Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,351
- 33,189
Uhakiki wa CCJ Dar vurugu tupu, TENDWA ADAI WANACHAMA HALALI NI 13 TU, ZOEZI LASITISHWA
Elizabeth Suleyman
VURUGU zimezuka wakati wa uhakiki wa wanachama wa Chama cha Jamii (CCJ), baada ya Msajili waVyama vya Siasa nchini, John Tendwa kusitisha zoezi hilo mkoani Dar es Salaam.Tendwa alichukua hatua hiyo baada ya kubaini kuwa chama hicho kina wanachama halali 13 badala ya 200 katika mkoa huo
Baada ya timu ya ukaguzi wa wananchama iliyoongozwa na Tendwa kubaini hilo na kutangaza kuwa wanachama walitimiza masharti ni 13 tu, viongozi wa CCJ walidai hizo ni hujuma za CCM.
Jana gazeti hili lilishuhudia wanachama zaidi ya150 kutoka maeneo mbalimbali wilayani Temeke wakiandikishwa wakati uhakiki ukiendelea katika viwanja vya Mwembe Yanga.
Tendwa alianza kuhakiki fomu 247 alizokabidhiwa na uongozi wa CCJ. Wakati akiendelea na zoezi hilo, ndipo utata ulianza kuhusu wanachama waliofika kuhakikiwa pamoja na viongozi wao.
Katika uhakiki huo, iligundulika kuwa Mwenyekiti wa CCJ, Richard Kiyabo ni miongoni mwa majina yaliyopo kwenye fomu za wanachama lakini hakuwa na kadi ya chama.
Mwenyekiti huyo alijititea kuwa kadi yake ilipotea alipovamiwa na majambazi eneo la Kariakoo mwaka huu na kwamba,taarifa alishatoa polisi.
Mkasa huo pia ulimkumba katibu wa chama hicho, Renatus Muabhi ambaye alijikuta katika wakati mgumu, baada ya kuambiwa na msajili kwamba, katika orodha ya majina yaliyopo kwenye fomu jina lake halipo, ila ana kadi kadi tu.
Mheshimiwa, huenda makosa yalifanyika wakati kuchapa majina hayo katika fomu hizo, alijitetea Muabhi.
Hata hivyo, Tendwa aliwaambia kuwa kwa vile wao ndiyo waanzilishi wa chama hicho, anawatambua, ingawa mmoja wao jina lake halipo kwenye fomu.
Wakati Tendwa aliendelea na uhakiki huo, alibaini kuwa kati ya wanachama 200 walioko katika chama hicho, 13 ndiyo waliotimiza vigezo vya kuwa wanachama.
Nashindwa kuelewa, viongozi CCJ walisema wana wanachama 200 mkoani Dar es Salaam na 7,000 kwa nchi nzima, lakini katika uhakiki niliyofanya, nimepata wanachama 13 tu ambao wana vigezo na nimerudisha kadi 27 ambazo hazina sifa," alisema Tendwa na kuongeza:
Baadhi ya wanachama, wamekuja na kadi yenye majina tofauti na yaliyoandikwa kwenye fomu ya orodha ya wanachama.
Tendwa alitoa mfano: Utakuta kadi imeandikwa jina Halima Mohamed, lakini kwenye fomu unakuta namba ya kadi ni ya Juma Salum.
Tendwa alipoanza kutoa kasoro hizo, viongozi wa CCJ akiwemo mwenyekiti walianza kulalamika na kusema wamesitisha zoezi hilo, kutokana na hujuma za viongozi wa CCM ambao hawataki CCJ ishiriki uchaguzi.
Mheshimiwa, tunaomba kusitisha zoezi hili kwa sababu tuna hofu na CCM, kwani hakina nia CCJ isajiliwe mwaka huu, alisema Kiyabo.
Alisema kuna haja ya kuwepo vyama vya hiari vitakavyotetea haki ya wanyonge, kwa sababu CCJ haitendewi haki kabisa kutokana na mipaka inayowekewa ambayo haina misingi.
Serikali ilisema mwezi huu mtahakiki na kukisajili chama chetu; sasa hivyo vigezo vya kusema kwamba, wanachama hawana vigezo vya unachama, vinatoka wapi ni bora mzee ustaafu kazi. Mnatuhujumu hakuna haki hapa, alisema kwa hasira na kudai kwamba wanasitisha zoezi la kuhakiki kuendelea katika mikoa iliyosalia.
Kiyabo alidai kuwa CCM hakitaki CCJ , isajiliwe ndiyo maana Tendwa anataka kuwa juu ya sheria kwa kutumia demokrasia ya kutuwahujumu .
Kufuatia hali hiyo, Tendwa alitoa amri ya kusitisha zoezi la uhakiki kwa Mkoa wa Dar es Salaam kutokana na wanachama wengi kugundulika kuwa hawana vigezo na kwamba kesho ataanza na mkoa wa Pwani Jumamosi atamalizia na Wilaya ya Ifakara, Morogoro.
Kwa Dar es Salaam, basi tena, tumesitisha zoezi hili badala yake tutaendelea na uhakiki katika mikoa iliyosalia, alisema Tendwa.
Uhakiki wa CCJ Dar vurugu tupu, TENDWA ADAI WANACHAMA HALALI NI 13 TU, ZOEZI LASITISHWA
HIVI VYAMA VIPYA VIJIAANDAE KWA UCHAGUZI WA MWAKA 2015 JAMANI VINALETA UWINGI KWENYE UCHAGUZI NA HAVIWEZI KUSHINDA.