Msaada wa kisheria kuhusu mikopo katika Mabenki

Mar 6, 2017
31
95
Habari za maisha wote mtakaopitia hapa. Ninahitaji msaada kuhusiana na mkopo nilioufanya katika moja ya benki hapa nchini.

Mie ni mwajiriwa katika manispaa ya Lindi mwaka wa sita sasa, tangu niajiriwe sikuwahi kufanya mkopo na benki yoyote hadi ilipofika mwaka jana mwezi wa nane nikalazimika kutafuta mkopo wa milioni 5 (Marejesho yawe miaka miwili Sep 2019-sept 2021).

Kabla mkopo huo haujaingizwa katika akaunti nikaugua na kulazimika kuja Dar (Muhimbili) katika matibabu. Mkopo ukaingizwa kwenye akaunti yangu na mie nikaichukua pesa hiyo.

Miezi ikapita takribani minne bila benki husika kunikata pesa hiyo katika mshahara, nikajaribu kuwasiliana nao mie nikiwa bado katika matibabu lakini sikupewa ushirikiano.

Niliporejea kazini baada ya kupona tatizo langu nilikwenda moja kwa moja katika benki hiyo ili nijue kwanini walikuwa hawajakata pesa kwa muda wa miezi minne? (Nilifanya hivyo sababu awali lengo lilikuwa kuchukua milioni 18 lakini sababu ya kuanza kuugua wakati najaza fomu ya mkopo nilipunguza nakuchukua milioni 5 tu huku nikisubiri nipate nafuu ya ugonjwa na miezi sita ipite ili ni top up mkopo ).

Kwa muda wote huo benki hawakuwa na taarifa kuwa sijaanza kukatwa hadi nilipojitokeza na kuulizia iweje sikatwi.

Baada ya majadiliano ya muda mrefu nilichogundua na wao pia wamekisema ni kuwa afisa utumishi wangu hakuingiza makato katika mfumo licha ya afisa wa mikopo wao kuipeleka fomu yangu kwa wakati.

Sasa kutokana na miezi minne kupita bila kukatwa pesa hiyo katika mshahara wangu, kuna kitu kimeongezeka wanakiita malimbikizo Tsh 943,126.76(arrears) hivyo wananitaka nijaze fomu upya kwa makato mapya (awali ilikuwa nikatwe 236,157.51 kwa mwezi kwa muda wa miezi 24) na sasa wanataka waongeze hadi 260,115.51 kwa mwezi kwa muda wa miezi 24.

Je, kisheria kosa hilo la kiutendaji lililofanywa na afisa mikopo wa benki hiyo na Afisa utumishi wangu adhabu yake naibeba mimi kwa kuongezewa makato katika mshahara.

Mpaka sasa sijakubaliana nao kujaza fomu hiyo ya makato mapya ili nipate ushauri kutoka kwa wadau wenye uelewa na hili.

Tafadhali msaada wenu ni muhimu sana.

Shukrani zangu za pekee
 

Dig the EA

Senior Member
Dec 7, 2017
102
225
Babia Ndonga Shokoloo, Hiyo ni ngumu kukwepa, kama hutaki kuongezewa makato, omba uongezewe muda.

Hilo walalotaka kufanya litakuwa lipo kisheria, limeandikwa kwenye mkataba wako na ulisaini mkataba. Kama una kifua kipana tafuta wakili akusaidie.

Lakini kwa nini na wewe ulienda kuomba- ungekausha tu-kimya!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom