Msaada wa makazi Dar es Salaam

Msaada wa makazi Dar es Salaam

Pap Joh

Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
69
Reaction score
48
Habarini ndugu zangu wanaJf,

Naomba niende moja kwa moja kwenye mada, kama ifuatavyo:

Mimi ni kijana wa kiume, kwa sasa nipo Dodoma na umri wangu ni 27.

Nimefikia hatua ya kuamua kutoka huku nilipo na kwenda Dar, kwa ajili ya utafutaji wa maisha. Kwa kifupi nimejipanga vizuri, kuhakikisha napiga hatua fulani za kimaendeleo, kwenye yale ninayotegemea kwenda kuyafanya. Hivyo namuomba Mwenyezi Mungu tu anifanyie wepesi...

Sasa shida kubwa ninayoiona mbele yangu, ni kukosa ndugu/jamaa ambaye angeweza kunipatia msaada huo wa makazi. Hivyo nimetafakari sana, kisha nikaona hakuna ubaya kama nikija kwenu wanandugu wa JF kuomba msaada huo wa makazi.

Naomba kupata msaada wa makazi, kwa muda usiozidi miezi miwili tu. Na katika kipindi hiko chote, itakuwa ni msaada wa kupata sehemu ya kujihifadhi tu, kuhusu mambo ya kula na mengineyo NITAJITEGEMEA. Ila pia Mungu akinijali kufikia malengo yangu mapema, basi nitakuwa nami natoa mchango wangu wa kulipia baadhi ya bill mfano maji, umeme n.k

Kuhusu tabia:
Binafsi sina utamaduni wa kutumia kilevi cha aina yoyote ile. Ila pia sina kabisa tabia ya tamaa....

Hivyo naweza kuhitimisha kwa kusema, naweza kuishi na watu vizuri.

Tafadhalini sana wadau wa Jf, naombeni msaada wenu wapendwa....hali yangu sio nzuri kabisa.
Asante.
 
mtafute jamaa mwenzio njoo nae mchange kodi vyumba vya elfu 30_40 dm vipo kibaoo, nunueni godoro chapa GSM wekeni chini anzeni mchaka mchka wa dsm,usifikir uje miezi miwil gari limechanganya labda uwe unajua unakuja kufanya kipi
 
Asante sana kiongozi.
Sasa unatuomba sisi wana JF Tukusaidie au unamuomba Mungu?
Wewe kama ni sehemu ya kulala njoo mpaka ubungo stendi ukifika nitafute, kuna chumba kipo Msewe, Ila hakina godoro wala umeme.
Ni chumba tu kama chumba.
 
Shukrani mkuu kwa ushauri wako, nimeupokea!
mtafute jamaa mwenzio njoo nae mchange kodi vyumba vya elfu 30_40 dm vipo kibaoo, nunueni godoro chapa GSM wekeni chini anzeni mchaka mchka wa dsm,usifikir uje miezi miwil gari limechanganya labda uwe unajua unakuja kufanya kipi
 
Sasa unatuomba sisi wana JF Tukusaidie au unamuomba Mungu?
Wewe kama ni sehemu ya kulala njoo mpaka ubungo stendi ukifika nitafute, kuna chumba kipo Msewe, Ila hakina godoro wala umeme.
Ni chumba tu kama chumba.
Mkuu msaidie huyu, mwamba atakuwa ndugu yako hakika nakwambia
 
Habarini ndugu zangu wanaJf,

Naomba niende moja kwa moja kwenye mada, kama ifuatavyo:

Mimi ni kijana wa kiume, kwa sasa nipo Dodoma na umri wangu ni 27.

Nimefikia hatua ya kuamua kutoka huku nilipo na kwenda Dar, kwa ajili ya utafutaji wa maisha. Kwa kifupi nimejipanga vizuri, kuhakikisha napiga hatua fulani za kimaendeleo, kwenye yale ninayotegemea kwenda kuyafanya. Hivyo namuomba Mwenyezi Mungu tu anifanyie wepesi...

Sasa shida kubwa ninayoiona mbele yangu, ni kukosa ndugu/jamaa ambaye angeweza kunipatia msaada huo wa makazi. Hivyo nimetafakari sana, kisha nikaona hakuna ubaya kama nikija kwenu wanandugu wa JF kuomba msaada huo wa makazi.

Naomba kupata msaada wa makazi, kwa muda usiozidi miezi miwili tu. Na katika kipindi hiko chote, itakuwa ni msaada wa kupata sehemu ya kujihifadhi tu, kuhusu mambo ya kula na mengineyo NITAJITEGEMEA. Ila pia Mungu akinijali kufikia malengo yangu mapema, basi nitakuwa nami natoa mchango wangu wa kulipia baadhi ya bill mfano maji, umeme n.k

Kuhusu tabia:
Binafsi sina utamaduni wa kutumia kilevi cha aina yoyote ile. Ila pia sina kabisa tabia ya tamaa....

Hivyo naweza kuhitimisha kwa kusema, naweza kuishi na watu vizuri.

Tafadhalini sana wadau wa Jf, naombeni msaada wenu wapendwa....hali yangu sio nzuri kabisa.
Asante.
Utaolewa ooh
 
Si nimesikia dodoma Kuna fursa nyingi na wa dar wanahama wanakuja huko!..nawewe waja huku..

Nikutakie kila la kheri.
 
tatizo wagogo mnapenda kusaidiwa sana..mtafute Ndungai akusaidie
 
Hivi si nasikia ilala kuna boarding houses za kulipa 500 per day?,zile wauza gahawa hulala?
 
Mdogo wangu licha ya kwamba unayatamani maendeleo ila inaonekana haujajipanga vizuri katika mipango yako.
1. Unaachaje kupanga mahali pa kufikia katika mipango yako? Je hujui kuwa kuna chamgamoto nyingi za kufikia nyumbani kwa mtu?
Kama kweli unaamini mipango yako itakaa sawa baada ya miezi miwili kwa nini usifikirie kuwa na mpango wa kupanga walau ‘’guest house’’ za gharama nafuu?

2. Katika bandiko lako hujaeleza chochote kuhusu eneo ambalo ungependa kuishi maana Dar es Salaam ni kubwa sana, kama unajua unachokuja kukifanya Dar basi walau ungefanya uchunguzi kidogo wa kujua wapi ufikie ili hicho unachokuja kukifanya kifanyike kwa urahisi zaidi. Maana hata Mbagala Kisewe, Kitunda, Buza, Kawe, Boko na Pemba Mnazi kule Kigamboni pote bado ni Dar es Salaam.

3. Jaribu kutafuta hata mtu unayefahamiana naye hapa Dar ili akutafutie hata vyumba vya bei nafuu kwa sasa ili ufanye mambo yako kwa uhuru.
Usalama wako na mali zako pia, kuishi kwa mtu kuna changamoto nyingi. Unaweza ibiwa vitu vyako na mwisho ukaishia kurudi Dodoma mikono mitupu.

4. Kama hutojali weka wazi unachokuja kufanya hapa Dar ili tukushauri maana vijana wengi walikuja wakiwa na ndoto kubwa lakini wameishia kuuza kahawa, maji na karanga hapa mjini.

5. Kwa Dodoma ilivyo sasa unaweza kufanikiwa ukiwa hukohuko kama tu utatuliza akili yako na kuwa na focus kwa unachokifanya.

6. Maisha ya Dar es Salaam sio rahisi kama unavyoona kwenye post za facebook na instagram, watu wanaishi maisha magumu sana. Vijana wengi ni vibarua na wanalipwa ujira mdogo sana na wameishia kuishi kwenye mageto.

Ni hayo tu kwa leo.
Kaka yako.
 
Back
Top Bottom