Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,339
- 51,864
Kwema wakuu!
Katika duru za kisiasa, kinachoendelea ni sakata la Mhe. Spika na Mkuu wa nchi, Mhe. Rais Samia.
Nimesikiliza pande zote mbili nikaona nami nitoe maoni yangu.
Kama mimi ndio ningekuwa Spika nisingeomba Msamaha, ningeweza kufafanua kauli zangu kwa namna ya kutetea kile nilichokuwa nakiamini.
Kitendo alichokifanya Ndugai ni kujisaliti yeye mwenyewe, kushindwa kutetea kile alichokiamini. Na hapa ndipo alipozidiwa na Ndugu Humphrey Polepole.
Sikuona sababu ya Spika kuomba msamaha wakati aliyoyasema yalikuwa ni dhahiri, kuhusu kukopa kaongea vizuri kabisa kuwa tusiwe taifa la kukopa kopa ingawaje hajakataza kukopa. Ndugai kwa upande wake kajaribu kutoa maoni yake kuwa yeye aliona bora kuminyana sisi kwa sisi kwa kutozana kodi kuliko kukopa kopa, huo ni mtazamo wake na ambao nafahamu wapo wengi watakaoungana na yeye kimtazamo na wapo watakaompinga vilevile.
Kitendo cha mtu kuomba msamaha kwa jambo alilolitenda kwa makusudi na ndicho anachokiamini ni kutia kitanzi mwenyewe na kutoa kibali cha upande wa pili kumshambulia atakavyo.
Kuomba msamaha sio ishara ya kukubaliwa isipokuwa kutangaza umeshindwa.
Kuomba msamaha kuna mata zaidi kama Mkubwa akimuomba mdogo msamaha lakini sio mdogo akimuomba mkubwa msamaha.
Mdogo akimuomba mkubwa msamaha huwa na mambo mawili, mosi; Unafiki kutokana na hofu kwa kuwa hana ubavu wa kupambana na mkubwa wake, mbili toba ya kweli ambayo hii wengi ni 10% lakini 90% ni unafiki
Lazima tujifunze kuwa Mtu mzima unapokosea kwa makusudi hata uombe msamaha haitabadilisha lolote upande wa pili, yaani tayari ushaondoa Uaminifu na kamwe huwezi kuurejesha.
Ndugai hakupaswa kuomba msamaha, angetulia na kuendelea na mambo mengine hii ingewapa kazi upande wa pili, lakini kujisalimisha ni kurahisisha kupigwa.
Ndugai pia kapoteza bara na pwani, wale waliokuwa wanamuunga mkono kwa mtazamo wake sasa wanamuona mnafiki, na wale aliowaponda wanakopa kopa pia wanamuona mnafiki hata angeomba msamaha kwa machozi ya damu.
Bora Polepole kabakiza uaminifu kwa wafuasi wake, wanamuona shujaa, na wanaweza kumsikiliza. Lakini sasa hivi nani atamsikiliza tena Ndugai, maana hata yeye mwenyewe hawezi kujisikiliza,
Hii inatupa fundisho sisi wengine wachanga namna ya kufanya maamuzi.
Kama utashindwa basi kwa nini uingie kwenye vita ambayo ulijua tangu mwanzo utashindwa na kudhalilika?
Wito; Kama Ndugai aliongea hayo akiwa na agenda ya siri kama ilivyotanabaishwa na Mhe. Rais basi awajibike au kuwajibishwa, lakini kama ni maoni yake binafsi na hakuna nguvu kutoka nje basi msamaha wake upokelewe.
Hata hivyo nafasi ya Urais sio ya mtu mmoja, hivyo yeyote anayetaka kuwania asionekane ni adui wa nchi.
Tuache demokrasia ichukue mkondo wake. Kutaka Urais 2025 sio dhambi wala sio kosa la jinai. Labda wanaotaka wawe wanahujumu utendaji kazi wa Serikali iliyopo madarakani lakini kama ni kuikosoa kwenye mapungufu yake ili ionekane haina sifa ya kuendelea 2025 hilo sio kosa kimsingi.
Tujenge nchi