Msaada wa ndoto anazoota huyu jamaa na mpenzi wake

Da Vinci XV

JF-Expert Member
Dec 7, 2019
3,837
6,372
Nimekuwa na Jamaa ya ambaye tumeishi wote toka shule ya Msingi , mpaka sekondari. Kwanzia kidato cha tano ndipo mtengano ulipotokea baina yetu kwa kuwa tulipangwa shule tofauti , lakini uswahiba wetu upo hata asa.

Tuseme kiubinadamu , kila mtu anakuwa na Yule Rafiki yake ambaye Amejawa Utayari kwaye kwa kumweleza lolote limsibulo pasi na Shaka wala Soni, Rafiki ambaye Humjua vizuri yeye alivyo Zaidi ya nduguze, Rafiki Ambaye ,wahenga Walisema Mchuma janga hula na Nduguye basi hapa anaongelewa huyu jamaa Shida yake ingekuwa yangu, Yangu ingekuwa yake. Na hata maisha yetu kwanzia Chuo, Ni vivyo hivyo kuvutana popote mmoja anapokwama Iiitajikapo swala lolote linaoitwa msaada pasi na kuangalia ,sababu ni nini. Bugana,Maarifa au Nguvu. Vingetumika


Kipindi cha sekondari katika harakati za ukuaji tulilambiana Mpaka Jezi(Pisi) , Na wala hatukugombana kwa lolote.


Kingine cha zaidi sote tumekulia katika Mazingira ya Elimu na Kutokuamini maswala ya Ndoto,Nyota, Waganga na mengineyo ya namna hiyo kama jicho la tatu na kadhalika

(NB: Hapa labda niseme sio kuamini kama havipo la haasha baali twaamini kama vipo lakini kwetu hatuvitumiki, wala kukubali kama vina Msaada) Haswa Uislam wetu Elimu ya Ujana na Mambo ya Shirk.

Lakini baadae nlimwacha mwenzangu kwenye kundi hili baada ya mimi kubadilika kuwa mdadisi wa jinsi Dunia inavyokwenda huku nikiamini Dunia yetu ni Pande Mbili, Akajua naandika makala nyingi ,nyingine tata nyingine za kawaida , Akatamani pia kufanya kile nifanyacho mwenzie akashindwa , msaada wake ulikuwa ni kuniuliza maswali tu.


Turudi kwenye mada

Wote tulikuwa tunaamini ile maana halisi ya Ndoto ya kisayansi ya kawaida kwamba , ndoto ni kama Refresh ya Matukio yaliyotekea siku hiyo , au jambo ambalo limekutia mkazo sana, Basi Ubongo hulichakata ili kujua kama tunaendelea nalo au ni la kupuuzwa .kama takataka nyinginezo.

Lakini wiki iliyopita akaanza kunisimulia ya kuwa katafutwa na Mpenzi wake ambaye alidate naye wakati tuko sekondari (Tulikuwa naye darasa moja huyu binti) Lakini binti huyu Tulipoteza ukaribu nae toka kidato cha 3 , hapo ndiyo walikuwa wameachana pia kichochagizwa zaidi kuachana ni Mtengano wa Madarasa sisi tulikwenda michepuo ya Sayansi Binti akawa Michepuo ya Sanaa.

Mpaka wakati wa kutamatisha masomo yetu ya sekondari ndiyo kabisaa haswaa, na mimi ndiye nlisaahau kabisa kama dunia inammiliki binti huyu katika Ardhi yake , nimekuja kumtanabahi hiyo wiki iliyopita baada ya kuambiwa ya kwamba alimtafuta jamaa yangu.

Baada ya binti kumtafuta Jamaa yangu wakaanza convo za kawaida , na hapa nina Imani ikafika hatua ya Kuulizana lengo la kutafutana , ile ya why Umentafuta. Kama itokeavyo kwa watu maEX 🤣😂.

Binti akafunguka bayana kwamba aliota Ndoto, ambayo, inahusiana mambo ya zamani kipindi kile twasoma, akiota mapenzi yake pamoja na yule jamaa yangu , Akaamua kwenda kwao ,kwa sababu binti naye yupo huko huko (Mkoa ambao tulisoma sote sekondari) , akaomba namba kwa nduguze jamaa. akapata lakini baada ya Hilo jamaa yangu ndipo alipo nihadithia ya kwamba , kabla hata hajatafutwa naye alikuwa akiota matukio ya sekondari yanayohusisha mapenzi na Yule binti. Aliota hizo ndoto takribani wiki moja ndipo yule binti akaja mtafuta.naye akasimulia yale yale


Akashtuka mfanano wa ndoto hizi.

Jamaa baada ya kujua binti naye alikuwa akiota ndoto zile zile ndipo aliponihadithia mimi

Nami muda wote huwa namrudisha kwa mkombozi wetu ambaye ni Sayansi , Lakini wakati huu Mkombozi wetu huu alitufanyia ukatili Alishindwa kutujibu tutakacho....😂😂

Lakini kingine , bado anaota karibia kila siku lakini sasa hivi tofauti na mwanzo saivi anayaota matukio ya zamani zamani zaidi tofauti tofauti ,mda mwingine ya Shuleni muda mwingine Nyumbani. matukio haya yametokea wiki iliyopita na Ndoto hizo za sasa anaendelea kuota kila leo.(huyo jamaa yangu) Huyo binti hatuelewi kama anaendelea kuota au laah kwasababu hakushirikishwa katika lolote
Basi atakuja kulijua hili Labda nayeye aje asome hapa

Wasaalam na nina mani hapa nitapata chochote kitu.




🙏
 
Back
Top Bottom