kwanza ufahamu hio njia ya android 6 unaitoa kafara sd card yako, ukiiformat itumike kama internal ujue itabidi ikae humo humo kwenye simu, haitasoma mahala pengine. pia unaweza iformat nusu, mfano ni sd card ya gb32 unaweza ukaiformat 16gb iwe internal na 16gb ndio itumike kama sd card.
njia hii ni tofauti na njia unayotumia wewe, hii inabadilika inakuwa internal kabisa, kama simu yako internal ni 8GB then umeformAt sd card ya 64GB itumike simu itasoma ina internal 72GB.
kuhusu swali lako kwanini vitu haviendi sd card, hili ni tatizo la developer wenyewe hawataki apps zao zikae sd card na sababu kubwa ni kwamba sd card zipo slow sana compare na internal memory, app zao zikikaa kwenye sd card nazo zitakuwa slow.
kwa mtumiaji simu asielewa hilo akiona app fulani ipo slow ataichukia na kuitoa kwenye simu, hivyo mwisho wa siku anaepata hasara ni developer.
memory card nzuri za kununua ni kuanzia class 10 na UHS series lakini still hio class 10 kuna baadhi zitakuwa slow.
samsung wenyewe by default hii njia ya adoptable storage wameifungia hivyo ukiangalia kwenye setting hutaiona itabidi utumie adb kui activate.