Msaada wa kuondoa tattoo

barbieloree

Member
Joined
Jan 2, 2024
Posts
28
Reaction score
52
Habari wana JamiiForums samahanini nina ndugu yangu amebahatika kwenda jeshini lakini ana tattoo ya jina mkononi, anashinda ndani analia hajui aiondoe vipi maana akijichoma na pasi wanasema makovu hawataki.

Anahitaji msaada afanyaje ni kitu alichokipigania sasa amebahatika ndo iko hivo msaada nini afanye
 
Wachora tatuu watakupatia mwongozo, ila Binadamu tuna utaahira sana kiukweli. Unajichoraje mwilini kama chatu ilihali uliumbwa na ngozi nzuri tu?

Ubinadamu ni kazi/Humanity is a work.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Kila unachokifanya katika maisha yako jua kinaweza kuwa na matokeo hasi au chanya na huna budi kukubaliana na matokeo hayo,but kachelewa sana
Kunadawa zinauzwa na wachina wanadai zinaondoa makovu,mwambie ajaribu,
 

Attachments

  • Screenshot_20240404-164541.png
    667 KB · Views: 22
Amebahatika au ana mpango wa kwenda.
Kwanini unakuwa muongo Kwa sasa hakuna nafasi walizoitwa watu sio jeshi la wananchi Bali hata jkt hawajaita watu ila uhamiaji tu ndio wanakaribia kuanza kuripoti makambini huyo wako kabahatika wapi?
 
Sasa Yuko jeshini tayar kwahiyo huko aliingiaje
 
Angalia huko tiktok/ IG
Wanatangazaga wanafuta tattoo, na wakifuta sijui mimi panabaki aje.
Emish mcheck IG, uwa naona anapost status kuwa wanafuta tattoo
 
Nenda insta, account ya bwana ake Amber Rutty, anafuta tattoos na chale, wengi wamefanikiwa, nikiwepo mimi.
Nenda usipuuze.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…