ris
Member
- Jun 16, 2017
- 73
- 109
Wanajamvi naombeni msaada wenu wa kisheria katika hili.
Iko hivi nina mdogo wangu wa hiari (tumekutana kazini sina vinasaba nae) mnamo mwezi wa nne alisimamishwa kazi.
Hivyo kutokana na majukumu ya kifamilia akaamua ajiingize kwenye biashara ya kununua mahindi na kuuza.
Changamoto ikawa mtaji maana mzigo upo ila mtaji haukidhi akajaribu kuomba mikopo ikashindikana akaamua kuuza baadhi ya vitu vyake vya ndan kama tv, fridge na kiwanja kimoja (alikua na viwanja viwili).
Mambo yote hayo alikua anayafanya na rafiki wa karibu sana ambapo walifanikisha kuuza vitu vya ndani kwa haraka kuliko kiwanja. Hivyo ikamlazimu dogo arudi vijijini kutafuta mahindi akampa taarifa huyo rafiki yake kuwa wasitishe zoezi la kuuza kiwanja. Wakati akiwa kijijini jamaa yake aliingia nyumbani kwa dogo akaibia document zote za viwanja akaenda akauza na hela akaenda akanunua gari ya kutembelea. Dogo akiwa kijijini aliibiwa hela tsh milioni tisa
Akaamua arudi mjini kuuza viwanja vyake aongezee mtaji maana tayari umepungua anakuta kiwanja kimoja kuna mtu anajenga kufuatilia anaambiwa kwenye uongozi wa mtaa anaambiwa viwanja vyake vimeuzwa viwili na alipigiwa simu siku vinauzwa na akatoa ruhusa (yeye dogo anadai hakupigiwa simu)
Ameenda polisi wamemuambia kama hana copy za document za ununuaji wa viwanja akubali tu maumivu wao hawana cha kumsaidia.
Amejaribu kukutana na wamiliki wapya wa viwanja kwa maongezi ya usitishaji wa ujenzi lakini huyo rafiki yake anawaambia nyie endeleeni na ujenzi huyo hana documnet zozote asiwatishe. Sasa dogo amekwama asijue nini cha kufanya hivyo naomba kwa wenye ujuzi mtusaidie msaada wa kisheria hapa tunafanyaje.