Msaada wa mawazo kwenye haya mahusiano yangu

Diaryjr

Senior Member
Jun 15, 2015
190
129
Habari wakuu.

Nimekuwa kwenye mahusiano na huyu binti kwa zaidi ya mwaka mmoja na malengo yetu ni kufunga ndoa halali ya kanisani next year.

Changamoto kubwa niliyonayo ni usiri wa huyu binti kwenye simu yake. Kwa mwaka mzima nimefanikiwa kushika simu yake mara moja na nilikuta sms ya mapenzi ila akasema ni X wake anajaribu kuomba warudiane.

Of course tuliongea na tukayamaliza. Baada ya hapo sikushika tena simu yake kwa zaidi ya miezi sita. Kuna siku nilijaribu tena kuishika lakini ilikataa katakata na tuligombana na kukata mawasiliano mpaka dada akaja akatupatanisha na huyu binti akasave password yake kwenye simu yangu.

Imepita kama miezi mitatu sikuangaika na simu yake. Jana nilijaribu kuichukua na kuifungua lakini nikakuta kabadilisha password. Nilimuomba anifungulie akagoma tena.

Nilimuacha kwa muda nikijua kuwa kama kuna mambo yake atayafuta lakini baada ya masaa kama mawili nikamuomba tena anifungulie akakubali kwa masharti nimwambie nachotaka kukiona anionyeshe nikamwambia hapana. Nahitaji kuangalia mwenyewe akanijibu straight kuwa hataki.

Kumbuka kabla ya kumuomba simu niliongea nae sana na nikamjulisha juu ya lengo letu so kama anahisi muda wake wa kuingia kwenye ndoa haujafika anijuze tu ili asinipotezee muda maana mimi lengo langu ni kuwa na familia.

Wakuu nishaurini. Huyu binti niko nae safari moja au napoteza tu muda wangu? Kumbuka kuwa yeye yupo free sana na simu yangu na wala haina password.

Niseme tu ukweli kuwa sijawahi kumuhisi kuwa na mahusiano mengine na upande wa maisha ni mtu ambae anajielewa na alinishauri viti vingi sana wakati nafanya ujenzi.

Nashindwa tu kuelewa kwenye simu yake ni kitu gani hicho muhimu kwake ambacho hataki mimi nikijue na yupo radhi nimuache lakini sio kuniruhusu nishike simu yake.

Hapa nilipo bado nina ugomvi nae tangu jana na nawaza nifanye maamuzi gani.

Asanteni kwa ushauri wenu
 
Kwann na ww ushike simu yake kama haujawahi muhisi anamakoloni ya kando?!
Sina kawaida kabisa ya kuishika na kwa zaidi ya mwaka mmoja nimeishika mara moja na pia kuomba kuishika mara mbili na wakati wote huo nakuwa tu nimejisikia kumjaribu tu nione kama atanipa.
Note that huyu ni mtu ambae naenda kuingia nae mkataba wa maisha so mara moja moja kutaka kujua vitu vyake ni muhimu kidogo
 
Samahani kwa kuusoma mstari mmoja wa juu kisha nikaanza kuandika hili....

Natanguliza pole sana kwako....

Naomba niseme hivi kuliko kupoteza muda wako kuanza kufikiria,kutaka au kufukunyua simu ya mwenzako wa karibu hasa msichana au mwanamke huko ni kuitesha akili yako.....

ACHA ACHA ACHA

tena acha kabisa, mwanamke au msichana ni mtu asiyetabirika ndio maana hakuna mwanadamu anayejua nyoka na wao walizingumza na walikubaliana nini pale bustanini zaidi ya sisi vidume kupokea tunda na kula

Niliwahi kufanya unachokifanya lakini niliwahi kuambiwa nimuache awe huru, hilo neno nilikuja kulielewa baada ya miezi 4 kupita, kaka fanya kazi,tafuta hela achana na biashara kichaa hiyo ya kufukunyua simu utakachokikuta kitakuumiza ni bora kikuumize wakati hujakiona kuliko utakapo kiona

Ni ushauri tu
 
Kama yu radhi kuachwa kuliko ushike simu yake bro achana naye kabla hujagundua mabaya mkiwa ndani ya ndoa kwan utaumia mara mia ya sasa

Halafu unaweza ukanipekua ukanikuta sina makando kando ukajua nakupenda peke yako kumbe nina kitochi changu cha mambo yangu mwenyewe we hujui haya mambo hayahitaji papara
 
wewe simu yake unataka ufanyie nini??? ulimnunulia wewe?? hata kama ulimnunulia si umempa??? kwa ushauri tu fanya hicho ni kiburudisho tuu......sio wako huyo......ila UKIMWI upo.....tena karibu yako....
 
Hivi kweli mme au mke mtarajiwa anaweza nyimwa simu!!!

Eti unamfuatilia sasa wewe usipomfuatilia atafuatiliwa na nani!!?

Kama kweli nia yenu ni moja na lengo moja la familia mbeleni, huyo hana sifa ya kuwa nawe bro.
 
Mwenzako ka download zake PORN zake wewe unataka kuja ziangalia.

mi ushauri wangu mridhishe kimapenzi mwenzako aache kupiga punyeto na hapo utaishika simu yake muda wowte

Ukitaka kuamini anaangali porn siku jifanye unashida na net then muombe simu akikuuliza unachotaka fanya mwambie unaingia google akikupa angalia history au bookmark ila usisikitike
 
Kama hujawahi mtoa bikra, wewe kwa sasa uko sawa na yule aliyemtoa bikra akamwacha, hivo utakua na uhalali wa kushika simu yake pale utakapokua umetoa mahari na kumuoa jumla.
Kwa sasa ame bet wanaume anaowataka, incase utamtema awe na sehemu ya kujishikisha, hata kama ushamuhakikishia utamuoa.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom