Blood Hurricane
JF-Expert Member
- Jun 21, 2012
- 1,175
- 305
Jinyonge kabla ya kutangazwa rasmi rais JM....
Unatumia mucus kufikiri.
Jinyonge kabla ya kutangazwa rasmi rais JM....
Leo jioni mida ya Saa kumi jioni nikiwa hapa Usa River, ulipita msafara mkubwa wa Waziri wa Ujenzi Ndugu Magufuli akiwa na escort nzito kama vile tayari ni Rais akisindikizwa kwa ving'ora na difenda na pikipiki za polisi.
Katika Msafara huo alikuwepo pia Mkuu wa Mkoa wa Arusha pamoja na Manyara na RPC wa Arusha na magari mengine kama 20 ya serikali.
Nauliza, hivi inaruhusiwa kwa mgombea Urais kupewa escort nzito kiasi hiko pamoja na msafara kiasi cha kutokaa foleni au ndio matumizi mabaya ya madaraka.?
Kweli kabisa mkuu, mwisho wao umekaribia...
Acha kubisha mkuu, hapakuwa na Makamu wa Rais wala Waziri Mkuu.
Nina mashaka na ubongo wako, kichwa chako kinapitisha upepo bila shaka
Alikuja hapa mererani mchana mahali alipokuwa anajinadi waliweka na makatapila akawa anayatumia kama sera yake.
Kilichonishangaza kuna jamaa m1 alikuwa na gari yake ya ndizi aliambiwa akae pembeni eti msafara wa rais unapita akabishana nao wakambeba na gari yake wakaenda kumueka selo mpaka jioni wakampiga na faini ya 50,000 kisa eti kakataa kuwa magufuli ni rais.
Kilichonikera zaidi anatumia serikali kama vile ndio rais tayari.
Huu ni uongo ulio kithiri. Tafakari upya....
Kuwa waziri lazima uwe mbunge. Bunge lilishavunjwa. Magufuli sio mbunge, sio Waziri. Rekebisha hapo kwanza.hapa Usa River, ulipita msafara mkubwa wa Waziri wa Ujenzi Ndugu Magufuli