msaada wa mawazo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

msaada wa mawazo

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by ossy, Aug 2, 2011.

 1. ossy

  ossy JF-Expert Member

  #1
  Aug 2, 2011
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 877
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Heshima yenu wakuu! wakuu naombeni msaada wa mawazo,nina mchumba wangu nipo naye kwa mwaka na nusu sasa,ni mwanafunzi wa chuo kikuu flani hapa tz,nilimtambulisha home but sijajitambulisha kwao but dada zake wote na ndugu zake wananifahamu kwa kukutana tu sehemu mbalimbali, tatizo mama yangu ameanza kuleta maneno ambayo siyaelewi akidai kwamba huyo msichana hanipendi na yuko na mimi ki maslahi zaidi,ameniambia nimchunguze sijaona tatizo lolote,sasa leo kaja na mpya kwamba ameoteshwa ndoto mbaya juu ya huyo msichana na amesema eti tufunge na kuomba week hii ili Mungu atupe jibu.
  inavyoonekana hampendi huyu msichana but mimi sioni tatizo lolote na nampenda,issue nyingine nna mtoto nilimpata nikiwa chuo so ameniuliza je nilishamwambia nikamwambia no! mda bado ukifika nitamwambia akawa mkali.Binafsi sioni tatizo la huyu msichana kwani anawapenda sana hata ndugu zangu na anainipenda pia.Sisi ni wachaga na huyo msichana ni mwarusha. Je niwakati mwafaka wa kyumwambia msichana juu ya mtoto wangu? je huyu mama anataka nini na nifanye nini? nawakilisha!
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  kwanza mwambie huyo msichana kuhusu mtoto


  halafu je mama yako aliwahi kuoteshwa nini huko nyuma ikawa kweli?????????
   
 3. ossy

  ossy JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2011
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 877
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  hakuna chochote alichowahi kuota kikawa kweli mkuu! ntamwambia mkuu!
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Aug 2, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  basi mama mpuuze

  halafu mwambie huyo msichana kuhusu mtoto kwanza
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Aug 2, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,189
  Trophy Points: 280
  kwa kifupi sana baada ya ujio wa Kristu hakuna mawasiliano moja kwa moja kwa Muumba.........................kwa hiyo haya ya kuoteshwa ni mawazo yake binafsui ambayo yamo kwenye fikra zake na ameyakumbuka wakati amelala............hili linanikumbusha utapeli wa babu wa loliondo ambaye naye adai ameoteshwa.........................wakati ni fikra zake za kujipatia utajiri wa haraka haraka.............na kwenye hilo kafanikiwa..........maana hata matapeli wetu serikalini nao wameonyeshwa kazi.....................

  angalia usije na wewe ukatekwa na ndoto hewa.............................................futata moyo wako na hata ukikosea utajua ya kuwa.................ulijitendea ubinadamu..................
   
 6. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #6
  Aug 2, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Mwambie kuhusu mtoto huyo msichana
  kaa na mama kwa ukaribu zaidi umuulize ni nini tatizo aliloliona kw ahuyo msichana mwombe kabisa awe wazi kwako aeleze hisia zake na akuambie wazi matatizo au mapungufu aliyoyaona na wewe utajudge kwa hizo taarifa kama zina lolote la kukusaidia. Afterall wewe ndie unayependa na ndie utakayekuja kuoa mama na ndugu zako ni wapitaji tuu kwenye familia yako mpya. So kama ni mambo ya ndani ni yako wewe na mke wako
   
 7. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #7
  Aug 2, 2011
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Usigombane na mama.........
  Funga hii wiki kama anavyotaka mama, na uombe kiukwelikweli, na usifanye hili sababu ya mama bali yako mwenyewe. ukishamaliza mfungo na maombi yenu, kama bado unajisikia kuendelea kumpenda kama ilivyo sasa, ongea naye kuhusu mtoto. Ingawa hili ulitakiwa kumwambia kabla hujampeleka kwenu ili afanye maamuzi yake.
  Kuhusu kupenda ndugu zako, hicho siyo kigezo cha kufanya umuoe, swala muhimu ni kama anakupenda wewe. kumbuka kuwa, mabinti wengi wanawapenda sana ndugu za waume kabla hawajaolewa, na mambo yanaweza kubadilika wakiingia ndani.
  huyo mama wala asikuumize kichwa, baada ya mfungo na yote hayo, ongea naye taratibu, usijaribu kugombana naye maana ndo atazidi kumchukia huyo binti na haitakuwa nzuri kwa ndoa yako. Jitahidi sana unapoongea na mama usimsifie saaana huyo mdada maana mama anaweza akapata wivu utakaosababisha mambo yakawa magumu zaidi.
   
 8. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #8
  Aug 2, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Wewe ndio muoaji, ! na mwisho wa siku wewe ndio mtoaji maamuzi, sisi na ndugu zako ni mashahidi tu wa hadi utayoweka mbele ya Mungu! Mpira wako huu cheza kwa makini!
   
 9. Yasmin

  Yasmin JF-Expert Member

  #9
  Aug 2, 2011
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  first of all u need to tell her the truth,and then if she accept it,and still love's u.then no matter what fight 4 your true love
   
 10. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #10
  Aug 2, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  1. Fungeni kama anavyoshauri mama kwani kufunga ni jambo jema na sadaka kubwa sana na ninaamini maombi yanayoendana na kufunga huwa na nguvu kubwa.
  2. Kaa na mama yako baada ya kufunga umwombe awe wazi kwako na kama sababu atakazozitoa sio za msingi... oa. Rafiki yangu aliwahi kuandamwa sana akapuuza baada ya kupeana ujauzito ndipo mama akbreak the news kumbe walikuwa mtu na dada yake......
  3. Kama utaafiki kuendelea na huyo msichana baada ya kikao na mama yako then muambie kuhusu mtoto na umuombe msamaha kwa kumficha jambo la msingi kama hilo hadi hatua hii though kama kazoeana na ndg zako na binadamu wanavyopenda kuchonga siku hizi (hata kwa yasiyowahusu) ni wazi alishatonywa na anataka tu klusikia kutoka kwako!!
   
 11. Tulizo

  Tulizo JF-Expert Member

  #11
  Aug 2, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 849
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Ossy, Jina na hii issue uliyotupa vinapingana kidogo..Yaani kwenye issue ni mwanaume,,na unatumia Ossy..Anyway, siyo big deal..

  Sasa, ndugu yangu kumbuka Kuoa au kuolewa siyo lele mama na pia hakujaribiwi. Ukikosea mara ya kwanza..utaendelea kukosea mara zote.

  Ndoa ni kifungo cha nadhiri cha muda mrefu labda kama unataka kumaliza tamaa za kimwili na sio kuwa na familia. Hivyo maamuzi ya mwisho unayo mikononi mwako na wala sio kwa ndugu zako.

  Lakini kumbuka, ingawa mama na ndugu hawana maamuzi katika familia yako ya baadaye lakini wao kama wadau wa karibu wa familia yako wana sehemu yao inabidi kutumia busara sana kuweka mambo sawa pale ambapo hawakubaliani nawe kwani wanaweza kukuletea ugumu wa maisha na kukutia kishawishini kama hutaweza kuwaweka sawa kwa sasa kwa kutumia busara zako. Kikubwa maisha yako hayana demokrasia kama chama cha siasa.

  Mama ana sehemu muhimu kwa maisha yako na inabidi kumuheshimu. Lakini kumbuka heshima isiwe ya uwoga kiasi cha kuogopa kumweleza ukweli vile vitu ambavyo kwa utashi wako hukubalini navyo, lugha ni muhimu kuwasilisha hayo kwa mama kwani mtoto hakuwi kwa mama.

  Ndoto zimepitwa na wakati kama unamwamini Mungu wa kweli kwa dini yeyote. Kufunga na kusali ni jambo jema endelea nalo lakini ni kwa kumwomba Mungu akusaidie kufanya maamuzi magumu na siyo kufuata ndoto ya mama.

  Kuhusu Mtoto mwambie mpenzi wako haraka sana hata leo. Sio hilo tu.. huu ni wakati wa kumwambia yote mazuri na mabaya yako. Bila woga tumia wakati huu kumwomba naye akupe yale anayofikiri ni mabaya kwake. Mwisho, Ni juu yenu wawili kuamua katika jinsi gani ya ku- balance equation ya mahusiano yenu.
   
 12. A

  Aine JF-Expert Member

  #12
  Aug 2, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Fungeni, kama ndoto ya mama ni ya ukweli mtapata jibu, kama si ya kweli pia mtapata jibu. Wazo la kufunga na kuomba ndio la msingi hapo usije kuoa mke wa mwenzako afadhali umuombe Mungu upate jibu mapema. Pia kuhusu mtoto mwambie mapema usianze mchakato wowote kabla hujamuambia kuhusu mtoto, usijifariji anakupenda na anawapenda ndugu zako ni mapema mno kusema hilo hasa la ndg bora wewe mwenyewe, ukimuambia ukweli ndio utagundua anakupenda au la, mwambie as soon as you can
   
 13. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #13
  Aug 2, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,982
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  Mchunguze nawe umwambie ukweli wote.
   
 14. ossy

  ossy JF-Expert Member

  #14
  Aug 2, 2011
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 877
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Asante kwa ushauri mkuu! namsubiri aje week end nimwambie kuhusu mtoto,kwani yupo chuo mkuu!!
   
 15. BlackBerry

  BlackBerry JF-Expert Member

  #15
  Aug 2, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 1,844
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Muulize vizuri mama yako anaweza kuwa nni dada yako,maana maisha tunayoishhi haya yamejaa mambo ya ajabu na siri nyingi sana
  <br />
  <br />
   
 16. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #16
  Aug 2, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  hapa umeongea mkuu!
   
 17. ossy

  ossy JF-Expert Member

  #17
  Aug 2, 2011
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 877
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  sio ndugu yangu mkuu! Its just mama ana wasawasi kuwa hana true love!!!!!!
   
 18. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #18
  Aug 2, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,314
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Dah! Huyo mama yako mwongo, anataka kukudanganya umwache mpenzi wako bila sababu, ila kuthibitisha upendo wa gf wako mweleze kuhusu mtoto, akikubali kumpokea kwa mikono miwili basi atakuwa mpenzi wa ukweli.
   
 19. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #19
  Aug 2, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Wamama wanajua sana kuwasoma mabinti wa kike, tukumbuke pia na wao walipitia stage hizo mnazopitia.
  Its better ukaresolve hiyo ishu mapema ili usije ukaingia kwqenye mkwaruzano na mama yako!
  Though huyo mwanamke ni wewe utaish naye na siyo yeye, kumbuka mama ni mama tu!
   
 20. Z

  Zero One Two JF-Expert Member

  #20
  Aug 2, 2011
  Joined: Sep 16, 2007
  Messages: 9,390
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Boss kumbuka ameota ma ra nyingi na kama kuna ambavyo vilitokea kuna ambavyo havija tokea. Aliota vibaya kuhusu huyo dada sababu tayari amesha fanya fixation about her. Ukweli ni kwamba mtu hawezi kumchukia mtu bila sababu. Kaa na mama yako umuulize tatizo ni nini na ni kitu gani aliona kufika kwenye hiyo conclusion (kwamba yuko na wewe kimaslahi zaidi). Based on that ndio umchunguze mpenzi wako.
  But kabla hujaanza mwambie kwanza mpenzi wako kuhusu mtoto. Mtoto ni baraka, sio aibu.
   
Loading...