Naomba ushauri wa kisheria kuhusu suala hili la ndoa

mnangagwa

JF-Expert Member
Dec 3, 2017
978
1,424
Kuna jambo naomba msaada wenu wa kisheria. Nilioa mwaka2008 ndoa ya kiislam, mwaka 2019 mke wangu aliondoka nyumbani na kuniachia watoto wa4 baada ya kutoa mimba ya hawara, kutishia kuniua na kutishia kuwawekea watoto sumu.

Baadae akaanza harakati za kunishtaki polisi, Ustawi wa jamii, Bakwata na karejea Tena Ustawi wa jamii manispaa ilala akiwa na malalamiko yafuatayo:

a) Anahitaji nimkabidhi watoto wote niliozaa nae na hatonidai huduma yoyote,hili nililikubali Ila tu Kama litaandikwa kisheria, alivyoona nimeng'ang'aniwa makabidhiano ya watoto yawe kisheria akaingia mitini.

b) Anahitaji watoto walioko shule std vii Musoma niwarejeshe DSM kwa kuwa nimewahamisha bila ridhaa yake
Mwisho wa siku hatukufikia muafaka suala ikabidi liende mahakamani kitengo cha watoto, kuja kushtuka suala halijapelekwa mahakamani Ila limeletwa kazini kwangu likiwa na madai mapya ya kuwatendea ukatili watoto kwa kuwapiga nikishirikiana na mke wangu wakati hata Serikali ya Mtaa hili Jambo halijaripotiwa kwao au kuripotiwa polisi, nifanyeje ili niwashtaki Hawa maafisa Ustawi jamii kwa kunipachika tuhuma ambazo sio za kweli?
 
Dalili tosha za kupiga chini jimama ubakie na vifaranga. Kama ameshatotoa unachotaka tena n nn
 
Pambania wanao hata kwa Panga
 
Kama kipato kiko vizuri; peleka watoto wako shule za bweni, na wewe ndio uwe unawahudumia kila kitu, mwanamke muache akapambane na maisha yake mapya.
 
Kwanini unataka kuwashtaki hao uliowataja kama ma Afisa Ustawi wa jamii? tia nyama kwanza hapo.
Kwa sababu shauri nililoitia mwanzo Kama nilivyoeleza hapo juu na hatukufikia muafaka tulikubaliana liende mahakamani kitengo Cha watoto,
Matokeo yake wamenizushia tuhuma mpya ambazo hazikuwepo awali na hazijatipotiwa kwa mjumbe,Serikali ya Mtaa au polisi,hizi ni dalili Tosha za kuchafuana na kuharibiana kazi,
Ndo maana naomba msaada wenu ni namna gani naweza kumshtaki huyu afisa Ustawi wa jamii kwa kunipachika tuhuma ambazo sio za kweli.
 
Kataa kabisa watoto kumpa ex wako ana mtego wake huyo life la nje limemshinda sasa anataka kufaidika kupitia kwako. Pia ukimpa watoto anaweza wapanga kama wewe ilikuwa ukiwa baka au kuwafanyia mambo mabaya. Jasusi limekuja kutimiza maangamizi hilo.
 
Unaposomewa shitaka kuna kukubali au kukataa, sasa cha kufanya ww kataa,kwamba sio kweli kisha wao wataleta wataambiwa wadhibishe juu ya shitaka lao la ww kuwapiga watoto na mke wako, lkn pia umwambie bosi wako juu ya kile anachokufanyia x wako. Na uwaeleze ndugu wa pande zote mbili nao wajue ,,kama baba mzazi wa x wako nk, hapo unaweza ukapata jambo zuuuli

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Kwa sababu shauri nililoitia mwanzo Kama nilivyoeleza hapo juu na hatukufikia muafaka tulikubaliana liende mahakamani kitengo Cha watoto,
Matokeo yake wamenizushia tuhuma mpya ambazo hazikuwepo awali na hazijatipotiwa kwa mjumbe,Serikali ya Mtaa au polisi,hizi ni dalili Tosha za kuchafuana na kuharibiana kazi,
Ndo maana naomba msaada wenu ni namna gani naweza kumshtaki huyu afisa Ustawi wa jamii kwa kunipachika tuhuma ambazo sio za kweli.
Afisa ustawi wa jamii hana kosa,yeye ametimiza majukumu yake,ameletewa malalamiko na mzazi mwenzako,yeye ameyafanyia kazi,kikubwa na uhakika na wewe watakusikiliza kwa upande wako,hakuna hukumu inayotoka bila mlalamikiwa kujitetea
 
Back
Top Bottom