Msaada wa ushauri mahusiano yangu yamevurugika

Ila bro ile Pm yako sijaweza kuifungua co Pm yangu inazingua maana ata baada ya kuirestart simu bado imegoma kufnguka so yale material ulionitumia bado sijafanikiwa kuyasoma mkuu
Dah pole sanaa mdogo wangu!

Ila shukuru hapo hujatoa mahali, je ungekuwa umetoa mahali?

Mda mwingine kuyumba kwetu kiuchumi huwa inakuwa sababu moja wapo ya hawa mabinti kutukimbia hasa tunapokuwa tushaanza relation,,

Wenzetu huwa hawakai na kitu moyoni,, huwezi amini yale yote yaliyotea kabla na baada, ameshaongea kwao,, kuna wale mama wadogo, mashangazi na mabibi wameshapitisha uamuzi kuwa aachane na wewe, ila hawezi kukwambia kuwa ameshauriwa ivo,,

Cha kufanya mdogo wangu kama wewe una hofu na Mungu anza kusali, hii itakupa mguvu mpya kidogo kuona unapunguza mzigo uliopo kichwani,, alafu jaribu kuwasimulia wakubwa wako kama makaka zako,, hao watakupa ushauri utakao kujenga vizuri kuanzia sasa, alafu hao hao kaka zako utagundua kuwa wapo waliopitia hayo uliyopita wewe na mda mwingine huenda wao waliumizwa zaidi yako sema ndo ivo walipigana wakatoka ktk hicho kifungo huru,,

Mawazo hayataisha leo wala kesho hadi pale utakapopata tulizo la nafsi yako, na hata ukipata bado utakuwa unakumbuka kumbuka haya yaliyokea, kwa sababu ulishamwingiza moyoni, na ukumbuke kumtoa mtu moyon hasa mpenzi si kitu rahisi kama vile unavodhani,, ila kikubwa unahitaji kujichanganya sana na marafiki ili kupunguza msongo wa mawazo,, hata kg nahisi zimepungua kwako.

Jaribu kukumbuka kabla ya kuwa naye je ulikuwa unapata pesa na inakaa? Je matumizi yaliongezeka sanaa? Kama jibu ndiyo basi tambua kwamba nia yako haikuwa mbaya ila ni kwamba hukujiandaa kubeba mahitaji yake yote,, sasa na yeye alivoona ivo uvumilivu ukamshinda na saa nyingine alisingizia akatibiwe kwao labda alihisi kuendelea kukaa hapo angezidi kuumia zaidi,, hawa viumbe wanafikri mara nyingi kuliko sisi,,

Mdongo wangu huyo hakuwa fungu lako ndo maana umempigania kadri ulivojaliwa, mda mwingine ulijinyima na pia ulikopa mahala flani na pia amekuachia madeni kadhaa japo unayajaribu kuyalipa lakini ndo ivo,, japo si kweli kama una madeni mengi [emoji23]

Ila bado na wewe sijajua mapungufu yako yapi maaana hizi kesi za upande mmoja huwa tunatoa majibu kwa upande huo huo,, ila kama na yeye angeongea yake basi huenda tungegundua mengi zaidi ambayo yamejificha,

PITIA HII KWANZA ALAFU UTOE COMMENT YAKO KIJANA,,

Nna mengi ya kuandika mdogo wangu basi tuuuu huku kutype kunaninyima uhuru wa kuandika hapa,
 
Hongera hasa kwa kuwa na mapenzi ya kweli ukiwa wewe mi "me"maana naona na uvumilivu pi unao

Mapenzi ni maisha na maisha aio leo tu fikiria na kesho pia yapange haya mawili na uchague moja la muhimu kwako

Kupenda wewe tu na usipendwe au
Kupenda wewe na ukapendwa pia
Haya chagua.....!
Wakuu habari za asubuhi, kama kichwa kinavyojielezea kuna mwanamke niko naye kwenye mahusiano kwa muda wa miaka miwili sasa lakini baada ya muda tuliojiwekea kwamba tuharalishe mahusiano yetu mwenzangu anaonekana kama tayari ame loose interest na mimi na hataki tena niende kwako,

Story ya mahusiano yetu iko ivi

Mwaka 2018 /01 /01 mimi na uyu binti tulianza rasmi mahusiano yetu kila mmoja akiwa anampenda mwenzake kwa dhati sana ilituchukua miezi minne katika mahusiano yetu tukaamua tuanze kuishi pamoja kienyeji nikimaanishaa yeye kutoka kwao na kuja kwangu tukaanza maisha,

Maisha yetu yalikuwa ya furaha japo ups and downs hazikukosa zikiwa zabkutosha tu kama ilivyo ada ya mahusiano yoyote yale baada ya miezi 5 ya kuishi pamoja mwenzangu alipata tatizo la kuugua na tukakubaliana aende nyumbani akanywe dawa za asili maana dawa za hospitali zilidunda nilitafuta nauli akaenda om mi nikaendelea na mishe mishe za maisha uku nikiendelea nae japo kwa kusua sua kama mnavyojua japo mapenzi yangu kwake hayakuwahi kupungua lakini kama binadamu yeyote yule kupitiwa kupo hasa kukiwepo na umbali kati ya wenza wawili.

Muda umeenda sana na kwa sasa muda rasmi niliomuahidi kwamba ndo muda tunaotakowa kuhararisha mahusiano yetu
Kushughurikia taratibu za kimila kidini na mambo mengine ndo umewadia.

Lakini baada y kumgusia mwenzangu swala hili hajalipokea kama nilivyotarajia na pia ushirikiano wake kwangu umekuwa mdogo sana na kuna muda ananiambia ili swala lisubiri kwanza ama tusilifanye kabisa kifupi nimeshindqa kumuelewa na imekuwa kinyume na matarajio yangu mambo yapo mengi yaliyotokea apo katikati katika safari yetu kuanzia tulipoanza mahusiano mpaka leo na siwezi kuyaandika yote nikayamaliza .

Wakuu naomba msaada wa kimawazo mtu mtu uyu nimfanyeje nimwelezeje ama nitumie nini ili niwese kumrudisha kwangu maana kwa sasa inaonyesha mapenzi yake kwangu yamepungua na pia najua kuna mwana anaweza naye akawa member wa Jf na akasoma huu uzi labda ndo anatoka naye kwa sasa na ndo amemfanya abadiri malengo

Kifupi uyu ni mwanamke ninayempenda sana sana sana namuhitaji mnowala sihitaji kumpoteza maana mapenzi yangu kwake ni makubwa lakini kwa kwa sasa amekuwa ni mtu ananifungia mlango hanipi ushirikiano sometimes majibu yake ni ya kuniumiza mno.

Nakiri mimi ni binadamu nina mapungufu yangu kama alivyo yeye .

Mwisho naomba msaada kwa yeyote yule ambaye aliwahi kuipitia hali kama hii na akaishinda alifanyaje alitumia nini ama alimtumia nani namaanisha aliyepitia hali hii na akafanikiwa kumrjesha himayani mwenzi wake basi anipwe msaada kimawazo kiushauri ama msaada wowote anaoweza kuutoa kwangu ili mradi nifanikiwe kumrejesha uyu shemeji yenu na wifi yenu himayani tafadhali wakuu.

Hili jambo ni serious mno kwangu na kwa ustawi wa afya yangu japo najua kuna watakao nibeza kuniona boya kunisimanga yote ni sawa maana hii hali na machungu haya ninaye yapitia ni mimi

Bado naamini Jf ni sehemu salama na bado kuna waungwana wengi na wenye hekima na busara wengi ivyo naamini nitapata msaada wa kutataua changamoto yangu

Ankai ..nwasirisha!!

Nb pm yangu iko wazi ntashukuru kwa msaada na kejeli yoyote mtakayonipatia.
 
Yeah kaka nimeiona hii nondo bt mi nadhani acha nitimize jukumu langu the rest nimwachie yeye ndo atadecide
Mambo yaliingiliana mkuu, ntakucheki leo muda wowote. Nilichukua contact zako.
 
Dah pole sanaa mdogo wangu!

Ila shukuru hapo hujatoa mahali, je ungekuwa umetoa mahali?

Mda mwingine kuyumba kwetu kiuchumi huwa inakuwa sababu moja wapo ya hawa mabinti kutukimbia hasa tunapokuwa tushaanza relation,,

Wenzetu huwa hawakai na kitu moyoni,, huwezi amini yale yote yaliyotea kabla na baada, ameshaongea kwao,, kuna wale mama wadogo, mashangazi na mabibi wameshapitisha uamuzi kuwa aachane na wewe, ila hawezi kukwambia kuwa ameshauriwa ivo,,

Cha kufanya mdogo wangu kama wewe una hofu na Mungu anza kusali, hii itakupa mguvu mpya kidogo kuona unapunguza mzigo uliopo kichwani,, alafu jaribu kuwasimulia wakubwa wako kama makaka zako,, hao watakupa ushauri utakao kujenga vizuri kuanzia sasa, alafu hao hao kaka zako utagundua kuwa wapo waliopitia hayo uliyopita wewe na mda mwingine huenda wao waliumizwa zaidi yako sema ndo ivo walipigana wakatoka ktk hicho kifungo huru,,

Mawazo hayataisha leo wala kesho hadi pale utakapopata tulizo la nafsi yako, na hata ukipata bado utakuwa unakumbuka kumbuka haya yaliyokea, kwa sababu ulishamwingiza moyoni, na ukumbuke kumtoa mtu moyon hasa mpenzi si kitu rahisi kama vile unavodhani,, ila kikubwa unahitaji kujichanganya sana na marafiki ili kupunguza msongo wa mawazo,, hata kg nahisi zimepungua kwako.

Jaribu kukumbuka kabla ya kuwa naye je ulikuwa unapata pesa na inakaa? Je matumizi yaliongezeka sanaa? Kama jibu ndiyo basi tambua kwamba nia yako haikuwa mbaya ila ni kwamba hukujiandaa kubeba mahitaji yake yote,, sasa na yeye alivoona ivo uvumilivu ukamshinda na saa nyingine alisingizia akatibiwe kwao labda alihisi kuendelea kukaa hapo angezidi kuumia zaidi,, hawa viumbe wanafikri mara nyingi kuliko sisi,,

Mdongo wangu huyo hakuwa fungu lako ndo maana umempigania kadri ulivojaliwa, mda mwingine ulijinyima na pia ulikopa mahala flani na pia amekuachia madeni kadhaa japo unayajaribu kuyalipa lakini ndo ivo,, japo si kweli kama una madeni mengi [emoji23]

Ila bado na wewe sijajua mapungufu yako yapi maaana hizi kesi za upande mmoja huwa tunatoa majibu kwa upande huo huo,, ila kama na yeye angeongea yake basi huenda tungegundua mengi zaidi ambayo yamejificha,

PITIA HII KWANZA ALAFU UTOE COMMENT YAKO KIJANA,,

Nna mengi ya kuandika mdogo wangu basi tuuuu huku kutype kunaninyima uhuru wa kuandika hapa,
Thanks bro asante sana kwa ushauri mzuri na makini hakika nitajitajidi kuufanyia kazi huu uwhauri wako nashukuru sana kaka!!
 
Nyumba yake inaungua, unamshuri afagie uwanja!!!!
Daaah nduugu wee acha watu huwa wanazijua akili zao wao wenyewe tu unashangaa sijui mtu anawaza nini asee!!
 
Mambo yaliingiliana mkuu, ntakucheki leo muda wowote. Nilichukua contact zako.
Sawa kaka nitashukuru sana kama utakuwa sehemu ya msaada kwangu nakusubiri kaka!!
 
Mkuu ukiona demu umemtangazia dau la ndoa ila anachomoa jua hakutaki........narudia tena hakutaki, tafuta mwanamke mwengine wa kuoa
 
Sawa kaka nimekuelewa
 
Ushauri wangu kama dada mkubwa:ukiona hana interest jitahd kuendelea na maisha yako japo n ngumu lakn ndo maisha yenyewe huwez pata kila kitu unachotaka,wakat mwingine inabid ukubaliane na hali yenyewe anyway jaribu kumsogeza Karibu ila ukiona kuna nature ya kulazimishana we chapa rapa
 
Umbal pia unaeza kupelekea kuharibu mahusiano na inawezekana alishapata mtu mwingine sasa ww mtu uende kijijin ukae mda wote huo na wakat before mlikuwa na uchumba sugu s utasema labda mwenzangu hanitak tena,nahis kumpotezea mda wote huo ulifanya kosa kubwa jaribu kumweka tena karibu
 
Kama ningekuwa wewe, ningetumia muda wangu na nguvu zangu zote kwenye mambo mengine yenye umuhimu tofauti na hilo.
 
Wakuu habari za asubuhi, kama kichwa kinavyojielezea kuna mwanamke niko naye kwenye mahusiano kwa muda wa miaka miwili sasa lakini baada ya muda tuliojiwekea kwamba tuharalishe mahusiano yetu mwenzangu anaonekana kama tayari ame loose interest na mimi na hataki tena niende kwako,

Story ya mahusiano yetu iko ivi

Mwaka 2018 /01 /01 mimi na uyu binti tulianza rasmi mahusiano yetu kila mmoja akiwa anampenda mwenzake kwa dhati sana ilituchukua miezi minne katika mahusiano yetu tukaamua tuanze kuishi pamoja kienyeji nikimaanishaa yeye kutoka kwao na kuja kwangu tukaanza maisha,

Maisha yetu yalikuwa ya furaha japo ups and downs hazikukosa zikiwa zabkutosha tu kama ilivyo ada ya mahusiano yoyote yale baada ya miezi 5 ya kuishi pamoja mwenzangu alipata tatizo la kuugua na tukakubaliana aende nyumbani akanywe dawa za asili maana dawa za hospitali zilidunda nilitafuta nauli akaenda om mi nikaendelea na mishe mishe za maisha uku nikiendelea nae japo kwa kusua sua kama mnavyojua japo mapenzi yangu kwake hayakuwahi kupungua lakini kama binadamu yeyote yule kupitiwa kupo hasa kukiwepo na umbali kati ya wenza wawili.

Muda umeenda sana na kwa sasa muda rasmi niliomuahidi kwamba ndo muda tunaotakowa kuhararisha mahusiano yetu
Kushughurikia taratibu za kimila kidini na mambo mengine ndo umewadia.

Lakini baada y kumgusia mwenzangu swala hili hajalipokea kama nilivyotarajia na pia ushirikiano wake kwangu umekuwa mdogo sana na kuna muda ananiambia ili swala lisubiri kwanza ama tusilifanye kabisa kifupi nimeshindqa kumuelewa na imekuwa kinyume na matarajio yangu mambo yapo mengi yaliyotokea apo katikati katika safari yetu kuanzia tulipoanza mahusiano mpaka leo na siwezi kuyaandika yote nikayamaliza .

Wakuu naomba msaada wa kimawazo mtu mtu uyu nimfanyeje nimwelezeje ama nitumie nini ili niwese kumrudisha kwangu maana kwa sasa inaonyesha mapenzi yake kwangu yamepungua na pia najua kuna mwana anaweza naye akawa member wa Jf na akasoma huu uzi labda ndo anatoka naye kwa sasa na ndo amemfanya abadiri malengo

Kifupi uyu ni mwanamke ninayempenda sana sana sana namuhitaji mnowala sihitaji kumpoteza maana mapenzi yangu kwake ni makubwa lakini kwa kwa sasa amekuwa ni mtu ananifungia mlango hanipi ushirikiano sometimes majibu yake ni ya kuniumiza mno.

Nakiri mimi ni binadamu nina mapungufu yangu kama alivyo yeye .

Mwisho naomba msaada kwa yeyote yule ambaye aliwahi kuipitia hali kama hii na akaishinda alifanyaje alitumia nini ama alimtumia nani namaanisha aliyepitia hali hii na akafanikiwa kumrjesha himayani mwenzi wake basi anipwe msaada kimawazo kiushauri ama msaada wowote anaoweza kuutoa kwangu ili mradi nifanikiwe kumrejesha uyu shemeji yenu na wifi yenu himayani tafadhali wakuu.

Hili jambo ni serious mno kwangu na kwa ustawi wa afya yangu japo najua kuna watakao nibeza kuniona boya kunisimanga yote ni sawa maana hii hali na machungu haya ninaye yapitia ni mimi

Bado naamini Jf ni sehemu salama na bado kuna waungwana wengi na wenye hekima na busara wengi ivyo naamini nitapata msaada wa kutataua changamoto yangu

Ankai ..nwasirisha!!

Nb pm yangu iko wazi ntashukuru kwa msaada na kejeli yoyote mtakayonipatia.
Tafuta hela ww acha ubwege wa kuweka moyo wte kwa mwanamke
 
Mfuate alipo mpe huru ya kufunguka yote ya moyoni naamini mkiwa pamoja ni rahisi kumshawishi ni vizuri umfuate ili uonekane unajali
 
In my years of dating I've come to realize that women who like you will make it known to you via actions. Zero doubts.

If you find yourself thinking she's sending mixed signs, move on. Women who like you don't send mixed signs.
 
Wakuu mambo yalinishinda na mahusiano yalivunjika moja kwa moja na sasa yeye aliolewa na mtu mwingine na mimi nina mtu mwingine sasa japo nilitumia nguvu nyingi sana sana kutaka kuyarudisha mapenzi yangu kwa yule mrembo

Huu ni mrejesho wangu katika huu uzi

Asanteni sana kwa wote mlionitiaga moyo na kunishauri vyema
 
Umeshaoa mkuu au nae unasubiri subiri
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom