msaada wa mawazo jamani

joda

Member
Joined
Apr 7, 2012
Posts
45
Reaction score
12
nimeolewa kwa miaka 7 sasa,Mungu ametujalia watoto 2 kwenye ndoa yetu.ndoa yetu kwa nje inaonekana ni yenye afya njema sana, lakini kiukweli ndani kuna moto unawaka.na tatizo kubwa ni mwenzangu ambaye amekuwa akirudia kuniambia kila wakati kuwa hanipendi na haelewi ilikuwaje tukafunga ndoa.anasema kwamba yeye hakuwa mtu wa kuoa alitakiwa aishi peke yake tu.na siyo kwamba anaongea tu mdomoni hata kwa matendo unaona ni mtu anayemaanisha kwasababu vitendo vinadhihirisha hanipendi.he usually crash me, ananigombeza, hanisikili kwa chochote, anamtetea even mdada wa kusaidia kazi mahali ambapo hakustahili kufanya hivyo mbele yake, siku nyingine tuko na marafiki zetu akaanza kusema weakness zangu mbele ya marafiki. ananishushua vibaya hata mbele za watu.akiamua kuninunia hata mwezi ananuna kama nisipoenda kumbembeleza,sikumbuki ni lini aliniita hata dear au kuniambia neno la kunitia moyo au hata kunikumbatia,tunafanya kazi wote yeye mshahara wake anauita ni wake hela zake zangu anataka ndiyo zitumike kwa sana na yeye anatoa kidogo katika nyingi alizonazo, na sijui zinaenda wapi hizo hela.hawasiliani na mimi hata kidogo tukiwa mbalimbali, nisipompigia mimi ndiyo imetoka.na wakati mwingine nikimpigia ananigombeza bila sababu,au anaongea halafu anakukatia hataki usumbufu.

nilipokuwa mjamzito kwa mimba zangu zote mbili ndiyo nilikomaga, yaani ndiyo anakua ananichukia zaidi.ananisema maneno mabaya mabaya ninalia miezi tisa yoteee, hadi wakati mwingine naamua kwenda kulala mbali na home, naweza nikaondoka hata saa nne usiku wala asishtuke, na nikirudi wala hajisumbui kuuliza.nikiwa nipo hospitali kwaajili ya labour wala hashtuki kuonyesha mwenzangu anaumia sasa hivi, hadi ndugu zangu walinote hiyo action yake wakaja kuniuliza nikawakatalia.yeye mwenye mke ambaye amejifungua usiku wa manane kwamba ameondoka ameniacha ninalia uchungu kesho yake anakuja hosp saa 4 asubuhi, ndugu zangu wazazi walishafika mapema saa kumi na mbili juu ya alama.yaani inakuaga ni aibu kwangu.

many times nimefikiria sijui tuachane then nawaza mara mbili mbili mbona kina mama zetu wako na baba zetu mpaka uzeeeni waliwezaje?, then nasema sijui twende kwa wadhamini naona kama kujidhalilisha, nabaki naumia tuu sijui cha kufanya.navumilia hata sasa.sijui nifanyaje nisaidieni,ungekuwa wewe ungefanyaje?ananidharau mpaka basi and in short anadharau wanawake sana. and usije ukadhani he is cheating with another woman hapana,hana mwanamke yeyote nje ya ndoa,nimechunguza mpaka basi hakuna na yeye ananiambia hautakaa uje usikie wala uhisi that nina affair na msichana yeyote.he is damn faithful au anajua kuficha track zake sana kitu nachojua hakifanyi.afta work he comes back home,hatoki atasoma vitabu atalala,ndiyo routine yake.he stays home.but he is bad very bad, ana bitter words to the maximum.what will u do?
 
Sasa si alishakujibu alikuoa by mistakes?
ulitaka jibu lipi tena?
 
pole sana dada ila mm nahisi labda huyo mwanamme amewahi kutendwa na mwanamke aliyempenda hapo awali sasa kawa kama simba aliyejeruhiwa kwmamba kila binadamu anayemwona anajua ni adui yake cha kufanya jitahidi kumzoea ipo siku atasahu yote na atakuwa mme mwema:rockon:
 
yap huwa inatokea na ni matatizo ya kisaikolojia hasa.nitaku pm 4 more assistance.
 
Inawezekana alishatendwa au ulimkosea bila kujua ongea nae kama kuna kosa lolote umuombe msamaha, kama haukuwai kumkosea rudi nyuma kwenye uchumba wenu wewe ndio unajua kaanza kubadilika lini ujue tatizo nini. mchukulie kawaida umjali usionyeshe kinyongo akikukrash omba msamaha hata kama huna kosa ye mwenyewe atajirudi tu coz ataona anamuukumu mtu asiyepaswa kuukumiwa.
 
::
Itafika mahali JF tuweke utaratibu za kusikiliza pande mbili maana Ushauri wa upande mmoja unaweza kuwa unfair
=
 

ndugu nimejaribu kuongea naye nadhani ten thousands times, na mara zote huwa anaavoid kuongea na hata akikubali ananisikiliza tu. yaani this is my cross naona.nimeshaomba msamaha mbinu zote nimeshatumia na zimegonga mwamba.the only solution ni separation ila ninaogopa sana aibu, kwamba ndoa imenishinda. and how am i going to face maisha alone?then nafikiria my kids nabaki ninalia tu peke yangu
 
je, wewe unampenda kutoka moyoni????[/QUOT

nilikuwa ninampenda sana, ila kwa sasa naona upendo haupo and its only bcoz ya anayonitendea, yameua upendo wote.tunaenda kwa mazoea tu.
 
Mimba ya kwanza iliingia by mistake. Mimba ya pili uliipataje?
 
sijaongea kama nilipata mimba kwa mistake, zote zilikuja kwa wakati wake.
 
wakati matatizo makubwa yaingiapo ndani ama yanapotokea daima suluhu huwa kati ya haya mambo 3.
a) reconcile hapa unaongea nae kinaga ubaga hadi mfikie suluhu, ngazzi hii usimshirikishe mtu bali nyie wawili tu ili mfikie mwish muutakao.

b)separation hapa ina maana u give each other space, ili kila mtu akae ammiss mwenzie and upweke, utarevive upya pendo lenu ama la wazazi wa pande zote mbili watawaweka chini msuluhishwe.

c) divorce hili ni jambo ambalo huwa silipendi kabisa kwani ni la mwishi kabisa kutokea, but when need arises you go for it. huitaj ushauri wa mtu katika hili ukishaamua ku divorce huna haja ya kutaka suluhu ama ushari kwa watu.panga your future and then decide your destiny.
 
Sijaona hata sehemu moja mdau akieleza weakness zake na yeye.
It seems she is perfect!! Mwanaume tuu ndo ana matatizo?? Mh!
 
Ninachoweza kukushauri kama wewe unamuamini Mungu omba kwa ajili ya mumeo..Tena funga na kuomba..Tena kama kuna mtu mchaji unamuamini au mchungaji whoever mshirikishe muombe pamoja..
Maana huyo mumeo sion ni nani atamshauri kwa hali aliyonayo ageuke kama Mungu hataingilia kati
 
Kama hana demu nje basi mwanasaicology anahusika may be havutiwi na mahusiano ya jinsi ya kike.pili je utavumilia mpaka lini??chukua hatua mapema kwa hiyo ww unatunza familia yy ni kama anasaidia tu loooh.sasa kumbe unaweza kwanini unaogopa kuface challenge ambayo unaweza kuikabili??jitu umekutana nalo ukubwani kwanini likusumbue
 
Mmmh..! Wanaume wengine wanatia karaha jamani..!

Mie kumganda mwanaume wa namna hiyo SIWEZI..!
 


my dear pole sana, kuna dada yangu alipata mume kama wako, na labda yeye alikuwa zaidi kwa sababu alikuwa anachelewa kurudi nyumbani....hebu fanya kama alivyofanya huyo ndugu yangu labda itakusaidia, yeye alifanikiwa na mume wake alichange mpaka leo wana zaidi ya miaka 15 kwenye ndoa.....
ni hivi, huyo dadangu alipoona amechoka kuvumilia aliamua kurudi nyumbani, na mama alimwambia afanye yafuatayo

1. mama alimwambia dada asimsemeshe sana mumewe na wala asimlalamikie kabisa kuhusu tabia yake. yaani amuache afanye anavyotaka na asimuulize hata kama amekasirika anyamaze tu. ni kama mama alimwambia dada funga mdomo wako kabisa..yaani abadilike na kuwa mkimya sana na mpole, asimuulize wala asigombane naye......

2. mama alimwambia dada pamoja na kufunga mdomo wake anatakiwa aongeze mapenzi kwa mumewe..yaani ajitume kumhudumia mwenyewe na asimuachie house girl kila kitu hasa anaporudi kazni..mama alimwambia dada kama mumewe anaangalia movies tu basi amuache na kama anasoma vitabu/magazeti amuongezee, yaani amnunulie mwenyewe.
3. Mumewe akimgombeza asimjibu chochote anyamaze kimya, ikibidi alie tu lkn anyamaze hata kama anamuonea....mama alimwambia dada kuwa hii itamfanya yule mwanaume ajikague maneno yake na ajue makosa yake mwenyewe, yaani asiambiwe na mtu..
pia mama alimwambia dada aongeze kumnunuliwa vizawadi vidogovidogo japo kila mwisho wa mwezi anapopata mshahara, na asilalamike sana kama mumewe hatoi matumizi yote..
4. mama alimwambia dada kuwa asiache kumpa chakula cha usiku mumewe pamoja na matatizo yoote hayo..
5.mama akamwambia dada afanye hivo kwa miaka 2, na akiona mume habadiliki basi arudi nyumbani na hapo atampokea kwa mikono miwili...alimwambia avumilie na asiache wala asichoke kufanya mama alivyomwambia

DADA akamwambia mama mimi ntaweza hayo? mama akamwambia utaweza mwanangu kama mimi mama yako nilivyoweza...mmmmmmmmmmmmmmhhhhhhhhhhhhhhh mi mwenyewe nilikuwa sijaolewa lkn nilichoka kabisa.....

basi dada alirudi kwa mumewe na akafanya km alivyoambiwa na mama japo wakati mwingine alikuwa anakuja nyumbani na kuliaaaaa mama anambembeleza na kumwambia avumilie...

wala haikuchukua muda mumewe akaanza kuwahi kurudi nyumbani.......hilo lilikuwa fanikio la kwanza na dada alivyoona hivyo akaongeza bidii kufanya hayo hapo juu km mama alivyomwambia....ipo siku mumewe alimfokea mbele yangu, nilimuonea dada huruma nikatamani......dada aliingia chumbani akalia wee lkn hakumjibu
ajabu jioni yake akamuomba msamaha kwa upole mbele yangu labda aliona aibu, dada akamwambia nishakusamehe...shemeji akamkumbatia mbele yangu nikaona aibu nikaingia chumbani...
tangu hapo dada anasema mumewe amebadilika kabisa amekuwa baba na mume mwema na wanaishi kwa amani sana huezi amini....
ila yataka moyo wa uvumilivu sana ndio utafanikiwa vinginevyo itakuwa ngumu.....huyu mume wa dada alikuja kumwambia mkewe kuwa background yake ilimfanya akawa vile mtu mwenye hasira hasira tu, lkn anasema ule wema na ukarimu aliomuonyesha dada ulimfanya akajiona yeye ni mtu mwenye thamani na akaona kwa nini namfanyia ubaya mtu ambaye ananifanyia wema wote huu?...
kwa hivyo mleta mada hebu jaribu mbinu hizo hapo juu labda na wewe zitakusaidia.....inaonyesha unaweza kuvumilia hebu jaribu mwaya usikate tamaa na wala usimuache mumeo...huwenda ana matatizo wewe ndio wa kumsaidia

neno moja tu.....kuwa mkimya, hebu nyamaza tu na uendelee na maisha na ufanye hayo mengine hapo juu uone, naamini atabadilika tu...shemeji yangu alikuwa mkatili over lkn sasa ni mume mzuri over.....
akishabadilika na wewe usiache hayo mana atarudi kuwa vile vile....usia wa mama kwa dadangu..
 
Pole sana bidada,

Umeongea mengi upande wa mwenzio bila kukoment upande wako,

ila unatakiwa ujue kuna watu wako hivo, hawapendi bughudha za watu wengine (kuwa arround kila saa nayo ni bughudha) kama hakuna cheating hakuna sababu ya kuachana wala ya kutafuta kidumu, ila ningekushauri ukae naye mbali kwa muda na umzoee hivo alivo!

Chukuwa likizo nenda kijijini kwenu ukatembee, ukirudi keep your distance wewe na wanao tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…