Kuna vyakula ukivichanganya vinakuwa sumu

Kindeena

JF-Expert Member
Sep 27, 2017
9,067
15,815
Aina sita ya vyakula ambavyo vikichanganywa hugeuka sumu

Kila binadamu ana kile alichojaaliwa na Mungu. Siku zote anachoamua mmoja kula huenda kikawa sumu kwa mwingine. Chakula anachokula mtu kinaenda sanjari na hali ya kiafya. Wengine huumwa hadi kusababisha kupoteza uhai na hii ni baada tu ya kupendelea kuchanganya chakula.

Mtu mmoja anaweza kula sawa na kwa urahisi, ila kwa mwingine kikageuka sumu. Hali hii huchochewa zaidi na matokeo ya baadae pale unaposhindwa kuweka mchanganyiko sahihi na wenye afya zaidi.

Kila aina chakula ina faida zake, ila kinapochanganywa kinaweza kusababisha shida kwa mtu. Kwa watu ambao wanataka kuchanganya lishe ili kupunguza unene na vichocheo vyake ni vyema kushauriana na wataalamu jinsi ya kupanga lishe bora.

Mtaalam wa lishe wa Nigeria Habiba Haruna ameiambia BBC kuhusu aina sita za chakula ambazo zinaweza kuwa sumu kwa mtu yeyote.

Samaki na Maziwa
samaki
Samaki na Maziwa ni vyakula vyenye virutubisho lukuki na kuvichanganya katika sehemu moja vinaweza visiwe na uwezo wa kutengeneza virutubisho sahihi na hii inaweza kuleta shidbaadaye.

Mwili wa binadamu hauhitaji vyakula vya aina tofauti vyenye kemikali za aina moja kuchanganywa. Huweza kusababisha sumu itakayopelekea mtu kutapika na hata kuharisha.

Maji ya limao na Maziwa
Maziwa na limao huwa haviwezi kukaa sehemu moja kwani vikichanganywa lazima maziwa yaweze kukatika. Ikiwa mtu atachanganya maziwa na maji ya limao anaweza kutengenezea sumu, vilevile yanaweza kuleta shida katika moyo.

Karanga na Mafuta ya mzeituni
Karanga ina umuhimu mkubwa sana katika mwili wa binadamu na hutumika katika sehemu nyingi sana.

Pia karanga ina kiwango kikubwa sana cha protini na wanga, vilevile karanga ni moja ya virutubisho muhimu katika lishe, haswa kwa wale ambao wanataka kupunguza uzito.

Kwa mafuta ya mzeituni yanamsaada mkubwa pia hasa katika masuala ya tiba kwa baadhi ya magonjwa, lakini mchanganyiko wa mafuta hayo na karanga yanaleta shida ila inashauriwa kutumika pale moja inapokosekana lakini sio kwa pamoja.

Dawa pamoja na sharubati ya limao
Kuchukua dawa na kuchanganya na kitu chenye gesi ina madhara makubwa, wataalamu wanasema kuwa kunywa dawa na soda kama fanta au Coca-Cola inaweza kukusababishia kifo kutokana tu ongezeko kubwa la gesi.

Ameongeza kwa kusema kuwa limao au kinywanji chochote chenye gesi hakipaswi kuchanganywa na dawa ni hatari.

Nyama na mayai mabichi
Kuchanganya nyama ambayo haijaungwa na mayai mabichi inaweza kusababishia matatizo katika mwili wa binadamu. Inaweza kuwa sumu kwa wengine, zingine zinaweza kusababisha kutapika na kuhara kwa sababu haifai kutumika hivyo.

Nyama mbichi inaweza kusababisha athari ikiwa usindikaji wake haufuatwi ili kupunguza kiwango cha virutubishi vilivyomo.

Mtaalamu anasema kuwa mayai mabichi hayana virutubisho kwenye mwili wa binadamu, yakiwa bado kwenye hali hiyo hayapaswi kuliwa mpaka pale yatakapochemshwa au kukaangwa ndio hujenga mwili.

"Mayai mabichi siyo ya kuyaamini," Anasema Mtaalamu wa chakula kutoka Nigeria, Habiba Haruna. Wataalamu wanashauri watu kula kile wanajua kitakuwa na faida na haitawasababishia matatizo yoyote.

Kujaribu kitu kipya kunaweza kuwa na faida kwa wengine lakini pia kunaweza kuwa na madhara. Kuna aina nyingi sana ya vyakula ambavyo vikichangwanywa vinaweza sababisha madhara.

Mtu anapaswa kuwa mwangalifu katika uchaguzi wa vyakula ni vyema aweke vyema virutubisho na kuepuka kuvichanganya.

BBC News, Swahili
 
Asali ikipakwa kwenye majani ya mihogo mbuzi wakigusa hapo hawatoboi.(not my intention kuchululia comment hii somo)
 
Nasikia pia asali na tango pia si vzr ni kweli?
Mkuu niliwai kuona kwa ma angu mdg alikua mchoyo kinoma noma.
Ametoka kutafuta tango peke ake alivomaliza akaenda kulamba asali ilikua kweny ki dressing table chake chumbani.
Baada ya dk kadhaa katoka chumbani kwake anasweat kweli kweli nkamuuliza akasema siko poa... Nkamuuliza umeenda chumbani ukala tena nn ety asali nkamwambia ww unataka kujiua ww.... Alitoa mimacho moyo mara anasema tumbo mara nn tulimpa tu maziwa alikesha bila kulala anaogopa atadead
 
Yawezekana mkuu.
 
Na hata uchanganyaji wa Aina tofauti tofauti za Matunda pia ni hatari kwa afya mfano....

Tikiti, chungwa, Tango.
Tango, karoti, Ndizi, parachichi.
Embe, Nanasi,miwa, ndizi nk

Hii ni hatari Sana.

NB.
UKILA ASALI NA TANGO UNAKUFA.
 
Ngoja ni Google nipate majibu ya wataalam ,maana kule kuna expert wamefanya tafiti za kina na sio majibu ya ramli
 
Na hata uchanganyaji wa Aina tofauti tofauti za Matunda pia ni hatari kwa afya mfano....

Tikiti, chungwa, Tango.
Tango, karoti, Ndizi, parachichi.
Embe, Nanasi,miwa, ndizi nk

Hii ni hatari Sana.

NB.
UKILA ASALI NA TANGO UNAKUFA.
Hii haina ukweli...!! Kula Tango na asali unakufa...?? Mm nlishakula Tango na asali mbona bado naishi na nipo hapa nmequote comment yako.
 
Hii haina ukweli...!! Kula Tango na asali unakufa...?? Mm nlishakula Tango na asali mbona bado naishi na nipo hapa nmequote comment yako.
Acha uongo usije kuua watu bure kwa masiara yako...Mimi kuna mzee jirani alikuwa anabisha akajaribu, haikupita hata nusu saa akaanza kutema povu
 
Pia Ukitaka kuona ngo'mbe wanakufa kama utitiri watilie tu asali kwenye chakula chao.. itakua historia na haichukui sekunde
Hii nimeijaribu jana. Asee lile ng'ombe bado zima na linagegeda kama limetumwa.

Nimepanga kuliua kwa kisu maana linawapiga sana wenzie likiwahisi wanataka kula tunda kimasihara lwa mademu zake
 
Acha uongo usije kuua watu bure kwa masiara yako...Mimi kuna mzee jirani alikuwa anabisha akajaribu, haikupita hata nusu saa akaanza kutema povu
Huyo alikuwa na maagano yake na ziraili. hili nalipinga kwa 100%. Nimeshabishana sana na nimeshagonga mbele ya wabishi kama wewe...

Au twende basi hata kwenye sayansi ndogo tu. Nini kiko kwenye asali ambacho kitakutana na kilichopo kwenye tango afu kitengeneze sumu kama ya nyoka koboko ???
 
Hii nimeijaribu jana. Asee lile ng'ombe bado zima na linagegeda kama limetumwa.

Nimepanga kuliua kwa kisu maana linawapiga sana wenzie likiwahisi wanataka kula tunda kimasihara lwa mademu zake

Oya acha masiara. Ng'ombe na mbuzi yeyote akila asali LAZIMA AFE. narudia tena, Ng'ombe na mbuzi akila asali LAZIMA AFE.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom