Msaada wa kujivua gamba tafadhari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wa kujivua gamba tafadhari

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by kabila01, May 20, 2011.

 1. kabila01

  kabila01 JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2011
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 3,015
  Likes Received: 1,828
  Trophy Points: 280
  Habari wana JF
  Hapa nilipo nina mpenzi wangu ambaye tuna miezi 8 sasa tokea tumeanza urafiki wetu. Huyu mpenzi wangu ananipenda sana lakin mimi moyoni mwangu hayumo kabisa, najitahidi kila mara angalau kumkasirisha nikidhani labda anaweza aka give up lakin wapi, shida yeyote nayoipata yupo mstari wa mbele kunisaidia. Sasa kila nikitaka kumwacha nashindwa maana naona ntamuumiza sana bint wa watu na nikisema niendelee naye nifunge ndoa nashindwa maana moyoni hajakaa kabisa
  Naombeni msaada wana JF jinsi ya kujivua gamba kwa huyu binti
   
 2. pangalashaba

  pangalashaba JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 1,089
  Likes Received: 885
  Trophy Points: 280
  nimekupata............ pole sana kwa kutompenda binti wa watu. subiri wataalamu wa masuala ya mahusiano,watakuja sasa hv na ushauri mzuri!!!!
   
 3. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #3
  May 20, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Kabila01 pleeeease be gentle with her but mwambie ukweli, siku zinapozindi kwenda ndo unaharibu.... Nashangaa sana (enways ktk mapenzi enthin is possible) kua umempata mdada anae kupenda lakini humpendi... Nakuonea huruma mana kupata mtu ambae ana mapenzi genuine kwako sasa hivi ni kazi sana.

  Wewe ndo unamfahamu vizuri hivyo the best way of breaking her heart iko mkononi mwako - ingawa naamini in which ever way utamwambia lazima ataumia. Acha kumpotezea mda tafadhali...
   
 4. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  muweke chini umueleze ukweli kwamba huna hisia sawa na zake...atakuelewa, japo ataumia lakini huna jinsi.
  ukiendelea tu huku moyoni hujaridhika, na siku zinaenda af itokee ghafla bin vuu umemuona umpendaye..hapo utamuumiza zaid.
   
 5. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #5
  May 20, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Sasa hapo tukusaidie nini wakati umeishasema haumpendi binti wa watu.
   
 6. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #6
  May 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Jamani dahhhh
  Kama waona si wako
  Basi usimzibie Ridhiki
  bora umwambie sasa..
  Itamuuma sana lakini
  ni bora kuliko kukaa usipopendwa..
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,499
  Likes Received: 19,913
  Trophy Points: 280
  bibie mambo, hapo kwenye red ni kosa kubwa sana ni bora akaanza tu kuwa mbali naye ,asiwe anampigia simu asiwe anapokea simu zake mar kwa mara , na kama una gf fanya fanya ili akuone naye
   
 8. Kaka Mpendwa

  Kaka Mpendwa JF-Expert Member

  #8
  May 20, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 771
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kama humpendi na una hakika kwamba haumpendi, ni vyema ukajitahidi umwambie ukweli sasa, kuliko kumletea maumivu makubwa hapo baadaye??

  Na kwanini ushindwe kumpenda mtu anayekupenda?..Hebu jichunguze vizuri..Punguza mawasiliano na mabinti wengine, mpe kipaumbele katika maisha yako. Upendo mzuri ni ule unajengeka na kukua taratibu..
   
 9. duda

  duda Senior Member

  #9
  May 20, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unamaanisha nn sasa kumshauri mwenzako ivo? umeniboa
  kwani ni kipi kimshinde kusema ukweli, yn wanaume wetu nyie kwa uongo???????? sijui mtaacha lini?. hakuna kitu kibaya kama kumuonyeshea gf mwingine, amweleze ukweli tu kwamba hana hisia nae, atamuelewa.
   
 10. k

  kisukari JF-Expert Member

  #10
  May 20, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,763
  Likes Received: 1,052
  Trophy Points: 280
  usimchoreshe binti wa watu,mwambie ukweli,ataumia lakini is for the best kwa upande wake.ila mwambie kistaarabu na umwambie hana tatizo lolote lile{wengine wakiachwa hujihisi maybe wana kasoro fulani}
   
 11. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #11
  May 20, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Mara ya kwanza ulipomtokea ulimwambiaje? Unampenda? Too bad, fikiri ungekuwa wewe. Act gently, kama mara ya kwanza ulimpenda na ukamtamani how come after 8 months usimpende tena?
  Ili kumsaidia mwambie ukweli, usiume maneno ili alie na baada ya muda atapona tu.
   
 12. Kbd

  Kbd JF-Expert Member

  #12
  May 20, 2011
  Joined: Oct 9, 2009
  Messages: 1,264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Ninauhakika wewe ndie uliyemtokea na baada ya miezi kadhaa ndio umegundua humpendi. Nikuhakikishie tu kuwa utavuna ulichokipanda.
   
 13. TATE

  TATE Member

  #13
  May 20, 2011
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Labda naweza kukuelewa ukisema baada ya kuingia kwenye relationship you didn't find what you were looking for au ulimtamani tu, it happens. Cha msingi be a man about it, tell her the truth, it is the best thing you could do for her. In future it is better to be clear about your feelings, kama unamtokea msichana mwambie wazi, we are just dating anything can happen, you can even date for a year before you decide to commit.
   
 14. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #14
  May 20, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  Dah! Ulikuwa humpendi tangu awali au ni siku hizi? Nahisi kuna mambo fulani fulani yamesababisha hayo. Kama hayupo moyoni ni nani aliye moyoni kwa sasa?
  Ondoa mawazo kwa huyo unaye mfikiria na uyarudishe kwa mpenzi wako.
  Au unataka kumwacha ubaki single kwa sasa?
  Kama ndio mwambie ukweli.
  Kama unataka kumwacha ili utafte mwingine unakosea maana uliye nae inaelekea anakupenda kwa dhati, ni suala la kuruhusu hisia zako zihisi unavyohisi. Hilo gamba nakushauri usilivue. Tafuta super glue ulibandike vizuri.
   
 15. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #15
  May 20, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Mi nakushauri utoke humu maana napata wasiwasi na U-Great Thinking wako mkuu....!
   
 16. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #16
  May 20, 2011
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  mi mwenyewe nataka kujivua gamba naombeni mwongozo....:tape::car:
   
 17. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #17
  May 20, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Pole sana mkuu, hilo tatizo lako nimelielewa vizuri sana kwasababu nilishawahi kupitia mtihani huo. Nilipokuwa chuo mwaka wa kwanza(Chuo nakihifadhi) nikiwa sina Girlfriend nikakamata msichana mmoja kwa ajiri ya kupotezea mda(kwa wakati ule nilimuona siyo mzuri sana ukilinganisha na wasichana wengine hivyo niliona huyu awe wa kupita tu) kadiri mda ulivyokuwa unakwenda ndipo akawa ananionyesha mapenzi ya hali ya juu sana ikafikia wakati hata upande wa kwetu yaani dada zangu, kaka zangu mpaka wazazi wakawa wanamfahamu, hii ni kutokana na ushiriki wake katika matatizo yaliyokuwa yanatokea nyumbani kwetu japo mimi kwao nilikuwa sitokei hata kama kuna msiba, nikiwa mwaka wa pili zoezi la kujitoa likaanza ili nitafute mtu nimpendaye. Nilimfanyia vituko vingi sana lakini haikuweza kutuachanisha na wakati mwingine nilimfanyia mambo ambayo yaliniumiza sana hata mimi kama binaadamu hatimaye mwaka wa Tatu nilifanikiwa kumpiga chini japo nilimsababishia matatizo makubwa mdada huyu mpaka akapata supplementary katika masomo mawili ambayo aliyarudia hakufanikiwa ku-clear somo moja, alirudia mwaka wa tatu mimi nikamaliza chuo nikaingia mtaani na nikapata kazi. Nikajikita na demu nimpendaye alikuwa pale IFM 2nd year (nilikuwa nimeanza ku-cheat naye wiki chache nyuma na ndiyo iliyonipelekea spidi kubwa ya kumpiga chini msichana niliyekuwa naye) nilispend naye for 8 months nikaachana naye kwa aliyonitendea(sitopenda kuyataja hapa kwani siyo jukwaa la wakubwa) Huwezi amini hapa ndipo nilipomkumbuka yule mdada niliyemuacha ningakundua mtu wa kuishi naye aangaliwe kwa factor zaidi ya moja. Binafsi yule msichana nilimuacha kwasababu tuu nilikuwa naona wasichana wengi wazuri zaidi yake, nilikaa kama miezi kadhaa sina permanent Girlfriend ndipo nikagundua hii siyo life maadamu niligundua makosa yangu nikafuatilia kama yule msichana ana mtu nikaambiwa hana mtu na amepoteza kabisa hali ya kuwa na boyfriend. Ilinichukua mda mrefu sana kumuelekeza kama najuta kwa niliyoyafanya nikamsisitiza kwamba nahitaji awe mama watoto wangu alinikatalia katakata hii ilikuwa mwaka 2005 mwanzoni, baadaye nikawatumia rafiki zake na nikawaambia ukweli kwa kila kitu mwishoni mwa 2006 nilikubaliwa ombi langu upya akiwa ndo amemaliza chuo, Harusi yetu ilikuwa mwanzoni mwa mwaka2008 na sasa tuna mtoto mmoja aliyepatikana mwanzoni mwa 2010, tunaishi vizuri tunaheshimiana na kutokana na tabia yake amekuwa ni mwanamke mzuri sana kwangu hanichoshi(NINAMPENDA SANA) japo najutia sana doa nililoliweka katika historia yetu. Plz nakushauri jiulize mara mbilimbili ni kitu gani kinachokufanya usimpende huyo mwanamke japo umekuwa naye for sometimes. Nimeiandika haraka lakini hii ni true story. For sure waweza kumuacha kwasababu ambayo inaweza ikufanye ujute sana kwa kumpoteza mtu akupendaye kwasababu kupata mtu akupendaye kwa dhati ni kazi ngumu sana hasa katika umri ambao mtu umekwisha rekebisha maisha kiasi fulani.
   
 18. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #18
  May 20, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  Pole na hongera kwa ezan.
   
 19. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #19
  May 20, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  gamba lako ufe nalo.
   
 20. TATE

  TATE Member

  #20
  May 20, 2011
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  truth will set you free, kwa sasa huo ndo mwongozo naweza kukupa
   
Loading...