makelejasitta
Member
- Jan 25, 2017
- 24
- 3
Niliuziwa kiwanja tukagonganishwa watu wawili huko simiyu,Mimi nikawa nimewahi kujenga nyumba pale baadae akaja mwenzangu na yeye anadai kauziwa,kumbe aliyemuuzia alishafanyaga ujanja mapema kabla Mimi sijauziwa akajifanya kapoteza ile ofa ya kiwanja,akaenda polisi akaandikiwa loss riport,kwa hiyo mwenzangu aliyeuziwa na copy ya ofa aliyoipata kupitia loss riport,issue ikaenda mahakama ya mwanzo akashinda na ikaamuliwa kwamba Mimi niliyejenga nirudishiwe gharama za nyumba,baadae aliyeniuzia akakata rufaa mahakama ya wilaya ilipofika kule kesi ikafutwa kwamba hukumu ile haikutendewa haki harafu haikupaswa isikilizwe mahakama ya mwanzo Bali ilipaswa kwenda mahakama ya ardhi,ikaelekezwa kwa yeyote mwenye lalamiko aende katika sehemu ihusikayo na mambo ya ardhi yaani kwenye mabaraza ya ardhi au mahakama ya ardhi.wakakaa kimpya,mpaka Leo
Sasa Mimi nipo DSM tangu mwezi 12.Leo nimeambiwa yule MTU kapeleka mchanga pale kwenye nyumba yangu.kisheria natakiwa nichukue hatua gani,naomba mnisaidie wanasheria tafadhari
Ili kufikia asubuhi kama wanaendelea kujenga Mimi nijue cha kufanya