che chaunichile
JF-Expert Member
- Jul 4, 2026
- 414
- 696
Mkuu umenichekesha kweli,dah! Pointing hii inalenga kuhalalisha kisasiNyoka akikugonga kisigino na kukuachia sumu ukajitibu ukapona inabidi akija tena umpe kisigino agonge mara ya pili kwa sababu shambulio la kwanza halikufanikiwa
Come on bro 🤦
Mbona haya ni mateso sasa dahHapa tunaamua kuyapokea maumivu tunaugulia weee halafu tunayaacha yapite.Tunaanza kujifariji,kama ulinidhulumu nitajisemea mbona hiki kinatafutwa TU,au hakuna atayezikwa na Mali nk.
Tukifanya hivi maumivu yanaisha ila kumbukumbu itabakia
My friends, ladies and gentlemen,Kuna msemo unasema, hakikisha unachagua upande
Usiwe vuguvugu
Kama ni moto, kuwa moto
Kama ni baridi, kuwa baridi
Japo watu wengi husema usijulikane kirahisi, ila tambua kuna hasara ya kutokujulikana
So unapokosewa, unapoudhiwa au kuumizwa, hakikisha unajulikana umesimama upande gani
Hii tabia ya kujifanya neutral kila wakati kuna muda sio nzuri
Jifunze kujua ni wapi uwe baridi, ni wapi uwe moto, na mara chache sana ujue ni wapi uwe vuguvugu
Kama mada inavyosema...
Msamaha au Kisasi?
Kama umekosewa na umeumizwa, halafu una uwezo wa kusamehe, samehe
Lakini samehe kwa dhati kabisa, kutoka ndani ya moyo
Kwa sababu ukisamehe, amani ya kwanza ataipata wewe kabla hata hajanufaika huyo uliyemsamehe
Sio unasema umesamehe halafu kila siku unanung'unika, unalalama na kurudia lile tukio
Hapo hujasamehe
Unajidanganya mwenyewe
Na huo unafiki wa kuonekana umesamehe wakati bado umebeba mzigo ndani, unaweza kukugharimu kihisia na hata kuharibu mambo mengine kwenye maisha yako
So kama umeamua kusamehe, samehe kweli
Usiwe vuguvugu
Lakini kama umechagua kisasi, ina maana kwako msamaha hauna tija, haukupi amani na unaamini kulipa kisasi ndio haki
Kuna dini inasema kisasi ni haki ya aliyekosewa
Kuna dini nyingine inasema samehe saba mara sabini
Yule aliyechagua kisasi amechagua kuamini kisasi ni haki yake
Na ukweli ni kwamba ana hoja, kwa sababu ni yeye pekee anayejua ameumizwa kwa kiwango gani
Lakini swali linabaki...
Baada ya kulipa hicho kisasi, una uhakika utapata amani, au ndio utaanza kuishi na majuto?
Mfano ukaona adhabu anayostahili aliyekukosea ni kumuua
Je, baada ya hapo utajisikia vizuri, au ndio utaanza kuishi na trauma ya kumwaga damu?
Unaweza ukaamini una haki ya kulipa kisasi
Lakini hakikisha kisasi chako hakiondoki na furaha yako hakichukui amani yako, wala hakiharibu destiny yako
Swali la mjadala👇
Wewe unaamini katika msamaha au kisasi?
Kwa nini umechagua upande huo?
Au wewe ni vuguvugu?
Na kama ni vuguvugu, unaelewa gharama za kutokuwa na msimamo?
ShesRise_1 🤚
Achana na neno kusahau ambalo haiwezekaniMsamaha.... Ila hua sisahau nikimsamehe mtu.... Sijui ni mimi tu¡ ila hata huyo niliemsamehe tunacheka vizuri tu¡
Kuna nyakati kisasi ni halaliMkuu umenichekesha kweli,dah! Pointing hii inalenga kuhalalisha kisasi
AmenUtusamehe... Makosa yetu... Kama nasi tuwasamehevyo walio... Tukosea.......
Amina........
Ambao hawatoi msamaha hawaendi.... Mbinguni
ngumu kumeza!Achana na neno kusahau ambalo haiwezekani
Je unapokua unacheka
Hua na moyo mweupe au unafiki?
Kusamehe tunasemehe ila kusahau ni uongo ubongo kazi yake ni kuhifadhi kumbukumbu ziwe nzuri au mbayaMy friends, ladies and gentlemen,
ni muhimu sana kusamehe na kusahau, kwasababu mbingu si hasira wataingia watakatifu tu.
Eeh chagua upande ishiiMaisha hayana extra time,
chagua upande sasa, ili hatimae uwe na uhuru kamili, ujasiri usiotikisika na uwe na uhakika wa kusimamia unachokiamini kibinafsi na mbele ya jamii. Kua neutral ni unafiki na ubinafsi wa kindezi mno.
Hapa umejuja kama shemasi 🐒ondoka kwenye Giza na sheria kali za agano la kale, na uingie kwenye Nuru katika agano jipya lenye sheria zilizohuishwa. Kung'ang'ana na habari ya visasi dhidi ya ubaya uliotendewa kabla, ni kujitafutia maradhi ya kimwili na kiroho, lakini pia ni maandalizi ya kujiangamiza kwa makusudi kijami, kisiasa na kiuchumi.
ni muhimu sana kuchukuliana kibinadamu na kusonga mbele bila manung'uniko na itapendeza zaidi 🐒
Nshakufamu yekhee!Daima mimi ni ntu wa kisasa. Ntu akinfanyia ubaya nami humlipa kwa ubaya na kuuzidisha kidogo.
Unasema 😮Ukiwa ntu wa wa kumsamehe sana watu wanakuona kama mataqo yao.
Wala sio tatizo lako nadhani kila mtu yupo hiviKusamehe ni jambo moja kusahau ni jambo lingine...
Naweza kusamehe ila kusahau hapana..
Imeze hivyo hivyo 🤣🤣ngumu kumeza!
kuna jamaa alinipiga 3K Yani akiniazima kitu simuamini tena... hapo ina kuwa unafiki?Imeze hivyo hivyo
Mimi sijui kuhusu standard za kisasiKisasi ni haqq ila fikiria Je? baada kulipa kisasi nitapata nafuu na hasira zangu.kushuka..?au ndo nitazidisha matatizo.? je.? hayo matatizo yanaepukika..?
KaribuNITACHANGIA VZR.:
Shukran mi nipo upande wa kisasi yani ukinifanyia baya. kazi..unayoMimi sijui kuhusu standard za kisasi
Wewe mkosewa ndiyo upime kama ulipe kwa njia gani bila kujiweka mtatani
Au chagua msamaha
Karibu
Ukikosewa show show bendera chuma mlingoti chuma 🔥🔥🔥Shukran mi nipo upande wa kisasi yani ukinifanyia baya. kazi..unayo
Ukikosewa show show bendera chuma mlingoti chuma