Amaizing Mimi
JF-Expert Member
- Feb 2, 2019
- 477
- 1,066
Habari za muda wana JF.
Naomba nijikite kwenye mada moja kwa moja.
Jana watoto wa kakaangu walikuwa wanachunga ng'ombe huko kijijini kwetu.sasa kuna wanafunzi wawili wakawa wanarudi nyumbani kutoka shuleni.
Wale watoto wa kaka wakaanza kuwafukuza.(umri wa wale watoto wa kaka ni miaka 12 na 13). Wakati wanafukuza wakatokea watu wengine, wale watoto ikabidi wakimbie waache mifugo.wale jamaa wakaswaga ng'ombe hadi polisi,kufika polisi wale jamaa wakatoa maelezo kuwa wale watoto walikuwa wanataka kuwabaka wanafunzi.Leo kaka ameenda polisi akaambiwa awapeleke wale watotokwanza(wachungaji wa ng'ombe).
Kaka amefanya hivyo sasa baada ya kuongea sana polisi wanataka millioni tatu ili wkufuta kesi na pia ili kaka arudishiwe ng'ombe wake.
Naomba msaada namna ya kumnasua kaka ni hizi gharama maana milioni tatu ni hela nyingi mno.