MSANII wa muziki wa kizazi kipya Pingu afiwa na mke pamoja na mtoto wake

Jicho la Tai

JF-Expert Member
Oct 10, 2012
1,449
574
MSANII wa muziki wa kizazi kipya Ramadhani Kalesela ‘Pingu’ yupo kwenye huzuni kubwa baada ya kufiwa na mke wake pamoja mtoto aliyekuwa tumboni leo majira ya asubuhi kwenye hospitai ya taifa Muhimbili.

Kwa mujibu wa taarifa iliyoifikia DarTalk, mapema mchana wa leo zinasema kuwa mke wa Pingu alikuwa na hali mbaya wakati wa kujifungua kutokana na kutokwa damu nyingi, ndio tatizo kubwa ilimpelekea kupoteza uhai wake pamoja na wa mtoto aliyekuwa tumboni.

Hata hivyo rafiki wa karibu na Pingu msanii Z-anto, alisema bado wanaendeea na vikao ili kujua watasafilisha au watazikia hapa hapa Dar, lakini hata hivyo nyumbani kwa Pingu Mabibo kuna watu wengi ambao wamejitokeza kumfariji mfiwa.
 
Pole sana Pingu,

Dah hili nalo ni janga sasa! siku hizi mwanamke ukijingua salama ni kumshukuru Mungu sana...
sijui ni mivyakula ya siku hizi??

RIP Mama na mtoto
 
:rip: Mama na Mwana.
Dah!! Imeniuma sana.
Miezi 9 yote kavumilia jamani,
Pole sana kaka Pingu.
 
dah pole sana brother.
mipango ya mungu, tunahaid kua na ww ktk kipindi hiki kigumu. bwana ametoa, na sasa ametwaa
 
In life sometimes tunapitia changamoto ngumu sana.. Hii ni mojawapo lakin hakuna jinsi zaidi ya kusonga mbele... Yap wanawake tunawazingua nao wanatuzingua but washkaji tuheshimu sana mwanamke anae kubebea mimba, just show her some love and respect hata kama ni bahati mbaya kumpa mimba... Wanapitia changamoto kubwa during deliveries na kwingineko.. Nilikuwa nimemchunia sweet hert but ngoja ni m call afurahi
 
Pole sana kaka umepitia experience ngumu sana but ndio mipango ya mwenyez mungu,anatoa na kutwaa
 
Imeniuma sn na kunikumbusha nilivyonusurika kufa na mwanangu,Mama na mtoto wameteseka mateso makuu hadi umauti ulipowafika, PUNZIKENI KWA AMANI WAPENDWA
 
In life sometimes tunapitia changamoto ngumu sana.. Hii ni mojawapo lakin hakuna jinsi zaidi ya kusonga mbele... Yap wanawake tunawazingua nao wanatuzingua but washkaji tuheshimu sana mwanamke anae kubebea mimba, just show her some love and respect hata kama ni bahati mbaya kumpa mimba... Wanapitia changamoto kubwa during deliveries na kwingineko.. Nilikuwa nimemchunia sweet hert but ngoja ni m call afurahi

My sweetheart mjamzito hapa anatapika balaa. Nilikua naona anajifanyisha... Dah nimeenda kumpa busu fasta baada ya kusoma hii
 
Back
Top Bottom