Kwa kauli zile za Mama, hata huo msamaha wa JN inaonekana amefanya kwa shinikizo baada ya kutonywa kwa yajayo. Lazima kuna mtu kavujisha siri ili amuokoe Mzee wa Galilaya. Wakaona kuomba radhi hadharani inaweza kunusuru.
Kwamba sasa Ndugs aungane na chadema kudai katiba mpya?
Shida ya wanasiasa wetu wakichukia mtu wanchukia na kile anachokisema ata kama kitakuwa kizuri au chenye faida kwake.
wafuasi wa chadema wakiongozwa na mzee Mbatia wamepoteza mwelekeo kabisaa...yaani wanachezeshwa ngoma bila kujua wimbo
Mama kama vipi avunje bunge aitishe uchaguzi mkuu upya, inaonekana kuna changamoto na misuguano ya ndani kwa ndani, mihimili ya sirikali kila mmoja unavutia upande wake, sio nzuri hata kidogo kwa maendeleo ya nchi.
Njia sahihi ni kwa mama kuchuja wabunge ambao ataenda nao sawa , sukuma gang watamchelewesha mama.
Ndugai ndiyo aliyeshiriki kuua mhimili wa bunge chini ya mwendazake.Shida ya wanasiasa wetu wakichukia mtu wanchukia na kile anachokisema ata kama kitakuwa kizuri au chenye faida kwake.
Kwa ilipofikia kama unampenda Ndugai mshauri ajiuzulu! Vinginevyo yajayo ayaeleweki! Nami naamini kwa unafiki wa wabunge hasa CCM hamna atakaejitokeza kumkingia kifua bosi wao, nawajua ni watu wa kuvizia upepo unavumaje!
Polepole amesema hakuna upinzani nchi hiiKutotambua katika siasa kuna agenda za kudumu si marafiki wala maadui kwa hapa kwetu kuna tuangusha.
Kwa hakika la Ndugai na Polepole linaanguka kwenye agenda za muda mrefu za upinzani.
Palitakiwa mipango mikakati ya kucheza na mipira "lose" kama hii.
Timu ya mpira inataka mabao siyo kuwa yamepatikana je.
Ndugai ana wakati mgumu sana;Ndugai kama binadamu alitoa mawazo yake kwa mtazamo wake. Hata hivyo bila shaka nje ya alichokiamini, kwa nia njema alilazimika kuomba msamaha.
Pamoja na kuomba msamaha kwa nia ya kuwaridhisha wakubwa kinyume cha utaratibu kumbe vita ndiyo bado asubuhi.
Alitoa mawazo yake pia Polepole kwa wakati wake. Huyu kaishia kuwekwa kufuli baada ya kujaribu kukomaa:
View attachment 2068711
Mtu mzima hatishiwi nyau!
Ndugu waungwana wenye kuzielewa hoja za bwana Ndugai - Aluta Continua.
"Bungeni kuna kura ya kukosa imani na mtaani kuna tuojisikia kuzibwa midomo."
Vyama vya siasa agenda zenu kuhusu uhuru wa maoni zinasema je? Kwani nyie mko na uadui wa kudumu na watu? Misahafu si inasema adui yako mpende?
Haipo namna ya kuchachandua uwezekano wa kupatikana katiba tofauti hapa yenye kutufaa sote?
Au kwetu ushabiki ndiyo dili na kila apambanae ni mchuma janga tu kwa wakati wake?
"Ndugai vs uliojichimbia zaidi ngoma bado mbichi.'
Tanzania bora zaidi yaweza kuzaliwa hapa!
Ndugai ndiyo aliyeshiriki kuua mhimili wa bunge chini ya mwendazake.
Tupiganie hoja za msingi za kutetea taifa na siyo kutetea wahuni waliogombana kwa zao wenyewe