Nilikuwa nasubiri kwa hamu sana kujua upande aliosimama huyu mpambanaji wa kweli katika tasnia ya bongofleva, hatimaye leo nimefahamu.....HONGERA SANA Prof J, huu ni uamuzi wa busara sana hasa kwa hadhi na jina lako katika sanaa, hiki ulichokifanya ni wazi kuwa umeamua kuishi na kutenda kadiri ya mistari ya tungo zako.
We ni mpiganaji na mkongwe katika fani ya muziki wa kizazi kipya, kama ambavyo umekuwa ukipaza sauti yako kupigania maslahi yenu, kwa majukwaa ya burudani, ni vema sasa ukatumia majukwaa ya kisiasa kutanua wigo wakuwatetea walalahoi wa taifa hili (na wasanii wenzako), kama ambavyo SUGU anafanya....
Taifa linatutegemea sana vijana, linatuhitaji sana vijana kupambana ili kuleta mabadiliko ya kweli na yenye manufaa kwa wote.
Mheshimiwa Joseph Mbilinyi- SUGU, amewaonesha njia ni vema wasanii wote wa muziki wa kizazi kipya, wanaharakati wanaoufahamu vema muziki huu ulikotoka wakajitokeza wazi na kumuunga mkono kama ambavyo leo Prof J ameafanya.
Kina SOLO THANG, DOLLA SOUL, MR PAUL, LADY JD, SOGGY DOG ANTER, na wengine wakitambo kile jitokezeni na nyie.
KILA LA HERI PROF J!