Msaada wa kisheria: Dada yangu katapeliwa nyumba Dodoma

radika

radika

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Messages
17,395
Points
2,000
radika

radika

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2014
17,395 2,000
Bila kupoteza muda niende kwenye mada.

Dada yangu na mume wake walinunua nyumba dodoma maeneo ya Nkuhungu ambayo waliuziwa na mdogo wa mwenye nyumba basi katika hayo mauziano alikuwepo wakili wasonga maarufu sana hapo Dodoma na Mwenyekiti wa kijiji kama shahidi na kulisimamia hilo zoezi.

Baada ya kama miaka kama mitano kupita aliibuka dada wa marehemu na kusema kwamba alieuza nyumba mdogo wao wa kiume hana mamlaka hayo na amelaghaiwa ktk kuuza kesi ikaanza ktk mabaraza ya kata ndipo wakina dada wakaomba aletwe ndugu yao aongee au aonekane jambo ambalo walipinga ndugu wa muuzaji kwamba hayupo kapotea.

Baada ya kuhangaishana sana walianza kutembeza rushwa ndipo waliposhinda kesi na dada yangu kushindwa na inasemekana mumewe na huyo dada yupo serikalini alikuwa akitumia hiyo fursa.

Dada alikata rufaa mahakamani bado hukumu zilitoka kama mwanzo maana michezo ilianza toka katika mabaraza ya ardhi ya kata wazee wa mabaraza tayari walikuwa wanajua nini cha kufanya.

Ilifika kipindi wakili wasonga alijitoa ktk kesi kwamba kesi imekuwa ngumu kwao wakati ktk mauziano ya nyumba alishiriki na kukagua hati za mauziano za nyumba na hata kubadili umiliki wa nyumba kwenda kwa dada na mumewe na allikuwa akilipwa kila hatua gharama za huduma yake.

Lengo langu naombeni msaada dada yangu alitolewa ndani ya nyumba na nyumba ikauzwa haraka sana.

Pia naweza nikawa sijatoa maelezao ya kunyooka sana kama kuna atakae hitaji kumsaidia kisheria na ushauri namba zake ni hizi.

0712 505 872
 
byembalilwa

byembalilwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2012
Messages
1,891
Points
2,000
byembalilwa

byembalilwa

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2012
1,891 2,000
Bila kupoteza muda niende kwenye mada.

Dada yangu na mume wake walinunua nyumba dodoma maeneo ya nkuhungu ambayo waliuziwa na mdogo wa mwenye nyumba basi katika hayo mauziano alikuwepo wakili wasonga maarufu sana hapo dodoma na mwenyekiti wa kijiji kama shahidi na kulisimamia hilo zoezi.

Baada ya kama miaka kama mitano kupita aliibuka dada wa marehemu na kusema kwamba alieuza nyumba mdogo wao wa kiume hana mamlaka hayo na amelaghaiwa ktk kuuza kesi ikaanza ktk mabaraza ya kata ndipo wakina dada wakaomba aletwe ndugu yao aongee au aonekane jambo ambalo walipinga ndugu wa muuzaji kwamba hayupo kapotea.

Baada ya kuhangaishana sana walianza kutembeza rushwa ndipo waliposhinda kesi na dada yangu kushindwa na inasemekana mumewe na huyo dada yupo serikalini alikuwa akitumia hiyo fursa.

Dada alikata rufaa mahakamani bado hukumu zilitoka kama mwanzo maana michezo ilianza toka katika mabaraza ya ardhi ya kata wazee wa mabaraza tayari walikuwa wanajua nini cha kufanya.

Ilifika kipindi wakili wasonga alijitoa ktk kesi kwamba kesi imekuwa ngumu kwao wakati ktk mauziano ya nyumba alishiriki na kukagua hati za mauziano za nyumba na hata kubadili umiliki wa nyumba kwenda kwa dada na mumewe na allikuwa akilipwa kila hatua gharama za huduma yake.

lengo langu naombeni msaada dada yangu alitolewa ndani ya nyumba na nyumba ikauzwa haraka sana.

pia naweza nikawa sijatoa maelezao ya kunyooka sana kama kuna atakae hitaji kumsaidia kisheria na ushauri namba zake ni hizi

0712 505 872
mada za utapeli mbona zimekuwa nyingi leo.
 
byembalilwa

byembalilwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2012
Messages
1,891
Points
2,000
byembalilwa

byembalilwa

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2012
1,891 2,000
hiyo namba upigiwe au sijaelewa?
 
Petro E. Mselewa

Petro E. Mselewa

Verified Member
Joined
Dec 27, 2012
Messages
8,762
Points
2,000
Petro E. Mselewa

Petro E. Mselewa

Verified Member
Joined Dec 27, 2012
8,762 2,000
Mkuu, sasa hapo ametapeliwa au ameshindwa kesi? Unaweza kuthibitisha utolewaji wa rushwa unaoudai? Kwasasa imekuwa desturi, kila anayeshindwa mahakamani hudai kutolewa kwa rushwa. Nashauri uende kwa Mawakili wengine, ukiacha huyo Wasonga uliyemtaja, na kuwaeleza jambo lako kwa msaada wa kisheria na wa uhakika.
 
radika

radika

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Messages
17,395
Points
2,000
radika

radika

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2014
17,395 2,000
Mkuu, sasa hapo ametapeliwa au ameshindwa kesi? Unaweza kuthibitisha utolewaji wa rushwa unaoudai? Kwasasa imekuwa desturi, kila anayeshindwa mahakamani hudai kutolewa kwa rushwa. Nashauri uende kwa Mawakili wengine, ukiacha huyo Wasonga uliyemtaja, na kuwaeleza jambo lako kwa msaada wa kisheria na wa uhakika.
Mkuu hayo mazingira ya hiyo kesi kushindwa yanatia mashaka sana ni vingi kafanyiwa ikiwa ni pamoja kutokupewa haki ya kutokusikilizwa ktk mabaraza ya kata ya ardhi
 
F

FRESHMAN

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Messages
3,316
Points
2,000
F

FRESHMAN

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2011
3,316 2,000
kwa nini ununue nyumba ya marehemu kwa ndugu mmoja tu bila familia yake kuhusishwa...

nahisi dada yako alifanya ulaghai ndio maana mahakamani ameshindwa kesi
 
N

niah

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2015
Messages
5,774
Points
2,000
N

niah

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2015
5,774 2,000

Je, msimamizi wa miradhi alikuwepo na je muuzaji hakuwa na ndugu zake na wakafanya kikao pamoja na mnunuzi kabla hawajaenda hata kwa mwanasheria kuanza michakato?

Utanununuaje nyumba ya familia kwa mtu mmoja bila kushirikisha ndugu zake?
 
F

FRESHMAN

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Messages
3,316
Points
2,000
F

FRESHMAN

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2011
3,316 2,000
watu wanakuwa wajanja wajanja ili wapate bei rahisi... wamemuona huyo jamaa ni mvuta bangi hana uelewa wa thamani za nyumba wakamlaghai awauzie nyumba kwa bei rahisi... ndugu zake wenye akili wameshtuka na kudai nyumba yao... mahakamani kweli wameonekana walaghai ... wanasema wamezulumiwa..

unazulumiwaje nyumba ambayo hata cement hujui ilijengwa kwa mfuko wa kiwanda gani?

jenga nyumba yako ndio uishi kwa amani.. au nunua kwa ushahidi ulionyooka

fisi 2

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Messages
1,795
Points
2,000
F

fisi 2

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2010
1,795 2,000
Ndio sababu inatakiwa kuwa na mtaalamu wa Ardhi kabla ya kununua wanasheria wao ni kuandaa documents tu. Huyo wakili hana Kosa wala lawama.
 
ISIS

ISIS

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2016
Messages
91,590
Points
2,000
ISIS

ISIS

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2016
91,590 2,000
watu wanakuwa wajanja wajanja ili wapate bei rahisi... wamemuona huyo jamaa ni mvuta bangi hana uelewa wa thamani za nyumba wakamlaghai awauzie nyumba kwa bei rahisi... ndugu zake wenye akili wameshtuka na kudai nyumba yao... mahakamani kweli wameonekana walaghai ... wanasema wamezulumiwa..

unazulumiwaje nyumba ambayo hata cement hujui ilijengwa kwa mfuko wa kiwanda gani?

jenga nyumba yako ndio uishi kwa amani.. au nunua kwa ushahidi ulionyooka
Muuzaji akiwa na power of attorney inayo mruhusu kuuza nyumba haitaji mtu yeyote mwingine
 
radika

radika

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Messages
17,395
Points
2,000
radika

radika

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2014
17,395 2,000
kwa nini ununue nyumba ya marehemu kwa ndugu mmoja tu bila familia yake kuhusishwa...

nahisi dada yako alifanya ulaghai ndio maana mahakamani ameshindwa kesi
Hiyo nyumba ilikuwa na hati aliyopewa muuzaji na ndio maana hapakuwa na mashaka
 
F

FRESHMAN

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Messages
3,316
Points
2,000
F

FRESHMAN

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2011
3,316 2,000
Muuzaji akiwa na power of attorney inayo mruhusu kuuza nyumba haitaji mtu yeyote mwingine
unaehisi huyo dada kwa nini ameshindwa kesi mahakamani na kuporwa nyumba?
 
N

niah

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2015
Messages
5,774
Points
2,000
N

niah

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2015
5,774 2,000
watu wanakuwa wajanja wajanja ili wapate bei rahisi... wamemuona huyo jamaa ni mvuta bangi hana uelewa wa thamani za nyumba wakamlaghai awauzie nyumba kwa bei rahisi... ndugu zake wenye akili wameshtuka na kudai nyumba yao... mahakamani kweli wameonekana walaghai ... wanasema wamezulumiwa..

unazulumiwaje nyumba ambayo hata cement hujui ilijengwa kwa mfuko wa kiwanda gani?

jenga nyumba yako ndio uishi kwa amani.. au nunua kwa ushahidi ulionyooka
Na muuzaji kapotea . Mh hapo sasa.
 
radika

radika

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Messages
17,395
Points
2,000
radika

radika

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2014
17,395 2,000
watu wanakuwa wajanja wajanja ili wapate bei rahisi... wamemuona huyo jamaa ni mvuta bangi hana uelewa wa thamani za nyumba wakamlaghai awauzie nyumba kwa bei rahisi... ndugu zake wenye akili wameshtuka na kudai nyumba yao... mahakamani kweli wameonekana walaghai ... wanasema wamezulumiwa..

unazulumiwaje nyumba ambayo hata cement hujui ilijengwa kwa mfuko wa kiwanda gani?

jenga nyumba yako ndio uishi kwa amani.. au nunua kwa ushahidi ulionyooka
Eti mvuta bangi

ndugu muuzaji alikuwa na vielelezo vyote ikiwemo hati miliki ya nyumba na ndio maana wakili alihusika na mwenyekiti wa serikali ya mtaa anamjua na alitoa maelezo ya yy ndo msimamizi hao wengine walikuwa hawaishi dodoma pia nyumba yenyewe ilikuwa ni pagala halikufikia hata level ya kupaua ni kama wao walinunua kiwanja wao wamijenga kuwa nyumba kamili

mkuu omba ufafanuzi ili wakat unaandika hayo upate picha kamali
 
Forum statistics

Threads 1,303,744
Members 501,077
Posts 31,490,832
Top