Msaada wadau, Mtoto mdogo wa mwaka mmoja amekatazwa vyakula, ana allergy sasa

Atui

Member
Jun 18, 2022
60
61
Mtoto mdogo wa mwaka mmoja amekatazwa ana allergy sasa

Samaki
Maziwa ya unga na ng'ombe
Karanga
Dagaa
Soya maharagwe
Korosho
Vyakula vyenye rangirangi
Uji wa lishe
Sasa wakuu huyu anapewa vyakula gani? Apate protini
 
Mtoto mdogo wa mwaka mmoja amekatazwa ana allergy sasa

Samaki
Maziwa ya unga na ng'ombe
Karanga
Dagaa
Soya maharagwe
Korosho
Vyakula vyenye rangirangi
Uji wa lishe
Sasa wakuu huyu anapewa vyakula gani? Apate protini
Kwa umri huo haishauriwi kabisa kumpa hivi vyakula maziwa ya mamaake yanatosha kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoto mdogo wa mwaka mmoja amekatazwa ana allergy sasa

Samaki
Maziwa ya unga na ng'ombe
Karanga
Dagaa
Soya maharagwe
Korosho
Vyakula vyenye rangirangi
Uji wa lishe
Sasa wakuu huyu anapewa vyakula gani? Apate protini
Kwa umri huo haishauriwi kabisa kumpa hivi vyakula maziwa ya mamaake yanatosha kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa umri huo haishauriwi kabisa kumpa hivi vyakula maziwa ya mamaake yanatosha kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuuu
Kitatibu, mtoto anatakiwa kunyonya maziwa ya mama pekee Kwa muda wa miezi 6 (exclusive breastfeeding)na baada ya hapo anaanza kupewa mchanganyiko wa vyakula pamoja na maziwa. (Complementary breastfeeding)
(Ananyonya huku anakula vyakula mbali mbali Hadi atakapofikisha miaka miwili ndo anaachishwa kunyonya)
Back to the topic, sidhan kama ni allergy kweli kwenye vyakula vyote hvyo
Inawezekana shida ipo kwenye kuandaa (vyakula haviandaliwi katika hali ya usafi au vile inavyotakiwa) au kwenye kuchanganya vyakula (Kuna baadhi ya vyakula ukivichanganya, vinakua na madhara)
Mwaka mmoja Bado ni mdogo sana, hvyo Kwa ushauri wangu...zingatieni uandaaji Bora wa chakula chake na pia anzeni na kitu kimoja kimoja na sio kumpa mchanganyiko Kwa wakati mmoja
 
Kwa umri huo haishauriwi kabisa kumpa hivi vyakula maziwa ya mamaake yanatosha kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app

mkuu mtoto wa mwaka siyo rahisi kutoboa na maziwa ya mama peke yake

Anahitaji energy zaidi kwa sababu Ameshaanza activities

By the way huwa nafatilia nakala za vyakula Vya Watoto

Wanasema tujitahidi kuanza na vyakula ambavyo ni allergic ili kupunguza reactions kadri mtoto anavyokua

Nimekua nikifanya hivi kwa Watoto wangu kuanzia miezi minne

Sijapata mtoto ana reaction na chakula chochote.
 
Mtoto mdogo wa mwaka mmoja amekatazwa ana allergy sasa

Samaki
Maziwa ya unga na ng'ombe
Karanga
Dagaa
Soya maharagwe
Korosho
Vyakula vyenye rangirangi
Uji wa lishe
Sasa wakuu huyu anapewa vyakula gani? Apate protini
Je umemuona pediatrician (dkt wa watoto) ndo kakupa hayo maelekezo au umeenda hospital ya alergy wamempima tu?? Alikuwa na shida gani hadi wampime alergy?? Hii iliwahi kunitokea mtt mdg alikuwa anawashwa mwilini nilizunguka sana nikaenda hospital ya alergy wakampima wakasema anaalergy karibu kila kitu we hivyo vyako vichache alibaki kunywa supu tu ya kuku wa kienyeji. After 1 week ile hali haikuacha Nikarudi kwa pediatrician kiukweli nilivyomuelezea aliniuliza we mama ni mchawi??? Humpi mtoto hivyo vitu vyote atakuaje?? Aliniuliza maswali ambayo ntakuuliza na wewe ujiasess
1. Je hivyo vyote ulikuwa unampa kwa mkupuo??
2.hiyo hali anayo toka amezaliwa??
3.je hivyo vyakula hali siku zote je siku hajala hali ilikuwa ni ahueni??
4.je mwanzo alikuwa anakula havimdhuru au vinamdhuru??

Well, akasema nimekosea sana kumuachisha vile vyakula na nianze kuvirudisha kimoja baada ya kingine... Ila akanirefer kwa specialist wa ngozi ambaye aligundua ugonjwa wa ngozi tena unaotibiwa na dawa tu ya 2500 pharmacy. Na nikamrudishia vyakula vyote na havijawahi kumdhuru mpaka leo anadunda
Nb: yule specialist aliniambia kwenye alergy kuna mambo mengi na pia kuna biashara ndani yake so ni kuwa makini sana na kupima mahali tofauti na pia daktari husika kumtibu mtoto ni muhimu saaana.
I hope utapata kitu kupitia story yangu.. Namuombea speed recovery.
 
Back
Top Bottom