Habari wakuu.
Nimekuwa kwenye mahusiano na huyu binti kwa zaidi ya mwaka mmoja na malengo yetu ni kufunga ndoa halali ya kanisani next year.
Changamoto kubwa niliyonayo ni usiri wa huyu binti kwenye simu yake. Kwa mwaka mzima nimefanikiwa kushika simu yake mara moja na nilikuta sms ya mapenzi ila akasema ni X wake anajaribu kuomba warudiane.
Of course tuliongea na tukayamaliza. Baada ya hapo sikushika tena simu yake kwa zaidi ya miezi sita. Kuna siku nilijaribu tena kuishika lakini ilikataa katakata na tuligombana na kukata mawasiliano mpaka dada akaja akatupatanisha na huyu binti akasave password yake kwenye simu yangu.
Imepita kama miezi mitatu sikuangaika na simu yake. Jana nilijaribu kuichukua na kuifungua lakini nikakuta kabadilisha password. Nilimuomba anifungulie akagoma tena.
Nilimuacha kwa muda nikijua kuwa kama kuna mambo yake atayafuta lakini baada ya masaa kama mawili nikamuomba tena anifungulie akakubali kwa masharti nimwambie nachotaka kukiona anionyeshe nikamwambia hapana. Nahitaji kuangalia mwenyewe akanijibu straight kuwa hataki.
Kumbuka kabla ya kumuomba simu niliongea nae sana na nikamjulisha juu ya lengo letu so kama anahisi muda wake wa kuingia kwenye ndoa haujafika anijuze tu ili asinipotezee muda maana mimi lengo langu ni kuwa na familia.
Wakuu nishaurini. Huyu binti niko nae safari moja au napoteza tu muda wangu? Kumbuka kuwa yeye yupo free sana na simu yangu na wala haina password.
Niseme tu ukweli kuwa sijawahi kumuhisi kuwa na mahusiano mengine na upande wa maisha ni mtu ambae anajielewa na alinishauri viti vingi sana wakati nafanya ujenzi.
Nashindwa tu kuelewa kwenye simu yake ni kitu gani hicho muhimu kwake ambacho hataki mimi nikijue na yupo radhi nimuache lakini sio kuniruhusu nishike simu yake.
Hapa nilipo bado nina ugomvi nae tangu jana na nawaza nifanye maamuzi gani.
Asanteni kwa ushauri wenu