Msajili abaini usiri fedha vyama vya siasa

Apr 4, 2020
16
7
1586411012485.png

OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa imemaliza kuhakiki vyama 19 vya siasa vyenye usajili wa kudumu na kubaini 18 havina uwazi katika masuala ya fedha kutokana na kutokuwa na mifumo sahihi ya kuweka fedha na kumbukumbu ya mapato na matumizi.

Aidha, tathimini ya uhakiki huo uliofanywa na ofisi hiyo kuanzia Machi 17, mwaka huu, umebaini pia kuwa, baadhi ya vyama havina akaunti ya fedha benki, jambo linalosababisha fedha nyingi kuingia katika mifuko na akaunti za watu binafsi. Hata hivyo, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeonekana kufanya vizuri katika masuala ya fedha tofauti na vyama vingine.

Katika hatua nyingine, ofisi hiyo ilikuta vyama viwili vya siasa vimegeuza sebule za nyumba za watu binafsi kuwa ofisi za vyama, huku wake zao wakiwa sehemu ya viongozi bila kufuata utaratibu. Akizungumza na gazeti hili kwa simu jana, Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Nyahoza, alisema matakwa ya sheria yameainisha maeneo yanayopaswa kufanyiwa kazi na vyama vya siasa ili kukidhi vigezo, lakini tatizo kubwa wamelibaini katika masuala ya fedha. “Kuna vyama havina akaunti ya chama kabisa.

Vingine havitumii akaunti za chama kuweka fedha bali wanaweka kwenye akaunti binafsi na wengine wanatoa mifukoni mwao kwa matumizi ya chama. Ukiondoa CCM, vyama vingine vyote ni changamoto,” alisema Nyahoza. Alisema wamebaini kuwa, kati ya vyama 19 vyenye usajili wa kudumu vilivyofanyiwa uhakiki, 18 havina mifumo mizuri ya kuweka fedha na kumbukumbu za mapato na matumizi, hivyo wamevipa miezi miwili kuhakikisha vinarekebisha eneo hilo.

Nyahoza alisema vyama vya siasa vinapaswa kuweka vitabu vya mapato na matumizi vizuri hata kama vinachangiwa fedha na wanachama au kupokea kutoka kwa wafadhali kwani ni ruhusa kisheria kupokea fedha za namna hiyo, lakini lazima uwazi katika matumizi na taarifa zioneshe hilo. Akitoa mfano wa CCM, Nyahoza alisema: “Si kwamba nawasifia, lakini mifumo yao ya mapato na matumizi iko ajili ya matumizi. Wanajiendesha kama taasisi, wana mkaguzi wa ndani na mtawala,” alisema.

Nyahoza alitaja maeneo mengine walikotoa muda wa vyama kurekebisha kasoro kadhaa kuwa ni, kufufua akaunti zisizotumika na kufungua wasiokuwa nazo na viwe vimekamilisha katika kipindi cha mwezi mmoja mpaka miwili. Alisema uhakiki huo ulihusisha kutembelea ofisi za vyama Tanzania Bara na Visiwani na kwamba walipofika Zanzibar, vyama viwili kwa nyakati tofauti vilionesha nyumba zao za kuishi kama ofisi za chama.

“Tulibaini baadhi ya vyama havina ofisi zenye hadhi ya chama (Bara na Visiwani), nyingine zina ‘fremu’ kama choo wameweka tu bango na bendera mbele, tena bendera imechomekwa jana yake baada ya kusikia tutafika.” “Tulipofika Zanzibar baadhi walitupokea sebuleni kwao, nyumba za familia nje kachomeka bendera kwenye tawi la mti.

Tukavua viatu tukakaa, mara mke akatokea akatambulishwa ni kiongozi wa wanawake wa chama, mara watoto wanachungulia,” alisema na kuongeza kuwa wameikuta hali hiyo katika vyama viwili na wamevipa miezi miwili kuwa na ofisi.

Alisema pia wamekuta vyama vitatu havina katiba wala kanuni na kwamba vimepewa wiki mbili kuwa na nyaraka hizo. Hata hivyo hakuwa tayari kuvitaja vyama hivyo na kueleza kuwa, watakuwa na mkutano navyo Aprili 16 mwaka huu na baada ya hapo, watavihakiki tena kuona utekelezaji wa maagizo hayo. Vyama vyenye usajili wa kudumu Tanzania ni CCM, Chadema, CUF, UMD, NLD, UPDP, NRA, ADA-Tadea, TLP, UDP, Demokrasia Makini, DP, APPT-Maendeleo, SAU, CCK, ADC, Chaumma, ACT-Wazalendo na NCCRMageuz
 
Vyama vyenye usajili wa kudumu Tanzania ni CCM, Chadema, CUF, UMD, NLD, UPDP, NRA, ADA-Tadea, TLP, UDP, Demokrasia Makini, DP, APPT-Maendeleo, SAU, CCK, ADC, Chaumma, ACT-Wazalendo na NCCRMageuz
In red ni wafu wanaosubiri kuoza na kuzikwa au wakioza hawanuki na hivyo hawaleti adha kwa watu
 
Back
Top Bottom