Msaliti wa Dk. Ulimboka yuko ikulu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaliti wa Dk. Ulimboka yuko ikulu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 16, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145


  [​IMG]
  Na Joster Mwangulumbi - Imechapwa 11 July 2012

  [​IMG][​IMG]
  ULIMBOKA ni neno la Kinyakyusa lenye maana ya Mungu uniponye. Neno hilo ndilo linatumika kama jina na ukoo wa Dk. Steven.

  Mtu akiwa kwenye matatizo, shida, mashaka au mateso huomba huruma ya Mungu amponye. Kwa huruma na upendo, Mwenyezi Mungu ndiye aliwashika wasamaria wema, kwa mkono wake wa miujiza, akawaongoza, bila kujijua kwenda kumwokota na kumfikisha hospitalini Dk. Steven Ulimboka aliyepigwa na kutupwa katika msitu wa Mabwepande akaachwa afe.


  Mungu aliyewaongoza wasamaria wema kumwokoa na kumfikisha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha mifupa (MOI), ndiye amemtia nguvu, anazungumza sasa kwa ‘ufasaha' alivyopigiwa simu na ofisa wa ikulu, alivyotekwa, alivyoteswa usiku kucha na alivyookotwa.


  Hivi sasa anapata matibabu katika hospitali moja nchini Afrika Kusini, akisubiri ubuponyi yaani uponyaji kamili kutoka kwa Mwenyezi Mungu mwenyewe.

  Katika mkanda wa mahojiano maalum akiwa MOI, Dk. Ulimboka haachi chembe ya shaka kwamba mkasa huo ulipangwa na kuratibiwa na kikosi maalum cha ‘mauaji' ambacho kina maslahi na mgomo wa madaktari ambao umedumu kwa wiki tatu sasa.

  Sehemu ndogo ya maelezo ya Dk. Ulimboka ni kama ifuatavyo….

  …Kazi yao ilikuwa siyo kufanya kazi kama askari, eeh its like they acted under instructions.

  Eeh, yaani unajua, kwa muda kama siku tatu mfululizo, huyu bwana alikuwa anajaribu kuwasiliana na mimi lakini kwa bahati mbaya ratiba yangu ilikuwa haiwezekani kumwona.


  Nilishawahi kumwona zamani, kwenye mgogoro ule mwingine, lakini this time of course alikuwa serious akinitafuta akisema kwamba anataka some hearing ili aweze kushauri. Huyu bwana anafanya kazi ikulu.


  Aah, mimi kwa sababu namfahamu kutokana na incident ya kwanza sikuwa na muda. Lakini jana aka-insist sana na akakaa Hugo pale muda mrefu sana, sisi tulikuwa tumekaa Leaders Club.


  Baadaye nikamwambia Deo kuna jamaa mmoja – ambaye Deo anamkumbuka sana kwa sababu mara zote huwa tunakwenda naye – anataka kutuona. Basi tukawaacha wenzetu wanafanya kazi nyingine, tukaondoka mimi na Deo around saa tano, ilikuwa na robo (5.15).


  Naye akatuarifu kuwa pale Hugo alipokuwa amekaa wanafunga, akawa ameenda kule juu sehemu inaitwa Stereo, akaniambia yupo pale. Mimi nikawasha gari hadi pale, nikaangalia meza ya kwanza pale sikumwona. Tulipoingia pale hatukumwona.

  Nikazunguka sikumwona, nikampigia simu akaniambia, nakuja hapo sasa hivi.


  It took like twenty to thirty minutes tangu aliposema anakuja. Tukaamua kuwasha gari ili kurudi pale Leaders lakini tukaona kama hilo haliwezi kuwepo. tukaishia pale Tunisia Road kuna kontena, tukakaa pale. Sasa akawa anapiga simu akisema anakuja kuna vitu anamalizia; tukawa tunawaza ni vitu gani?


  Basi tukiwa tumekaa, ghafla tukamwona anafika, kwa gari. Akasema uko na Deo, nikasema eeh. Basi tukaanza mazungumzo.


  Kitu ambacho nili-notice, while tukiwa tuna-discuss naye, akitaka kujua namna gani tuweke understanding; matatizo yetu ni yapi, which are the priority areas, eeh kama alivyosema yeye mwenyewe ili aweze ku-advise, kwa sababu wakati mwingine…


  Sisi tukasema mambo yote yanafahamika. Tukaongea naye kwa muda mfupi tu, akawa anaandika kwenye diary yake, kwa hiyo pia alikuwa very bussy communicating, unaona.


  Kwenye simu yake sasa, tukafika kwamba tumemaliza. Ila sisi tulikuwa tuna vinywaji kwa sababu ilikuwa siyo rahisi sana tumwache yeye aondoke sisi tuendelee kubaki. Yeye alikuwa anakunywa maji akasema bwana mi naondoka.


  Kwenye ile line ya yeye kusema anaondoka tu, hapo hapo wakatokea watu kama wanne watano hivi, wakasema, wakaja straight kwenye meza yetu, as if they were directed. Wakasema upo chini ya ulinzi, yaani mimi hapa. Kama mtu hakujui hawezi kuja saa 5 usiku kuja kukukamata.


  They came direct towards me, nikauliza kwani kuna kosa gani? Wakanipiga mtama nikaanguka barabara ya lami. Nilichokifanya kitu cha kwanza ni kutoa simu na kumpa Deo. Sasa they pushed me na kufanikiwa kuchukua simu moja na wallet yangu.


  Nilichowahi ni kuchomoa simu yangu kumpa Deo. Wakaniburuza huku wakini-push again na kuvuka barabara hadi kwenye gari ile, ilikuwa haina namba ile, ni kama Starlet hivi. Nikaamua tu kubaki patient.


  Wakafungua lango la nyuma wakanitupa huko. Wakaja wakanitupa huko. Basi mmoja akaingia upande wangu wa kulia mwingine wa kushoto. Wakaanza kunipiga ngumi, wakanipiga ngumi; mwingine akanipiga vichwa, naona, wengine wana kama dude fulani kama la plastiki hivi, wananipiga kichwani. Wananiambia tulia tutakuua sisi. Kama una ndugu zako aga kabisa kwa sababu leo hurudi.


  Unatuletea usumbufu sana wewe… sasa nikawa najiuliza usumbufu gani? Kwa sababu hata hapo usumbufu, wewe unajua unachokifanya kwa hiyo tunataka kukomesha hiyo tabia. Wakanipiga kwenye gari hiyo huku inakwenda, ilikuwa inaenda mwendo wa kasi sana. Nikafanikiwa kuchungulia hivi nikagundua tuko maeneo ya Victoria…

  …Hata na ile miguu wakafunga sana. Basi wakaendesha gari, wakaendesha this time muda mrefu sana. Sikuwa najua wanaenda wapi. Walipokuja kunishusha, wakaanza kunipiga tena.

  Sasa kwa sababu I was helpless nimefungwa, basi nikawa napigwa nageuka hivi, nikigeuka hivi, nikaona wananipiga kwa sikio la huku, wengine wakawa wananipiga sikio la huku walinipiga sana kama half an hour hivi, and then I think I lost consciousness.


  Unaona na nilikuwa na-bleed sana wakati ule. Kwa hiyo nilichofanya nikawa napata feelings hawa watu they are carrying me somewhere.


  Nikafika mahali nikaona kama vile wamenitupa kwenye shimo hivi. Sijui kama wanataka kunifukia? Unaona, nikawaambia why I are you burring me alive?...

  Katikati ya mateso kama aliyopata Dk. Ulimboka kuna uponyaji. Kwa kuteswa kwake Yesu Kristo binadamu wamepona (biblia).

  Kwa kujichoma moto, mmachinga wa Tunisia baada ya mgambo na polisi kuvuruga biashara yake, nchi nzima iliwaka moto na Watunisia wakapata demokrasia.

  Kutokana na maandamano katika viwanja vya Tahrir na serikali kujibu kwa risasi, Misri iliwaka moto, hatimaye imefanya uchaguzi huru.

  Watu wote wasio na hofu ya Mungu, ndio wanaweza kujisikia raha kuteka watu wasio na hatia na kuwatesa, wakati mwingine, kwa kufurahia vipande vya fedha.


  Yuda Isikarioti alifurahia vipande 30 vya fedha kwa kazi ya kumsaliti Yesu. Aliishia wapi? Kwa kuteswa kwake Dk. Ulimboka, Mungu atawatia adabu walioratibu mpango huo.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Tahrir = ? then Ulimboka?
   
 3. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Nilimsahau Deo, ntamuongeza kwenye orodha ya wahusika wakuu kule kwenye ile movie inayotayarishwa yaitwa "Mabwepande and The Wrath of Pliers".
   
 4. kadoda11

  kadoda11 JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 16,267
  Likes Received: 8,330
  Trophy Points: 280
  picha linaendelea......
   
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Vipi hali yake, hajambo> anarudi lini? ataendeleza migomo? vipi huyu alikuwa chadema?

  Nasikia kuna kada wa CCM kauliwa Singida, vipi? mnasemaje kuhusu hilo?
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Go to hell!
   
 7. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Zombie ni kitu kisicholewa kitu kwa sababu ya hali yake kwa kukosa utimilifu wa kibinadamu
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  nagombea ubunge kilwa kupitia ccm naomba sapoti yako
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kweli mimi silewi. Jamani mpaka ulewe ndio uwe na "utimilifu'? huo ni ukosefu wa maadili.
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Timing ikikaa sawa tutakupigia debe, usiwe na shaka.
   
 11. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kwani wewe ni Zombie?
   
 12. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #12
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kwi kwi kwi teh teh teh! Ya ngapi?
   
 13. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #13
  Jul 16, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Watashindana naye, hawatashinda!!, ndo wanazidi kujitengenezea anguko
   
 14. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #14
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Kada wa ccm? Unamuuliza nani hapa jamvini? Nenda lumumba
   
 15. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #15
  Jul 16, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,323
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  Hizi siasa za maji taka zinatupeleka wapi? Uhuni unaingizwa kwa makusudi kwenye siasa. Ipo siku tutakosa wote maana haitawezekana kufungana. Kwanini tusihimizane kutafuta maendeleo tunahimizana kumalizana kisiasa tu? kama leo ntaambiwa niiongoze system, economic intelligence would be my first priority...watu wakila na kushiba hakutakuwa na kelele za hovyo za kisiasa
   
 16. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #16
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Jibu ya Uli basi au hata hayo niende Lumumba?
   
 17. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #17
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Kwani jack zoka na Ahmed Msangi wanasemaje iwapo ataendelea na mgomo?
   
 18. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #18
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,569
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Nisha jua real id ya huyo zoba!
   
 19. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #19
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Hii story ya Ulli inaingia moja kwa moja katika 'lane' ya kumbukumbu mbaya kabisa za taifa hili chini ya JK. SOON waliomtesa watamwona mtaani, si katika hali waliyomwacha nayo pale Mabwepande, bali ktk hali mpya na ya uzima tele.
   
 20. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #20
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kwanza jibu maswali yangu halafu uulize lako. Ngoja nikukumbushe:

   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...