Msanii gani maarufu umewahi kuonana naye live mkaongea mawili matatu

Nakumbuka kwangu enzi nipo Arusha miaka ya 2016 , Nlikuwa na kawaida ya kwenda club D maeneo ya Moshono.

Siku ya siku wakaja kina Mr Blue na Rommy Jons ambae alipewa u DJ.

Cha ajabu hatukuwa wengi sana, hatukufika hata 30,

Basi ikawa Mr Blue ananipa mic sana tu niwe nafuatiliza nyimbo zake maana nilikuwa nimezikariri nyingi.

Ilikuwa poa sana ile siku kwangu, Jamaa yupo peace hana makuu
Rose Mhando.
 
Mkuu Bishop Hiluka mzee wa vibe na busara...

Longtime bra! hivi Gayo bado anatoa movie? Lyamba yupo wapi siku hizi? Yule mshkaji boge alikuwa pale petrol station Magomeni mzee wa stori nyingi yupo?
Yeah, long time...

Gayo ame-advance mno, bado yupo kwenye creative industry na sasa yupo international level. Lyamba anaishi Mongolandege ila sijui anafanya nini nowadays. Bonge aliyekuwa Petrol Station (Julius Mhilu) sijawasiliana naye for 2 years now, sijui anafanya nini ila nafahamu anaishi Ubungo/Tabata, karibu na Mwananchi...
 
Chidi nimekutana nae juzi kimara mwisho Hana mwili kabisa yaani Mimi nae yeye Mimi baunsa

Amekaa kijiweni kimara mwisho
Nilikutanaga nae pale kinondoni B Kwa Dr.mvungi..

Jamaa anapiga lapa itakua ni zile anatembea mpaka msasani mpaka masaki Kwa miguu..

Nikajisemea moyoni Huyu ndio chuma..ilala mabegani...mwili umeishaa duu..

For that naogopa sana kushindwa au kufail in life NIDHAMU NIDHAMU NIDHAMU
 
Enzi hizo 2013 au 2014 kama sikosei Hussein Machozi alikuja na kile ki bi mdada cha kizungu hapo ndo penzi lao limeanza anza ofisini kwetu kwaajili ya huduma flani.
Sehemu nyingi za huduma kama yetu walitaka kumtoa pesa ndefu alipofika ofisini kwetu jamaa wakamleta kwangu na mzungu wake..wengine wote hawakumtambua mi nilipomuona tu nikamjua hii chapa ya Singida one wa kunyumba, nikamhudumia saafi na pesa ndogo ya karibu na bure maana nilibless tu na sikutaka kutumia usanii wake kumuumiza.
Alikua humble na Peace pia sio mjuaji kwa kitu asichokijua.

Mwingine Pasha...nilikutana nae Mnazi mmoja kachoka wa kawaida sana hapo havumi tena ata nyusi hajatinda.

Wengine siwataji maana thank God sasahiv nilipo wao ndio wanaona bahati kukutana namimi au kupata nafasi ya kuonana namimi.
 
Late but, nimesimama kama dakika 10 na Will smith nikimurlekeza mambo fulani alipokuja Arusha ku shoot movie yake amabayo hadi leo hii siijui,alipiga kambi kisongo,karibu kabisa na mahali ilipokuwa panajengwa kiwanda cha nguo cha AtoZ, jana yake ndiyo crew yake ilifikia hapo na kuanza kutafuta eneo ambalo wataweza kulitumia kwa muda,nilitumwa kuwaelekeza,na kazi ya kuweka kambi ikaanza fasta,kesho yake ndiyo alikuja mwenyewe smith, wale crew members wakamwambia Mwenyeji wetu huyo hapo,smith akanisogelea,akanipa mkono,then story 2-3 akasepa zake!! Mwingine ni guitarist wa kundi flani la muziki huko UK linaitwa U2,mwenyewe anaitwa BONO huyu nilikutana naye Aicc,kwenye kampeni ya Roll back Malaria, kipindi hicho huyu mwamba aliteuliwa kuwa balozi wa UN kwa misaada africa,so alikuwa mtu muhimu sana kwenye ile issue ya kutokomeza Malaria Africa,huyu tulizurura naye siku nzima,ila crew ilikuwa kubwa kweli kweli,nina picha nyingi za hayo matukio hata sasa, siku chache mbele yake ndiyo alikuja yule Rais wa Liberia,?Mama Hellen johnson salief,nilikuwa kwenye picha yake ya ukaribisho, nyuma kabisa,sijui niiweke? Ila itakuwa uchawi.
 
Kwa hapa wasanii wa bongo- kuna siku nimeenda kinondoni mkwajuni,pale karibu na maghorofa ya hananasif,hiyo mitaa ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kukanyaga,na nilifika usiku kama saa nne hivi, basi nikaingia kwenye nyumba niliyopangiwa kulala,nikampigia rafiki yangu ambaye alishaniambia anaishi mitaa hiyo,akaja, tukaanza kukata mitaa,mwishoni tukajikuta kwenye ki grocery flani kwenye kona sijui ndiyo niliambiwa inaelekea soko la ma tx, tukiwa pale mara ugomvi ukatokea, jamaa mmoja kapigwa ngumi kaniangukia,nikaamka, nikawa mbogo! Mambo gani haya! Jamaa aliyepigwa akainuka, ananiambia "si umeona bro? Huyu# kanipigia nini man? Nikamsukuma nje, jamaa mbishi,ndiyo yule mwenyeji wangu anamuita, oya TIDI tulia basi ndugu yangu! Nikamuuliza mwenyeji, unamjua huyu? Akaniambia huyu si TIDI!! basi tukamkokota hadi kwenye kaduka flani akasogea dirishani mwa duka,akamuita huyo aliyekuwa ndani,nakumbuka jina aliita dada Zai, tukamuacha hapo,nikaenda kulala,niliondoka huo mtaa saa kumi kasoro adhuhuri, hata leo ukiniambia nikupeleke huko sipaju tena,mwisho
 
akati naendesha bolt nimekutana na wengi sana..

jay moe mtu poa very likable dude

amber lulu nilimpakia mara 2 ni mpole sana tofauti ya mtandaoni nikamwambia nataka niwe msanii akaniambia ata usijihangaishe hamna kitu huku ila mpolee au labda first impression.

Abby charms alinipa tip ya elf 10 nilikua na gari bovuuu na halina a.c maza ake akanitilea shombo aka cancel trip njiani abby alivoshuka akanishikisha 10 kimya kimya.

Ila nshakutanaa na wengne wengiii studio, na sinza vatican kwa mwanangu..wasanii wengi sana wanakaa sinza.
Mkuu hebu nipe faida na hasara za hii Kazi kwa hapa Dar..Maeneo unatakiwa kutega abiria
 
Buster rhymes....Sean Kingstone...lil kim na wengio wengi waliowahi kuja bongo...

Hawa wakibongo nakutana nao sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom