Msaada wa kumjua baba yangu na ndugu zangu wengine

Msaada wa kumjua baba yangu na ndugu zangu wengine

Very true. Amelelewa na mama amekua mtu mzima tena amshukuru Mungu na elimu amepatiwa. Badala ya kusonga mbele na kuangalia future anamtafuta mtu ambae hata babu yake ajawahi kumuona. Ajiulizi hata kwanini mama yake ataki kumwambia ukweli! Vipi je kama mama alibakwa ndo akapatikana yeye.

Kijana ebu anza kufikiria wanao wataishi vipi siku watakapo patikana.

Pegine wala huyo anaemtafuta si baba'ke, mara nyingi watoto wanaofichwa baba zao huwa ni wa ndani ya familia (incest). Pengine ni wa huyo-huyo anaemwita babu yake.
 
Mpum...bavu yoyote mwenye uume unao simama, anaweza kumzalisha mwanamke, lakini ni mwanaume wa ukweli tu ndio anaye wza kutunza watoto wake na familia yake. Fatherhood does not determined by D.N.A, its determined by REPSONSIBILITY. Mwanaume aliye kulea ndio baba yako! Achana na huyo mpu...mbavu aliye mpa ujauzito mama yako.Matter fact ilikuwa ni starehe yake! Unless otherwise uniambie hauna vitu vya msingi vya kufanya!!! Miaka 25 unamtafuta 'baba' yako? wenzako wanatafuta hela!!! Plz respect yourself

IJUE KWELI NA KWELI ITAKUWEKA HURU!
watu wengi wanafikiri fedh ni kila kitu lakini wanashindwa kutambua umuhimu wa utu wao na matokeo yake yanatokea mambo yote ya ajabu ajabu badala ya kuangalia mambo ya msingi kwanza.
hili jambo si dogo kama mnavyofikiria katika ulimwengu wa kawaida, linaweza kuwa chanzo cha yeye kutofanikiwa na kuzipata hata hizo fedha mnazofikiria anatakiwa azipate.
huwezi kujua baba alitamkanini wakati anaachana na mama yake na ikawa ni laana kwa mtoto, lakini pia huwezi kujua ukoo aliotoka ni matambiko gani yanamfunga ambayo anatakiwa kupambana nayo ili asimame!
ni vigumu kunielewa lakini katika ulimwengu wa roho hicho kitu ni muhimu kuzidi unavyofikiria.
fedha kitu gani bana hata kwa mganga zinapatikana japo zinakuwa za mazingaombwe.
msimdanganye bwana hili ni muhimu
achilia mbali mahitaji yenu sio yake.
 
W

Ni rahisi kusema ivi labda kwa sababu umelelewa na wazazi wote wawili hauwezi kuhisi nn nafsi ya uyu jamaa inakosa hata alifanya makosa bado ni baba ake itabaki ivo sioni tatizo kuwatafuta ndugu zake usiombe kuonja kikombe hiki ki-chungu sn mtani nina uhakika hata ww una mapungufu kibao ukihukumiwa sijui itakuaje just say thnx 2 ur dad 4 being there 4 u ila usimuhukumu baba wa mwenzio haujui tofauti zao kwny mimba zilikua nn...m talkin' thru ma experience.
 
Habari wakuu kichwa cha habari chahusika!!!!!!
Mie nimezaliwa miaka 25 iliyopita kwa sasa nipo chuo kikuu kimoja hapa dar es salaam. Tangu nizaliwe miaka 25 iliyopita mpaka sasa baba yangu simjui kwa maana kila nikijaribu kumuuliza mama huwa mkali sana na naogopa kumkwaza nahisi labda ni kwa jinsi (baba) alivoikataa mimba au kuna jambo lingine mie sijui.Ila kuna siku nilikaa na babu ambaye ni mjomba wa mama, ambaye ni mwananjeshi mstaafu (babu ni mwanajeshi msitaafu) NIKAJARIBU KUMDADISI akaniambia kuwa baba yangu alikuwa ni mwanajeshi kambi ya lugalo (makongo) na alikuwa akiishi area D kwa maana hata babu yangu aliishi area D mpaka anastaafu!!! Sasa kuna siku nikamwambia anitafutie walau picha yake naye hakusita akatoa albamu tukatafuta ila kwa bahati mbaya hatukupata hata picha moja!!!! Nikamuomba anitajie jina lake akasema huyu ( baba yabgu) anaitwa RAJABU MKWAYU na alikuwa mwenyeji wa mkoa wa TANGA akaongeza kusema kuwa kuna kipindi alihamishwa kwenda kufanya kazi mahakama kuu na alikuwa akimwendesha JAJI MKUU na kwa bahati mbaya sana babu akaniambia kuwa huyu mzee RAJABU MKWAYU keshafariki ila ninachoamini ni kuwa japokuwa yeye kafariki atakuwa ameacha watoto wengine na ndugu wengine ambao sio mbaya kama nikiwafahamu.
MAOMBI KLANGU NI:
  1. Kama kuna mwanajeshi yeyote msitaafu au hata kama hajastaafu ambaye aliishi LUGALO kwenye zile KOTA za area D ana taarifa zaidi kumhusu baba yangu aniambie.
  2. Kama kuna mfanyakazi yeyote wa mahakama kuu ambaye alishawahi kuliona hili jina la RAJABU MKWAYU basi sio mbaya akanipa taarifa zaidi ili nijue huko TANGA alikuwa anatokea wilaya gani,tarafa na hatimaye kijiji ili niweze kufautilia japo niwajue ndugu zangu.
  3. Kama kuna mtu yeyote humu ambaye anamfahamu huyu mzee basi aniambie
  4. Kama kuna mtoto wake au ndugu yake mwingine humu basi sio mbaya tukawasiliana.
SAMAHANI KWA MPANGILIO MBAYA ILA NADHANI NIMEELEWEKA NA NAOMBENI MSAADA WENU.
Kuna mwanajeshi anaitwa Ramadhan Mkwayu yupo kambi ya jeshi pale kabuku-Tanga
 
Watu kama wewe hamjaanza leo, hata mitume walipokuja kuwakataza maovu mliwaambia hivyo-hivyo. Kipi kibaya na cha kuharibu mada ulichokiona wewe?

Mitume ni pamoja na mbakaji ? Au umesahau alizini na mkwewe ? Na kusimamia uporaji wa misafara ya wafanyabiashara, wewe bado wajinasibu kuwa Huyo naye ni mtume ? Mtume wa NGO.no !!!!
 
Mitume ni pamoja na mbakaji ? Au umesahau alizini na mkwewe ? Na kusimamia uporaji wa misafara ya wafanyabiashara, wewe bado wajinasibu kuwa Huyo naye ni mtume ? Mtume wa NGO.no !!!!

Hivyo ndivyo mnavyodanganywa. Kusoma hamuwezi basi hata picha hamuoni?

Na nyinyi mnakuja hapa kutetea maovu, tazama sasa huyu kijana hamjui baba'ke na anahangaika kwa sababu ya uzinzi tu, sijui kama wewe unamjuwa wako? Ikiwa leo kanisa linawaoza waume kwa waume? wachungaji wenyewe wanaowana wanaume kwa wanaume, wanawake kwa wanawake.

Tutegemee nini kutoka kwa mtu kama wewe? zaidi ya ujinga unaouonesha hapa.
 
IJUE KWELI NA KWELI ITAKUWEKA HURU!
watu wengi wanafikiri fedh ni kila kitu lakini wanashindwa kutambua umuhimu wa utu wao na matokeo yake yanatokea mambo yote ya ajabu ajabu badala ya kuangalia mambo ya msingi kwanza.
hili jambo si dogo kama mnavyofikiria katika ulimwengu wa kawaida, linaweza kuwa chanzo cha yeye kutofanikiwa na kuzipata hata hizo fedha mnazofikiria anatakiwa azipate.
huwezi kujua baba alitamkanini wakati anaachana na mama yake na ikawa ni laana kwa mtoto, lakini pia huwezi kujua ukoo aliotoka ni matambiko gani yanamfunga ambayo anatakiwa kupambana nayo ili asimame!
ni vigumu kunielewa lakini katika ulimwengu wa roho hicho kitu ni muhimu kuzidi unavyofikiria.
fedha kitu gani bana hata kwa mganga zinapatikana japo zinakuwa za mazingaombwe.
msimdanganye bwana hili ni muhimu
achilia mbali mahitaji yenu sio yake.

Ivi kama mtu kampa mimba mama wa watu,japo kweli hatujui kilicho tokea mpaka wakaachana bt matukio haya sio mageni kwetu, Leo mzazi wa watu kakuza kasomesha,kwa kipindi chote hicho baba hajajitokeza!! Ivi hata akijitokeza atamsaidia nini?? ni utu upi huo ataumuonyesha??

Mungu ana mipango na maisha ya kila mtu jamani, hakuna alie zaliwa kwa bahati mbaya eti. Haya ikatokea uyo baba alisha fariki kweli kama alivyo ambiwa hayo matamko yatafutwa na nani? Kwanini asisonge mbele na mambo yake? kama ni laana,mikosi na mengineyo kuna namna ya kuyafuta kimaombezi, inategemea na imani ya mtu.
 
Pegine wala huyo anaemtafuta si baba'ke, mara nyingi watoto wanaofichwa baba zao huwa ni wa ndani ya familia (incest). Pengine ni wa huyo-huyo anaemwita babu yake.

Kama tu akuona umuhimu wa mtoto akiwa tumboni leo ndo atamthamini!!Kama anajali kwanini hakumtafuta mpaka asubiri kutafutwa.
 
Kwanza, nakupa pole sana kwa yanayokufika.

Pili, nakupongeza, huu ni ujaasiri wa hali ya juu.

Tatu, hili ulilotoa hapa ni darsa kubwa sana kwa wanaoona uzinzi ni sifa.

Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya - Qur'an 17:32

Faiza,
Shikamoo,umetoa darsa zuri sana.
 
Nimeguswa sana na hiki kisa,pole sana ndugu yangu. Pia nafurahi kusikia upo chuo kikuu. Hongera sana.
 
Hivyo ndivyo mnavyodanganywa. Kusoma hamuwezi basi hata picha hamuoni?

Na nyinyi mnakuja hapa kutetea maovu, tazama sasa huyu kijana hamjui baba'ke na anahangaika kwa sababu ya uzinzi tu, sijui kama wewe unamjuwa wako? Ikiwa leo kanisa linawaoza waume kwa waume? wachungaji wenyewe wanaowana wanaume kwa wanaume, wanawake kwa wanawake.

Tutegemee nini kutoka kwa mtu kama wewe? zaidi ya ujinga unaouonesha hapa.

Kama matendo ya mtume wako ni ujinga : basi mjinga atakuwa sio Mimi wala mtume wako. Mjinga atakuwa yule aliyemtuma... Ujin.ga raha kweli unakufuru kwa shetani mungu wenu wala hujitambui na shetani alivyokatili subiri adhabu yake , au umesahau nini alimtenda Muhammad ?
 
Ivi kama mtu kampa mimba mama wa watu,japo kweli hatujui kilicho tokea mpaka wakaachana bt matukio haya sio mageni kwetu, Leo mzazi wa watu kakuza kasomesha,kwa kipindi chote hicho baba hajajitokeza!! Ivi hata akijitokeza atamsaidia nini?? ni utu upi huo ataumuonyesha??

Mungu ana mipango na maisha ya kila mtu jamani, hakuna alie zaliwa kwa bahati mbaya eti. Haya ikatokea uyo baba alisha fariki kweli kama alivyo ambiwa hayo matamko yatafutwa na nani? Kwanini asisonge mbele na mambo yake? kama ni laana,mikosi na mengineyo kuna namna ya kuyafuta kimaombezi, inategemea na imani ya mtu.

unachosema ni kweli
bado yule mzazi aliyemtunza ataendelea kubaki na heshima ileile na sio kwamba akikutana na baba yake kuwa atabadilisha kitu lakini kuna umuhimu mkubwa sana.
hata ukienda kwenye huduma kama unaelewa chanzo cha tatizo lako na kwa kiasi fulani ulifanya juhudi kulimaliza katika mwili unafunguliwa vizuri sana.
kwa kuwa unajua unapiga wapi kuliko ukiwa mweupe
huyu hamwitaji baba yake kwa kuwa anataka msaada au kutunzwa naye anachotafuta ni true identity.
unajua wale ambao mmezaliwa kwenye ndoa halali mkilelewa na wazazi wote wawili hata kama baba hana mchango katika maelezi yako huwezi kuelewa ni kwa kiasi gani hiki kitu kinaumiza.
na unaweza kuona ni upuuzi tu lakini hiki kitu kinawaumiza watu wengi hata wale ambao wamefanikiwa kuwa na maisha mazuri.
nina rafiki yangu mmoja ambaye yeye baba yake na mama yake waliachana akiwa mdogo na baba akarudi kwao nchi moja ya ulaya huwa hana furaha
pamoja na kuwa na kila kitu na utajiri wa mabilion shule nzuri lakini mpaka leo amechemsha kumuona baba yake na ameshamtafuta kwakwenda katika hiyo nchi zaidi ya mara mbili
hivyo hili sio swala la mzaa.
 
mkuuuu nakusubiri mkuuu naona kimya
Akina Mkwayu ni watu WA LUSHOTO-TANGA, Kuna Mzee mmoja alikua mwanajeshi alifariki ILA sina uhakika alikua akijulikana kwa jina gani. Nitajitahidi kupata details za akina MKWAYU kutoka LUSHOTO vijiji vya Ngulwi na Kituja then I will get back to you. Unaweza kuni-PM maana naona akina faiza kama kawaida yake anataka kuharibu mada. Mwanamke mlaanifu huyu
 
Watu mnapanic ! Kama hujui /humjui ustaarabu bei gani?
Hongera kijana kwa ujasiri, utampata/utawapata ndugu zako hapa ndo jf!
Goodluck
 
Hakuna kitu kinachouma kumkosa baba,hata awe kichaa au katili baba ni baba.Kwa wale ambao hali kama hii haijawahi kuwakuta,ni rahisi kuongea chochote mnachojiskia.Hii hali inauma sana tena sana,ni rahisi kusema aliyekutunza kusema huyo ndo mzazi,ubinadamu si vitu kama elimu,matunzo nk,ni ukamilifu wa nafsi.Masahibu ya namna hii yanawapata wengi,na mbaya zaidi inakukuta ukiwa mtoto.Mleta mada nenda hapo mahakama kuu,orodha ya madereva waliowahi kumwendesha Judge Mkuu utaikuta na utasaidiwa.Ni vema kuijua asili yako,hii ina maana kubwa sana kimaadili kwa sababu isije ikatokea siku moja unamuoa ndugu yako.Mkuu fight for your roots!!
 
Pole kijana na nakutakia kila la heri katika harakati zako za kumtafuta baba yako.
Kila mtu anajua umuhimu wa akifanyacho hivyo naamini nawe kumtafuta baba yako lina umuhimu kwako.
Usikatishwe tamaa
 
Back
Top Bottom