Msajili ajipanga kuanza uhakiki wa CCJ wiki hii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msajili ajipanga kuanza uhakiki wa CCJ wiki hii

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 31, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 31, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa najiandaa kwenda kupumzika saa kumi na nusu hizi za alfajiri wakati vinzi karibu na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa vinadokezakuwa leo mchana msajili amepanga kukutana na uongozi wa CCJ.. Nadhani itasaidia kuepusha hisia mbaya baina ya pande hizi mbili na masuala ya umuhimu wa kitaifa yataweza kupatiwa suluhu ya haraka ili hatimaye kila mmoja afanye anachotakiwa kufanya katika kuendeleza demokrasia na hatimaye kulipatia taifa uongozi unaostahili wenye ajenda isiyo na utata.

  Nalala kama sungura.!! see u later inshallah.
   
 2. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2010
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Ameshapata hela za kuhakiki majina?
   
 3. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Nafikiri lile tamko la wanasheria kutoka Mkoa wa Arusha limemkurupusha Tendwa usingizini! Watu hawaendi, mpaka kwa viboko kwani wamekuwa punda?
   
 4. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2010
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ngoja tusikie km hizo tetesi zitakuwa habari iliyothibitishwa...
   
 5. k

  kisikichampingo Senior Member

  #5
  May 31, 2010
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 129
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Samahani mkuu, wanasheria wa mkoa wa Arusha walitamka nini?
   
 6. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tendwa apondwa kwa kutoisajili CCJ


  na David Frank, Arusha

  CHAMA cha Mawakili Tanzania (TLS) Mkoa wa Arusha, kimemkosoa msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa kwa kukataa kukisajili Chama Cha Jamii (CCJ) kwa madai ya kutokuwa na fedha za kuhakiki wanachama wake walioko mikoani. Mawakili hao wamemtaka Tendwa kukisajili chama hicho na vyama vingine bila ubabaishaji kwa kile walichoeleza kuwa hana sababu ya msingi ya kukataa kusajili vyama kwa madai ya kutokuwa na fedha kwani kufanya hivyo ni ukiukaji wa sheria.

  Wamesema kitendo cha msajili huyo cha kuweka visingizio kadhaa vya kukisajili chama hicho kinaweza kumtia matatizoni kwa kushtakiwa kwa kutofuata sheria kwa kuwa hakuna sheria inayomtetea kwa hilo.

  Tamko lao la Mei 28 mwaka huu lililosainiwa na Mwenyekiti wa TLS Mkoa wa Arusha, Duncan Oola, limebainisha Tendwa ana wajibu wa kusajili na kutoa hati ya usajili wa kudumu kwa chama hicho na vingine vilivyowasilisha maombi na kutimiza masharti yaliyowekwa kisheria.

  "Tunachukua fursa hii kumkumbusha msajili huyo kwamba kama cheo chake kinavyojieleza chenyewe, kazi yake ya msingi kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa Sura Na. 258 (R.E. 2002) kama ilivyorekebishwa na Sheria Na 7 ya 2009 ni kusajili vyama vya siasa," inaeleza sehemu ya tamko hilo.

  Aliongeza kuwa kifungu cha 8 (5) cha sheria hiyo kinatamka wazi kwa lugha ya Kiingereza kuwa lugha iliyotumika katika kifungu hicho ni ‘shall' na siyo ‘may' kwa maana Msajili hana hiari kukubali au kukataa kusajili chama ambacho kimetimiza masharti ya kisheria ya kupewa usajili ama wa muda au wa kudumu.

  Tamko hilo liliongeza kuwa ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inatakiwa kupokea na kushughulikia maombi ya usajili wa muda na wa kudumu wakati wote kwa kuwa sheria haijatenga kipindi maalumu cha kuwasilisha maombi ya kupewa usajili huo na kwamba sheria haijatamka muda ambao msajili anaruhusiwa kutopokea maombi ya usajili wa chama cha siasa.

  Tamko hilo lilisema kuwa msajili anawajibika kuahirisha shughuli zote ambazo si za msingi ili kushughulikia maombi ya usajili wa chama cha siasa ikiwa ni pamoja na maombi ya Chama Cha Jamii kwa kuwa ndiyo kazi yake ya msingi.

  Aidha, lilisema Tendwa anawajibika kuomba au kutafuta fedha za kumwezesha kutimiza majukumu yake ya msingi bila kutafuta visingizio kwani kutofanya hivyo ni kukwepa wajibu wake wa kisheria unaoweza kusababisha ashtakiwe kwa mujibu wa kifungu cha 6 cha sheria iliyotajwa hapo juu.

  Hivi karibuni vyombo vya habari vilimnukuu msajili huyo akiwaambia viongozi wa muda wa CCJ kuwa hana fedha za kuzunguka kufanya uhakiki wa wanachama wake na kwamba kwa sasa ana majukumu mengine muhimu ya kufanya.

  CHANZO: Tanzania Daima
   
 7. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #7
  May 31, 2010
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kutokana na hadhi yako (Mwanachama mwanzilishi) ndani CCJ nilitegemea uwe na habari za uhakika kuhusu hili na wala si tetesi, anyway ngoja tuone..!
   
 8. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mzee usiwe optimistic sana, nchi hii ni ya ajabu! Naama, inshallah!
   
 9. M

  MJM JF-Expert Member

  #9
  May 31, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Hiki ndiyo kitu walitakiwa kufanya tangu awali badala ya kujibizana kwenye vyombo vya habari
   
 10. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #10
  May 31, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280

  Heshima kwako kyachakiche,

  Unaweza kutubandikia hilo tamko la wansheria wa mkoa wa Arusha.wengine hatukubahatika kulisoma.
   
 11. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #11
  May 31, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Mkuu naona muungwana ameshatundika hapo juu.
   
 12. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #12
  May 31, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Mkuu, pitia kuanzia juu utaona ndugu yetu mmoja keshaibandika hiyo habari.
   
 13. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #13
  May 31, 2010
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Labda anaenda kuwaambia wampe hizo hela maana walisema kama hana awaeleze wao watampa.
   
 14. M

  Mkono JF-Expert Member

  #14
  May 31, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 569
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mwenyezi Mungu angesaidia Tendwa akaendelea kujifanya jeuri ili CCJ ikaendelea kujipatia ujiko hawakumbuki ile issue ya kumfukuza ZITTO ilivyompandisha chati za kisiasa!
   
 15. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #15
  May 31, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Lakini viongozi wa CCJ leo wanakanusha kuwa wamekutana na Tendwa!!!!
   
 16. A

  August JF-Expert Member

  #16
  May 31, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  hivi shughuli kuu za msajili wa vyama ni kuangalia sheria za uchaguzi au kusajili vyama, maana the mtaalamu wetu Tendwa anasema sasa hivi wapo busy na sheria za uchaguzi
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  May 31, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Taarifa ambazo nimezipata kutoka vyanzo vya uhakika toka ofisi ya msajili vinadokeza tu kuwa presha kubwa ambayo wananchi kwa kutumia mtandao wa simu wametoa kuanzia wiki iliyopita. Msajili ameonesha nia ya kutotaka mgongano na kwa kutumia hekima ameamua kufanya mazungumzo na uongozi wa CCJ leo na hatimaye kuafikiana kuanza uhakika katika mikoa minne ili kuweza kujiridhisha kuwa CCJ ina wanachama inaosema inao ili hatimaye kukipatia usajili wa kudumu.

  Tunamshukuru Msajili kwa hatimaye kuepusha mgongano uliokuwa utokee huko mbeleni pasipo ulazima na hekima imetumika. Ni matumaini yangu katika uhakiki huo watafanya kwa haki, kwa wazi na kwa kutumia vipimo vile vile ambavyo vimetumika kwa vyama vingine pasipo kukibebesha CCJ mzigo ambao chama kingine hakikutakiwa kubeba kilipojaribu kupata usajili wa kudumu.

  Tayari habari hizi zimeshagusa mamia ya watu mbalimbali nchini ambao wanasubiri kwa hamu usajili huu wa kudumu. Wakati huo huo timu za kuandika Katiba ya Kudumu ya CCJ pamoja na mambo ya Ilani, na utaratibu wa kupata wagombea ziko kazini ili kuhakikisha tu pindi CCJ ikipata usajili wa kudumu, mkutano mkuu wa kwanza wa taifa kufanyika ili hatimaye kupitisha Katiba mpya na kujipanga kuelekea Uchaguzi Mkuu.

  Habari ndiyo hiyo.
   
 18. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #18
  May 31, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  All the best. Hili Taifa ni la watu wote hata wanachama wa CCJ. Wapewe haki yao bila mizengwe mizengwe
   
 19. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #19
  May 31, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,558
  Likes Received: 1,916
  Trophy Points: 280
  Nasubiri waimege ccm kwanza mkuu!Kila la kheri na hongera kwa hatua hii!
   
 20. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #20
  May 31, 2010
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  CCM na serekali yake wapo Very very advance subirini mtajioneya wenywe .
   
Loading...