Qunax
Senior Member
- Oct 16, 2016
- 100
- 127
Ndugu zangu wana JF nina ombi mimi ni mtumishi wa serikali katika halmashauri moja ya Mkoa wa Mtwara, nimebahatika kumuona mtoto mmoja ambae uwezo wake kisoka (football) nadiriki kumfananisha na Neymer au hata kudiriki kusema ni zaidi ya Neymer kutoka moyoni, nimeanza kushabikia mpira tangu enzi za picha za bublish za wachezaji na nimekutana na watoto wengi na washikaji kibao tangu nasoma ngazi zote ambao wanasakata ndondo kisawa sawa ila nadiriki kusema hakuna wa kumfananisha na huyu.... mpka kuja kutoa maoni hapa JF ni kujaribu kuomba msaada kama kuna namna ya kusaidiwa huyu mtoto nikijaribu kuwaza kuwa kipaji chake kitapotea hivi hivi chozi linanitoka ukizingatia anaishi katika familia duni sana, nimejaribu kufuatilia fuatilia taratibu mbali mbali za kimichezo lakini sikuona njia nitakayoweza kumsaidia huyu kijana. Hivyo ombi langu kama kuna uwezekano huyu mtoto apate timu ya kuja kuonyesha kipaji chake hata kwa dakika 5, Maana kwenye ndondo huku naona kila timu inamtumia tu na mwishoe kumlipa elf 3 au 5 ya chakula. Umri wake ni kati ya miaka 19-22, Ana speed na stamina ya ukweli, ana dribbing zilizoenda shule, shooting power yake ni ya speed ya risasi.