X_INTELLIGENCE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 9,680
- 12,255
Wana JF mimi na familia yangu tunaitaji msaada wenu kisheria juu ya kesi inayo mkabili mama yetu.
Kuna mambo ya mila ambayo yalisababisha sisi tuwe mbali na bibi yetu mzaa mama, yaani tulimpenda kama bibi ila tulikuwa hatushirikiani nae kwalolote
Siku moja bibi alikuja nyumbani wakayasuluhisha tulimpokea tukaishi nae nyumbani, bibi yetu ana nyumba sita hapa mjini ila sisi kutokana na kutoelewana sana na bibi mama hakupenda kwenda kuishi kwenye nyumba za bibi
Kutokana na mapatano yetu na bibi hatimae tulianza kuishi na bibi nyumbani kwetu tulipo panga, bibi yetu ana watoto sita 6 ambapo mama yetu ndio wa kwanza.
Kutokana na hali ngumu ya maisha aliyotukuta nayo bibi pale nyumbani aliamua kumwambia mama kuwa yupo tayari kuuza nyumba zake 2 ili aweze kutusaidia, mama alikubaliana nae.
Mama akatafuta mnunuaji wa zile nyumba ambazo bibi alilizia kuziuza zile nyumba ziliuzwa milioni 50, bibi alienda mahakamani ili kukamilisha mauziano ambapo alikiri kukubari kuuza nyumba zake na mama yetu ndie mrithi wake ambapo yeye mama yetu alisimama kama shahidi.
Nyumba ziliuzwa kisha bibi akamwambia mama anunue kiwanja ajenge nyumba, mama alifanya kama alivyoagizwa huku bibi akimsisitiza kuwa hati zote za hii nyumba mpya aandike majina yake {mama aandike majina yake} ili wajomba zetu na mama zetu wadogo wasije kuhusika kwenye hiyo nyumba mpya.
Baada ya zile fedha kutumika kwenye ujenzi na matumizi mengine ya pale nyumbani, zilibakia kiasi kidogo kama milioni 8 ivi.
Siku moja bibi alimuita mama akamwambia nimekupa kila unachokita mwanangu naomba uwe mrithi wa huu mfuko wangu wa UCHAWI, mama alikataa kata kata hapo ndio ugomvi baina ya mama na bibi ulipo rudi upya.
Bibi aliondoka nyumbani akaenda kwa wanae wengine ambao hawakuhusishwa kwenye mauzo ya zile nyumba mbili, akawaambia kuwa mama yetu kamshawishi kuuza nyumba bila idhini yake.
Wakashirikiana wamefungua kesi ambayo inamuendesha sana mama angu.
Kwa yeyote atakaeguswa na hili tatizo tafadhali tunaomba msaada wa sheria kwani mama alilala mahabusu akafikishwa mahakamani tukamtolea zamana mahakama iliamua kuwa mama arudishe zile fedha milion 50 ambazo matumizi yote yalikuwa yanatoka kwa idhini ya bibi.