Msamaha na Kisasi

Msamaha na Kisasi

ShesRise_1

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2025
Posts
15,152
Reaction score
35,333
Kuna msemo unasema, hakikisha unachagua upande

Usiwe vuguvugu
Kama ni moto, kuwa moto
Kama ni baridi, kuwa baridi

Japo watu wengi husema usijulikane kirahisi, ila tambua kuna hasara ya kutokujulikana

So unapokosewa, unapoudhiwa au kuumizwa, hakikisha unajulikana umesimama upande gani

Hii tabia ya kujifanya neutral kila wakati kuna muda sio nzuri

Jifunze kujua ni wapi uwe baridi, ni wapi uwe moto, na mara chache sana ujue ni wapi uwe vuguvugu

Kama mada inavyosema...

Msamaha au Kisasi?

Kama umekosewa na umeumizwa, halafu una uwezo wa kusamehe, samehe

Lakini samehe kwa dhati kabisa, kutoka ndani ya moyo

Kwa sababu ukisamehe, amani ya kwanza ataipata wewe kabla hata hajanufaika huyo uliyemsamehe

Sio unasema umesamehe halafu kila siku unanung'unika, unalalama na kurudia lile tukio

Hapo hujasamehe
Unajidanganya mwenyewe
Na huo unafiki wa kuonekana umesamehe wakati bado umebeba mzigo ndani, unaweza kukugharimu kihisia na hata kuharibu mambo mengine kwenye maisha yako

So kama umeamua kusamehe, samehe kweli
Usiwe vuguvugu

Lakini kama umechagua kisasi, ina maana kwako msamaha hauna tija, haukupi amani na unaamini kulipa kisasi ndio haki

Kuna dini inasema kisasi ni haki ya aliyekosewa

Kuna dini nyingine inasema samehe saba mara sabini

Yule aliyechagua kisasi amechagua kuamini kisasi ni haki yake

Na ukweli ni kwamba ana hoja, kwa sababu ni yeye pekee anayejua ameumizwa kwa kiwango gani

Lakini swali linabaki...

Baada ya kulipa hicho kisasi, una uhakika utapata amani, au ndio utaanza kuishi na majuto?

Mfano ukaona adhabu anayostahili aliyekukosea ni kumuua

Je, baada ya hapo utajisikia vizuri, au ndio utaanza kuishi na trauma ya kumwaga damu?

Unaweza ukaamini una haki ya kulipa kisasi

Lakini hakikisha kisasi chako hakiondoki na furaha yako hakichukui amani yako, wala hakiharibu destiny yako

Swali la mjadala👇

Wewe unaamini katika msamaha au kisasi?

Kwa nini umechagua upande huo?

Au wewe ni vuguvugu?

Na kama ni vuguvugu, unaelewa gharama za kutokuwa na msimamo?

ShesRise_1 🤚
 
Kusamehe Kwa dhati, imekuwa Ngumu sana Kwa Binadamu, Maana ukisamehe mtu akakukosea Tena, Huwa tunarudia na kusema hii ni mara ya pili unanikosea, Mwanzo ulinikosea!Na Visasi tunavyovingi hata Kama mtu hakukukosea, Mfano mtu unamkopa Hela, ukiwa unaamini atakukopesha, kumbe hana, Sasa Kwa Kukosa kukukopesha,siku akija na shida ya kukopa,unamnyima wakati unazo, unakumbuka Yeye hakukukopesha, kumbe alikuwa hana!
 
Msamaha ni kwa ajili yangu, si kwa ajili ya aliyenikosea ukifikiri kuwa hata mimi huwa nawakosea wengine, hivyo huachilia, maana kisasi kina hasara kubwa.

Fikiria kama mtu amekuchukulia mke wako halafu na wewe unaenda kulipiza kisasi labda kwa mke wake, au vyovyote ukakutana na magonjwa majuto anakuwa mjukuu
 
Samehe kwa mkakati maalumu, pia lipa kisasi kwa mkakati maalumu....
..... kisasi kisikupe majuto, kama ukajikuta upo jail, ukakimbia mji wako, miradi yako n.k
......msamaha usikufanye uonekane bwege ukaonekana huna mipango
 
Back
Top Bottom