matokeo yake ikaishia kuaibika vibaya.
   
 9. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #9
  Aug 28, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Kweli huyu mzee amechoka na maana ya "chama kushika hatamu" wanalotambia ni nini kama hawawezi kutoa maagizo?
   
 10. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #10
  Aug 28, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Gari imenasa kwenye tope, mzee msekwa anajaribu kuinasua hivyo!!
   
 11. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #11
  Aug 28, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Kama chama hakiwez kumpa maagizo Kikwete nan atakayempa maagizo rais. Tumejua kuwa kwanin Rais anavurunda, tatizo ni chama kushindwa kumshaur. Chama hakijui majukum yake.
   
 12. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #12
  Aug 28, 2011
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ninasita kuchangia zaidi hasa kwa sisi ambao hatukuona kipindi hicho.

  Kama kuna mtu aliifahamu vizuri maana ya Chama kushika hatamu kuliko hata Nyerere basi ni huyu Msekwa ambaye aliandika kitabu kabisa kuhusu principle ya Chama Kushika hatamu.

  Leo, anaposema Chama hakitoi maagizo huku anaunganisha na dhana kwamba Chama hakishiki hatamu, maana yake ni kinyume na dhana yake iliyojaza journals siku zile.

  Kwamba ideology ya Msekwa imebadilika. Kama ni kweli, basi nina mashaka na mleta mada ama hakumwelewa Msekwa, kwani kubadili ideology si rahisi kufafanuliwa kama mleta mada alivyoileta ambapo hata paragraph moja haikutimia!
   
 13. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #13
  Aug 28, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  yule mzee hafai anajitoa
   
 14. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #14
  Aug 28, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  wenyewe mnaona wanavyopandana kichwani..wewe umeona wapi Raisi anaarifiwa taarifa nyeti siku moja baada ya maamuzi kufanyika?!

  wacha tumalizie mipango wataondoka mmoja baada ya mwingine....
   
 15. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #15
  Aug 28, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  wamepigwa kwenye mshono......yule mzee anadai eti ameborehsa ngoro ngoro wakati hakuna lolote.....mwizi mkubwa sana yule.....
   
 16. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #16
  Aug 28, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  haya maneno ya nape yamenitia faraja hata ninajua nini cha kutarajia kutoka serikalini,
  kila siku nilikuwa nasugua kichwa inakuwaje wanauza nchi na mali asili zake kama marimao/machungwa
  kumbe wako dukani

  wakuu kuweni makini na kauli za nape ana maanisha
   
 17. only83

  only83 JF-Expert Member

  #17
  Aug 28, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Mkuu,hii ni kawaida ya serikali hii ya awamu ya nne....chini ya kijana JK....kuna mifano mingi ya kukinzana nakupa michache...
  1. Kikwete v/s Luhanjo(ishu ya Jairo)
  2. Kikwete v/s Magufuli(ishu ya bomoabomoa)
  3. Ewura v/s Ngeleja(ishu ya mafuta)
  4. Kikwete v/s Prof.Tibaijuka(uzio wa ubungo)
  Hii ni mifano michache ya kutusaidia kutoshangaa kutofautiana kwa hawa magamba............
   
 18. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #18
  Aug 28, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huyu Msekwa kachoka wenzie wote wamepumzika kabaki yeye na Wasira. Chama ndio kinacho ongoza serikali kupitia manifesto yake na kinaiagiza serikali nini cha kufanya kwa mujibu wa manifest
   
 19. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #19
  Aug 28, 2011
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kama na wewe ni mwepesi kuamini hayo kwenye red basi nyinyi ndiyo mnaofanya humu paonekane kijiwe cha porojo badala ya ThinkTank.

  Hii ndiyo taabu ya mitandao ambayo mnawasiliana bila kujua mwenzako ni calibre ya aina gani. Hivi wewe na akili yako unaweza kuamini porojo kwamba Luhanjo alipoenda kwenye media basi wewe umekuwa more informed figure than the president!

  Kama huju kwamba president yoyote is the most informed person in the world nenda pale Butiama kwenye makumbusho ya Mwl. Nyerere. Utaona kuna redio yenye zaidi ya mitabend 24. Nyerere alikuwa anatembea nayo na alikuwa anakamata karibu kila station duniani.

  Ukisoma maelezo unaambiwa kwamba alipewa zawadi toka Ujerumani mwaka 1962.

  Leo unatuletea habari za wapuuzi kwamba Rais anashindwa kujua Publc imejulishwa nini tena na mtu alieko ofisi moja! Nimeyasoma hayo magazetini nikayapuuza lakini cha kushangaza inaonekana kuna wengi kama wewe mmepatikana wa kuamini porojo hiyo!

  Kama ni kumpa likizo apishe uchunguzi wa bunge hilo ulitakiwa ulitegemee maana hujamsikia Kikwete akitutangazia kuwa Luhanjo kakosea.

  Rudi kwenye mada ya Msekwa, toa hoja zitakazotufanya tui-miss JF tunapokatiwa umeme au coverage.
   
 20. m

  mwl JF-Expert Member

  #20
  Aug 28, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 862
  Likes Received: 588
  Trophy Points: 180
  Tuyakumbuke maneno ya Prof. Lipumba "Kuna ombwe la uongozi ktk serikali ya CCM". huu ndio ukweli.
   
Loading...