afkombo
Member
- Feb 9, 2008
- 93
- 11
Habari wana JF!!Mimi ni mwanafunzi nasomea udaktari lakini huwa navutiwa sana juu ya kufahamu ufanyaji kazi wa Computer!!Nina maswali mawili
1:Kwa nini ukinunua Computer mpya,ukishai-format,ikifika sehemu ya kuchagua regional and language options katika masuala ya muda na tarehe,kwa nini unapochagua tu kwa mfano (GMT +03:00)Nairobi au (GMT +08:00)Beijing nk,ukisha-click "OK" tu basi inakuletea muda kamili wa sehemu hiyo.Sasa mi nauliza hii computer inatoa wapi hizi informations ambazo ziko sahihi namna hii wakati ndiyo nimetoka kuiformat muda si mrefu na sijaunganisha katika internet ?kwa nini isingingeniambia nirekebishe saa na tarehe kama ninavyofanya kwenye saa yangu ya mkononi au simu?Je,hizi informations zinapatikana kutoka katika Windows au Computer yenyewe inajua mambo hayo yote kabla hata ya kuinstall windows?kivipi?
2:Kwa nini ninapozima computer yangu hata kwa week nzima,na huwa nachomoa waya inayounganisha kwenye umeme,lakini siku nikiiwasha tena inaniletea tarehe na muda sahihi wa siku hiyo?Nilisoma baadhi ya article zinazohusu CMOS na BIOS,lakini maneno mengi yaliyotumika ni ya ki-physics maana kwa hiyo sijaelewa vizuri.Je,hata kama nikiizima kwa mwaka mmoja inaweza kuniletea informations kamili?kwa nini?
Mwenye ujuzi huo naomba animegulie tena kama itawezekana katika lugha ya kiswahili ili nielewe vizuri.NB siyo maneno yote,maana kuna baadhi ya maneno ya kisayansi siyajui kwa kiswahili.
Ahmad Kombo,Xi'an Jiaotong University,P R China
Na kama kuna mwenye kutaka kunisaidia in private e mail yangu ni afkombo@hotmail.com