Msaada wanajamvi, siwezi kulala nje ya kitanda changu

Msaada wanajamvi, siwezi kulala nje ya kitanda changu

Je, kuna maagano yoyote (mfano ya kiswahili) umefanya kama vile kupata mali, elimu, mke or whatever? Na je, ukiulizia family members nao wanakuwa na shida kama yako? Nadhani hilo ni shambulio la kiroho na unahitaji kweli msaada wa haraka iwezekanavyo wa kuombewa.
 
Kama una mke basi alikuendea kwa nganga akakupa dawa ili usichepuke kame usilale nje. Na ukilala nje usilale na mwanamke mkaenjoy. Basi kama una mke ni mchawi na mbinafisi. Kukunyima raha ya usingizi,

embu sogea hapa unambie kwa siri vip ukipata mwaliko wa mechi ya kirafiki unafanyagaje ati???
 
pole sama tatizo ni dogo lkn ni kubwa 7bu hujajua chanzo nini na linatibika bila shida ni hv juzi tu nimetoka kumtibu mtu tatizokma hilo yeye ilikuwa akilala kitanda kingine ile usingizi unataka kumchukua tu anatandikwa bakora mfululizo
 
Hili tatizo sio lako peke yako,kuna wengine linaanza kuwatokea kuanzia wakiwa watoto wadogo. Mimi binafsi kinachonitokeaga ni kulala kwa muda mfupi sanaa niwapo ugenini,na sio usingizi mzito kwahiyo huwa naamka mara kwa mara hata mara 5 kwa usiku mmoja.

Hali hii nilikuja kugundua inaondoka pale nnapoenda kulala nikiwa nimetandika shuka langu juu kabisa ya kitanda then nachukua nguo yangu yoyote naitandika juu ya mto na huwa natembea na rasket mara nyingi kwajili hiyo,na hata kuoga huwa nakuwa na sabuni yangu na sio zile za guest houses. Nafikiri ni kutokana tu na Mazoea.

Kuna wengine ni kama miiko flan,unakuta mtoto ni mdogo kabisa ila ukienda kumlaza mbali na nyumbani kwao atalia usiku mzima mpaka arudishwe kwao.
Mtoa mada pitia hapa kwa makini, kuna kitu utajifunza!
 
Una allergy na ni ngumu kujua ni aina gani!

Je ukiwa kwako unaogea sabuni ipi na ugenini sabuni ipi?

Ukiwa kwako unalalia mashuka ya aina gani na ukiwa ugenini aina gani?

Ukiwa kwako unaoga maji ya baridi au vuguvugu au moto?Ukiwa hotelini maji gani waoga?

Ukiwa home unakula na kunywa kinywaji gani na ukiwa nje ya home vinywaji na chakula gani?

Kupata hasa allergy yako ni nn inachukua muda sana
 
Una allergy au tatizo linalotokana na mojawapo ya matatizo haya: Ini,figo au mchafuko wa damu. Lala kwenye gari lako ukiwa safarini au tafuta tiba.
 
Una alergy na ni ngumu kujua ni aina gani!

Je ukiwa kwako unaogea sabuni ipi na ugenini sabuni ipi?

Ukiwa kwako unalalia mashuka ya aina gani na ukiwa ugenini aina gani?

Ukiwa kwako unaoga maji ya baridi au vuguvugu au moto?Ukiwa hotelini maji gani waoga?

Ukiwa home unakula na kunywa kinywaji gani na ukiwa nje ya home vinywaji na chakula gani?

Kupata hasa alergy yako ni nn inachukua muda sana
Inaweza msaidia these reason..!!!
 
kijana mkimya

Pengine una allergy. Onana na daktari wa ngozi (dermatologist).

Kama ni shuka, itakuwa sabuni ina manukato fulani ambayo ambayo huifanya ngozi yako kuwasha. Pia, kutakuwa na vumbi ambalo linaifanya ngozi yako kuwasha. Au kuna chakula ambacho damu yako haipatani nacho.

Unaweza ukapima damu au skin test kujua kitu gani kinakufanya ujiwashe washe.

Kuna Kliniki ya Mashia wa Ithnashree karibu na msikiti wao , Mtaa wa India na Morogoro Road. Wanapima Damu kujua "allergy triggers" pale.

Pia, wanaweza kujua allergy kwa kupima katika ngozi yako. Wanaweka "allergen" ndani ya ngozi yako halafu wanaangalia kama itakuwasha. Watajua kama pollen au chakula fulani kinakudhuru.

Kumbuka, wakati mwingine ukiwa na allergy, haina dawa. Hasa, kama inatokana na kula chakula fulani au ipo katika hewa "pollen". Ila unaweza kupewa dawa (cream au vidonge) kupunguza uwasho.

Kwa Kiingereza, vipimo utakavyohitaji ni hivi:

Allergy blood test (immunoassay tests)

1. Enzyme-linked immunosorbent assay (ELISA)

2. Radioallergosorbent test (RAST)

Na

3. Skin test (intradermal test)
 
Hilo tatizo ni kwa hotel za tz tu au mpaka ile ndefu ya pale dubai

Tukianzia hapo tatizo lako itakuwa ni easy kulifunga
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom