Msajili alaani vurugu zilizotokea katika mkutano wa wanaosemekana ni viongozi wa CUF na Waandishi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,713
13,463
MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KULAANI VURUGU ZILIZOTOKEA KATIKA MKUTANO WA WANAOSEMEKANA KUWA NI VIONGOZI WA CUF NA WAANDISHI WA HABARI

Nimesoma na kuona katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusu vurugu zilizotokea tarehe 22 Aprili, 2017 katika hoteli ya Vina, Mabibo hapa Dar es salaam, zinazosemekana kuhusisha wanachama wa CUF.

Ni ukweli usiopingika kuwa, suala la mgogoro wa uongozi katika chama cha CUF lipo mahakamani, lakini nikiwa msimamizi wa Sheria ya Vyama vya Siasa na kutambuliwa na jamii kuwa ni mlezi wa vyama vya siasa; nimelazimika kuwasihi wadau wa siasa hususani wanachama wa chama cha CUF, kutambua kwamba, kuwapo kwa shauri mahakamani siyo fursa ya kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani, kwani jambo hili ni uvunjifu wa sheria na linaleta sura mbaya kwa jamii.

Hivyo, ninalaani vurugu hizo, ambazo zilionekana kuvunja amani na utulivu na watu kuumizwa, tofauti na tunu zetu za taifa za amani na utulivu. Pia, nawaasa wanachama wa CUF pamoja na tofauti walizonazo, madhali masuala haya yapo mahakamani hebu tuheshimu utawala wa Sheria.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na hata Jeshi la Polisi lipo kushughulikia malalamiko yoyote yanayohusu uendeshaji na shughuli za chama chochote cha siasa. Hivyo, hakuna haja ya wanachama wa chama cha CUF kukiuka taratibu za kuendesha chama hicho au kujichukulia Sheria mkononi.

Aidha, ninaviasa vyama vya siasa kuelewa kuwa havipo juu ya Sheria, vinapaswa kuheshimu na kufuata Sheria za nchi, ikiwamo kutunza amani na utulivu tulionao.

Mwisho, ninaomba vyombo vya ulinzi na usalama katika nchi yetu kulifanyia kazi tukio hilo, ili wahusika wafahamike na kuchukuliwa hatua za kisheria. Kwa upande wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inayosimamia utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa, haitasita kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa Sheria.

IMG_5746.jpg
 
Msajili analaani kwakuwa aliyeumizwa baada ya uvamizi ni mtu wa upande anao usupport. Huu uhuni haukuanza jana wala leo na yy ndio sehemu ya hilo tatizo. Huko kulaani ni kama kumfariji mjeruhiwa ambaye yeye anaelewa huo mchezo wanaoucheza kwani hao wavamizi wana baraka zake.
 
Mwisho, ninaomba vyombo vya ulinzi na usalama katika nchi yetu kulifanyia kazi tukio hilo, ili wahusika wafahamike na kuchukuliwa hatua za kisheria. Kwa upande wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inayosimamia utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa, haitasita kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa Sheria.
Tunasubiri kuona na kusikia (toka kwako na polisi) hatua gani zitachukuliwa. Nawapa benefit of doubt.
 
Tatizo kubwa hapa ni msajili . Msajili kama mlezi wa vyama hana msimamo thabiti amemkumbatia Mr . Lipumba kwa mikono miwili na hata kumpa ruzuku hili ni tatizo na vyema mahakama ikatoa hukumu ya kesi ili kuepusha majanga makubwa zaidi .
 
Mtetezi wahuni analaani nini? Kwani hajui kuwa hayo ndiyo matunda ya uhuni anaolea?Acha kujidai hujui Mutungi mtu wa ajabu sana.PHD ovyo kabisa.
 
MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KULAANI VURUGU ZILIZOTOKEA KATIKA MKUTANO WA WANAOSEMEKANA KUWA NI VIONGOZI WA CUF NA WAANDISHI WA HABARI

Nimesoma na kuona katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusu vurugu zilizotokea tarehe 22 Aprili, 2017 katika hoteli ya Vina, Mabibo hapa Dar es salaam, zinazosemekana kuhusisha wanachama wa CUF.

Ni ukweli usiopingika kuwa, suala la mgogoro wa uongozi katika chama cha CUF lipo mahakamani, lakini nikiwa msimamizi wa Sheria ya Vyama vya Siasa na kutambuliwa na jamii kuwa ni mlezi wa vyama vya siasa; nimelazimika kuwasihi wadau wa siasa hususani wanachama wa chama cha CUF, kutambua kwamba, kuwapo kwa shauri mahakamani siyo fursa ya kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani, kwani jambo hili ni uvunjifu wa sheria na linaleta sura mbaya kwa jamii.

Hivyo, ninalaani vurugu hizo, ambazo zilionekana kuvunja amani na utulivu na watu kuumizwa, tofauti na tunu zetu za taifa za amani na utulivu. Pia, nawaasa wanachama wa CUF pamoja na tofauti walizonazo, madhali masuala haya yapo mahakamani hebu tuheshimu utawala wa Sheria.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na hata Jeshi la Polisi lipo kushughulikia malalamiko yoyote yanayohusu uendeshaji na shughuli za chama chochote cha siasa. Hivyo, hakuna haja ya wanachama wa chama cha CUF kukiuka taratibu za kuendesha chama hicho au kujichukulia Sheria mkononi.

Aidha, ninaviasa vyama vya siasa kuelewa kuwa havipo juu ya Sheria, vinapaswa kuheshimu na kufuata Sheria za nchi, ikiwamo kutunza amani na utulivu tulionao.

Mwisho, ninaomba vyombo vya ulinzi na usalama katika nchi yetu kulifanyia kazi tukio hilo, ili wahusika wafahamike na kuchukuliwa hatua za kisheria. Kwa upande wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inayosimamia utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa, haitasita kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa Sheria.

View attachment 500432
AIBUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU imewatoa pangoni.
 
wewe mwenyewe ndio mtuhumiwa namba moja
 
Back
Top Bottom