Msaada wa PC aina ya dell inasumbua charging system na kuboot

Mar 26, 2018
72
59
Habarini wana jamvi,

Kama nilivyoainisha kwenye kichwa cha thread hapo juu,

Nina PC yangu aina ya Dell ambayo batterry yake imeshakufa kitambo nikawa naitumia direct bila battery.

Kwa sasa PC hiyo inaniletea shida kwani kuna muda inawaka na kuingiza moto kama dakika 10 alafu inazingua haiwaki tena, then sahivi hata nikichomeka adapter hainyeshi ile taa ya kwamba imechomekwa ila niki/istart kutumia power button kuna muda inagoma kabisa alafu kuna muda inakubali kuboot na beep alarm nyingi zisizo na idadi then inaweza kuingiza moto kwa muda na ikate tena hadi nije niibahatishe tena hata kesho yake.

Je tatizo litakuwa nini? Je nifanye nini kuditect tatizo? Au kuna ashakutana na kesi kama hii anisaidie?
 
Back
Top Bottom