Msaada wa tatizo la laptop 'windows failed to connect to service' na mengineyo

chazy255

JF-Expert Member
Mar 31, 2016
1,363
1,752
Salamu ndugu.
Nina laptop kila nikifungua inaniambia window failed to connect to service, na kila nikiplay wimbo hauanzi kawaida sekunde za mwanzo kuna vitu kama mawingu hivi na sauti haitoki vizuri mpaka sekunde kama sita hivi ndo inaplay vizuri na mwisho kila nikizima laptop inachukua muda sana mpaka inakaribia dakika tano ndio inazimika. Wataalamu naombeni msaada.
 
Punguza hiyo AVG maana humo kuna windows Defender pia antivirus zaidi ya moja kwenye mashine lazima tu iwe nzito
 
Mkuu fanya mchakato uweke window 10 hii ndio ipo updated window 7na 8 sasa hiv zinasumbua kwasababu ni zazamani
Tusije sema win10 "yasumbua" just coz "Windows Next" imekua released...

Kulingana na matumizi; Windows 7 na XP zilikua very stable compared to Vista na 8.0!
 
Nipo moshi mkuu.
I hope ulipata usaidizi.

Ilivyosemwa , tatizo dogo hilo.

Kubadilisha Operating System should never be your first option for any issue coz itakua the same na kutuma SWAT team ilipue nyumba: kisa na maana, eti uliona mbu kwa ukuta
 
Win 7 & 8 hazina tatizo lolote bt matumizi mabovu hizo win zote zipo ok ishu kutatua ilo tatizo....solb badilisha win then activate hiyo win only that
 
Mkuu fanya mchakato uweke window 10 hii ndio ipo updated window 7na 8 sasa hiv zinasumbua kwasababu ni zazamani
Hizi windows inategemea na matumizi mfano mimi nina tools za zamani za kutengezea simu zina fanyakazi kwenye Win xp coz of driverrs etc lakini Windiow 7 ni Rafiki zaidi
 
kubadili windows sio solutions.
Tatizo linaitwa "Windows all users install agent service"
A. Bonyeza windows KEy + R andika "services.msc" kisha bonyeza enter.
B.
tafuta "Windows all user install agent service"
c. Windows all user install agent service kawaida ni manual.
d. Click Windows all user install agent service right click kisha start service.

tatizo halitajitokeza tena. u naweza weka automatic ili iwe inajistart automatic




 
Mkuu window 10 ni window mpya inamaana mapungufu yaliyokuwa katika window zilizopita Microsoft wameweza kuyaweka sawa katika hii window mpya vilevile wanampango wa kuziondoa sokoni window za zamani zisitumike ili wawe wanaifanyia tu update Hii window mpya sasa ili usipate usumbufu ni bora ukatumia hii window mpya kwasababu iko poa na haisumbui kabisa
1475070136182.png

Mkuu nipe darasa hiyo window 10 ikoje
 
Back
Top Bottom