kijana mkimya
JF-Expert Member
- Sep 10, 2015
- 277
- 121
niende moja kwa moja kwa jambo lilonileta hapa. wakuu tatizo kubwa lililonileta hapa, ndugu yenu siwezi kabisa kulala hotelini, siwezi kabisa kutumia mashuka, mto na kitanda cha hotel kulalia. si hotelini tu, sehemu yoyote ukiacha kitanda changu siwezi kujilaza kabisa na endapo nikitumia basi nawashwa mwili mzima mpaka natoka alama kama nimetambaliwa na chavichavi. haijalishi hoteli au sehemu niliofikia ni safi kiasi gani lazima hii hali inikute.wakuu hali hii inanifanya nikose amani kabisa pale ninapokuwa na safari maana najua siwezi kulala hata kama nikikaa mwezi, ninachofanya nakua nalala mezani kama wanavyolala wanafunzi wakiwa wanasoma mezani. wakuu nisadieni niondokane na hii hali inaninyima kufanya mambo mengi, sababu mambo mengine siwezi kufanyia nyumbani au kitandani kwangu lazima nipate sehemu ya maficho. msaada wenu unahitajika wakuu.