Umuhimu wa Mbegu za Chia katika Ukuaji wa Mtoto

Aug 31, 2022
54
99
chia-seeds_annotated-2f7ca595a9bd4342a8f70623be8d9985.jpg


Mbegu za chia ni kati ya vyakula mashuhuri kwa afya bora, kwa sababu ya kusheheni virutubisho vya mwili.

Gram 100 zimesheheni:- Fibers: 39 gm, Protini: 16 gm, mafuta: 37 gm (18 gm ikiwa ni Omega-3, iliyomuhimu katika kuimalisha ubongo na 6 gm Omega 6); Madini kwa kiwango kinachohitajika kwa siku: calcium: 64%, Manganese: 107%, Magnesium: 107% na phosphorous: 96%.

Mbegu za Chia zina viwango vizuri vya vitamin A, B, E na D, madini joto (iodine), madini ya chuma, sulfa, zinc, na chemikali za kulinda mwili (anti-oxidants) na viinilishe vya tindikali mafuta (essential fatty acids).

Hivi ni virutubisho muhimu vinavyopatikana ndani ya mbegu hizi kwa kila gramu 100 (kijiko kimoja)

Faida kubwa za mbegu hizi kwa watoto ni pamoja na kuwa chanzo kizuri cha protini,kuupa mwili wa mtoto nguvu,chanzo kikubwa cha omega 3 na 6 ambazo ni muhimu kwa ukuaji wa ubongo wa mtoto.

MBEGU ZA CHIA ZINAWEZA KUPEWA KWA WATOTO CHINI YA MWAKA MMOJA?

Ndio,Mbegu hizi zinaweza kupewa kwa watoto walio na umri kuanzia miezi 6 kuendelea na ambao tayari wameanza kupewa vyakula vingine tofauti na maziwa ya mama,mfano uji nk.

Japo zinapaswa kupewa kwa kiwango kidogo kulinganisha na watu wenye umri mkubwa.Mtoto anahitaji kuwekewa nusu kijiko cha chai kwenye chakula.maelezo ya jinsi ya kumpa yapo mbele kwenye makala hii.

FAIDA ZA KUWAONGEZEA WATOTO MBEGU ZA CHIA KWENYE CHAKULA

1.CHANZO KIZURI CHA PROTINI.
Mbegu hizi zina sifa ya kuwa na kiwango kikubwa cha protini hivyo kuwa chanzo kizuri sana cha protini.Ndani ya gramu 100 (kijiko kimoja cha chai) kimesheheni gramu 16 za protini.
Kama tunavyojua proteini ni mojawapo ya kirutubisho kinachosaidia katika ukuaji wa mwili.
Unaweza kumuongezea mtoto wako mbegu hizi katika kila chakula unachomwandalia.

Zifuatazo ni faida za protini mwilini:
Ukuaji wa mwili na akili
kutengeneza seli mpya za mwili,
kukarabati seli zilizochakaa au kuharibika;
kutengeneza vimeng’enyo(enzymes), vichocheo(hormones), damu na mfumo wa kinga,
huupa mwili nguvu pale ambapo kabohaidreti haitoshelezi mahitaji ya mwili.

2.CHANZO KIKUBWA CHA ANT OXIDANTS
Antioxidants ni viini ambavyo vina uwezo wa kukinga seli za mwili zisiharibiwe na chembechembe haribifu (free radicals) ambazo huweza kusababisha saratani na magonjwa mengine. Viini hivyo huungana na chembechembe hizo haribifu na kuzidhibiti ili zisisababishe madhara. Ant oxidants zinazopatikana kwenye mbegu hizi kwa wingi ni vitamini C, E, na A.

Kuhusu vitamin E
Huondoa chembe haribifu mwilini, husaidia umetaboli wa seli za damu, huimarisha kinga ya mwili, hupunguza kasi ya seli kuzeeka kiurahisi, hukinga seli nyekundu za damu kuharibiwa na chembe haribifu mwilini; kinga dhidi ya saratani.

vitamin C
Kusaidia matumizi ya madini ya chokaa, ufyonzwaji wa madini chuma, huboresha kinga ya mwili na kuondoa chembe haribifu mwilini. Husaidia kuimarisha mishipa ya damu, huzuia uvujaji wa damu ovyo, husaidia umetaboli wa protini.

Vitamin A
Ukuaji wa akili na mwili, kuimarisha seli za ngozi, kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya maradhi, kusaidia macho kuona vizuri, kulinda utando laini katika sehemu mbalimbali za mwili.
Vitamini zote hizi zinapatikana kwa wingi ndani ya mbegu hizi.

3.CHANZO KIZURI CHA FIBERS
Sababu nyingine ya kumpatia mtoto mbegu za chia ni kwamba zina kiwango kikubwa cha dietary fibers.hizi husaidia kuimarisha mfumo wa chakula na kuzuia matatizo kama kukosa choo au kupata choo kigumu sana (constipation) pia kumkinga mtoto na tatizo la chango( abdominal colic) kwa watoto.

4.KUIMARISHA AFYA NA UKUAJI WA UBONGO

Chia seeds zina kiwango kikubwa cha Omega -3 na Omega- 6 Fatty acids ambazo ni muhimu sana katika kusaidia ubongo kutengeneza seli zake.

5.CHANZO KIZURI CHA CALCIUM
Ambayo ni muhimu kwa uimara wa mifupa na meno.

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA UNAPOMPA MTOTO MBEGU ZA CHIA.
1.CHAGUA MBEGU BORA NA SAFI.

Unaponunua mbegu za chia hakikisha unachukua mbegu ambazo hazina uchafu kama nyasi,magugu nk,pia chagua mbegu zilizokomaa(utaona zina rangi nyeusi au nyeupe na sio za njano)

2.KIASI KWA SIKU.
Mpatie mtoto kiasi cha kijiko cha chai 1 hadi 2 kwa siku.

JINSI YA KUZIANDAA
Kwa mtoto anza kwa kuziweka mbegu zako kiasi unachotaka kumpa mfano kijiko kimoja hadi 2 kwenye glasi au kikombe kisha ongezea maji nusu kikombe na uziloweke kwenye maji usiku mzima. mbegu hizi zikifyonza maji zinavimba na kutengeneza ute mzito (jelly). hapa sasa unaweza kuziweka kwenye chakula chochote mfanom kwenye uji,supu,maziwa, boga, matunda nk.

Usimpe mtoto mdogo mbegu ambazo hujaziloweka kwenye maji kwani zitampelekea kumfanya kupata kiu sanan na saa nyingine kumpelekea tatizo la tumbo kujaa gas.

Mbegu hizi pia unaweza kuongezea kwenye mchanganyiko wako wa unga wa lishe na kuzisaga kwenye unga wako wa lishe.

1674297814842.png
 
Back
Top Bottom