Airtel Yafunga Fibre Unit Kenya Miaka Miwili Baada ya Launch

Airtel Yafunga Fibre Unit Kenya Miaka Miwili Baada ya Launch

Omu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
401
Reaction score
86
Airtel Africa inafunga Airtel Kenya Telesonic, kampuni yake ya wholesale fibre na internet nchini Kenya, baada ya biashara hiyo kushindwa kupata revenue na kuendelea kurekodi hasara.

Financial records zinaonyesha Telesonic ilirekodi hasara ya Sh16.1 milioni mwaka 2025, kutoka Sh2.9 milioni mwaka uliotangulia, huku accumulated losses zikifikia takribani Sh19.08 milioni. Cha kushangaza zaidi, kampuni hiyo haikurekodi revenue katika kipindi hicho.

Telesonic ilikuwa imeundwa kuuza fibre capacity na bandwidth kwa kampuni nyingine, serikali, data centres, cloud providers na internet service providers—tofauti na huduma ya fibre inayouzwa moja kwa moja majumbani.

Lakini kabla biashara hiyo haijapata nafasi kubwa sokoni, Airtel iliwasilisha ombi la kurejesha Network Facilities Provider Tier 2 licence yake kwa Communications Authority mwishoni mwa 2025. Licence booklet ilirejeshwa Februari 6, 2026, na kampuni sasa inatarajiwa kuondolewa kwenye register kufikia Desemba.

Exit hiyo inatokea wakati fibre market ya Kenya inaendelea kukua. Kufikia Desemba 2025, subscriptions za fibre zilikuwa zimeongezeka hadi takribani milioni 1.4, huku Safaricom, Jamii Telecoms na Wananchi Group zikiwa miongoni mwa players wakubwa.

Hivyo, Airtel haiondoki kwenye fibre Kenya kabisa. XStream Fibre, huduma yake ya nyumba na biashara, iko chini ya Airtel Networks Kenya na haiathiriwi na kufungwa kwa Telesonic.

Source: NTV Kenya
 

Attachments

  • NTV_Kenya_-_Airtel_Fibre_Unit_Bows_Out_Airtel_Africa_is_shutting_down_its_Kenya_bNWh2S.mp4
    3.9 MB
Back
Top Bottom