djesco
Senior Member
- Jun 26, 2013
- 166
- 52
Habari wakuu kichwa cha habari chahusika!!!!!!
Mie nimezaliwa miaka 25 iliyopita kwa sasa nipo chuo kikuu kimoja hapa dar es salaam. Tangu nizaliwe miaka 25 iliyopita mpaka sasa baba yangu simjui kwa maana kila nikijaribu kumuuliza mama huwa mkali sana na naogopa kumkwaza nahisi labda ni kwa jinsi (baba) alivoikataa mimba au kuna jambo lingine mie sijui.Ila kuna siku nilikaa na babu ambaye ni mjomba wa mama, ambaye ni mwananjeshi mstaafu (babu ni mwanajeshi msitaafu) NIKAJARIBU KUMDADISI akaniambia kuwa baba yangu alikuwa ni mwanajeshi kambi ya lugalo (makongo) na alikuwa akiishi area D kwa maana hata babu yangu aliishi area D mpaka anastaafu!!! Sasa kuna siku nikamwambia anitafutie walau picha yake naye hakusita akatoa albamu tukatafuta ila kwa bahati mbaya hatukupata hata picha moja!!!! Nikamuomba anitajie jina lake akasema huyu ( baba yabgu) anaitwa RAJABU MKWAYU na alikuwa mwenyeji wa mkoa wa TANGA akaongeza kusema kuwa kuna kipindi alihamishwa kwenda kufanya kazi mahakama kuu na alikuwa akimwendesha JAJI MKUU na kwa bahati mbaya sana babu akaniambia kuwa huyu mzee RAJABU MKWAYU keshafariki ila ninachoamini ni kuwa japokuwa yeye kafariki atakuwa ameacha watoto wengine na ndugu wengine ambao sio mbaya kama nikiwafahamu.
MAOMBI KLANGU NI:

- Kama kuna mwanajeshi yeyote msitaafu au hata kama hajastaafu ambaye aliishi LUGALO kwenye zile KOTA za area D ana taarifa zaidi kumhusu baba yangu aniambie.
- Kama kuna mfanyakazi yeyote wa mahakama kuu ambaye alishawahi kuliona hili jina la RAJABU MKWAYU basi sio mbaya akanipa taarifa zaidi ili nijue huko TANGA alikuwa anatokea wilaya gani,tarafa na hatimaye kijiji ili niweze kufautilia japo niwajue ndugu zangu.
- Kama kuna mtu yeyote humu ambaye anamfahamu huyu mzee basi aniambie
- Kama kuna mtoto wake au ndugu yake mwingine humu basi sio mbaya tukawasiliana.