Ili kupata passport, unatakiwa uwe na.
1. Cheti cha kuzaliwa.
2. Cheti cha kuzaliwa cha mzazi mojawapo.
3. Kitambulisho cha Taifa.
4. Kitambulisho cha Kazi Kwa watumishi wa umma au barua ya utambulisho KUTOKA Serikali za mitaa Kama hujaajiriwa.
5. Barua ya maombi ya passport kama uko mkoani anapitisha kwa kamishna WA mkoa kwenda Kwa kamishna mkuu, anwani zao za posta unaweza kuzipata ofisini kwao.
6. Uthibitisho wa safari ukionyesha nchi unayokwenda.
7. Baada ya kuwa na vielelezo vyote utaanza kujaza form ya maombi online kupitia uhamiaji portal, kuna sehemu uta upload barua ya utambulisho na Cheti cha kuzaliwa.
Kama ombi limekamilika utapewa contral namba ya kulipia 20,000 ili uweze Ku print form.
Ukishaprint form utatafuta mashaidi waijaze na pia mwanasheria.
8. Baada ya hapo utaenda ofisi za uhamiaji ukiwa na hiyo form na vielelezo nilivyotaja hapo juu,
9. Ombi litapitiwa kama hakuna dosari, litapitishwa, utalipia 130,000 Kwa kutumia control namba, halafu utakamilisha ombi Kwa kupiga picha pamoja na kuchukuliwa alama za vidole.
10. Baada ya hapo utasubiri Kwa mwezi mmoja passport kuwa tayari.
11. Kama unahihitaji Kwa haraka na hauna baadhi ya vielelezo unaweza watumia vishoka, Ila utawalipa gharama za ziada almost 100-200k.