Kama kweli hutanii basi ushauri wangu ni kwamba, achana na mawazo hayo ya kishetani, anza kufikiria mambo chanya yaani mambo mazuri. Kumbuka tabu kila mtu duniani hupitia katika nyakati fulani na haipaswi kukata tamaa wewe mwombe Mungu wako huku ukijitahidi kufanya kazi kwa bidii. Hao unaodai wanakutegemea wasaidie kwa kadiri uwezavyo tu wasikusababishe wewe ujiue, kila mtu kazaliwa kivyake na kama siyo watoto wako wa kuwazaa mwenyewe huwezi kuwa na dhamana nao mia kwa mia, ni jukumu la jamii au serikali kuwaangalia, haiwezekani wewe ukabeba dhamana ya wadogo zako kwanza kuna ndugu wengine ni lazima watoe michango yao. Hatima ya binadamu yeyote yule ipo mikononi mwake mwenyewe hasa akishafikisha umri wa utu uzima kama wewe. Usiniambie eti unataka kujiua kisa wadogo zako, hujawazaa wewe, huna hatia nao. Ikiwezekana waombe watu wanaosaidia watoto yatima wawatunze.